Picha:Freemasons wapo kila mahali lakini...

Picha:Freemasons wapo kila mahali lakini...

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,904
Usibweteke na uwepo wa Freemasons, wapo kila kona lakini hata hivyo vipo vikundi siri vingi sana visivyojulikana na tunaishi navyo kila siku....hawa ndio hatari zaidi kwani lengo lao ni baya na mwanadamu ni uwanjwa wao wa vita. Wachawi kwa mfano ni kikundi siri kikubwa pengine kuliko vyote vilivyopo duniani. Unaweza kuwa na mama, baba, kaka, dada, rafiki. mme, mke mchawi lakini usijue maisha yako yote! na wengi wetu ndivyo tuishivyo, ni kundi lenye usiri mzito mno na kuvujisha siri ni kujitakia hukumu ya kifo, na hukumu hii hutolewa kwa furaha sana na utelelezaji wake ni utii kwa mkuu wao.
upload_2017-8-16_20-57-32.jpeg


na alama zao zipo wazi na zina maana zilizofichika kwa mbiu kuu ya "kama ilivyo juu ndivyo ilivyo chini pia..." Hizi picha za karibu nimechukua wiki hii katika mji mmoja Africa
upload_2017-8-16_20-59-24.jpeg
 
Sijui kwanini aijawahi kuamini kufungamana kwa Freemasons na mambo ya kiimani...[emoji45] [emoji45]
 
Sasa hilo jumba mbona hamna hata mtu anaingia?? Kuna haja gani kutuonesha jumba bila mlango wazi?
 
Funguka kwa undani tukuelewe,, maana nahisi kama kuna mengi ya kujifunza kutoka kwako,,
 
Funguka kwa undani tukuelewe,, maana nahisi kama kuna mengi ya kujifunza kutoka kwako,,
Dunia hii ina ule upande unaonekana kwa macho ya kawaida na upande ule usioonekana isipokuwa kwa njia ya kiroho pekee yake. Ajabu ni kwamba mambo yasiyoonekana ndiyo mengi na yana nguvu zaidi ya yale yanayoonekana. Wenye kujua siri hii ndio wanaotawala na wale wasiojua ndio wanaotawaliwa. Kujua hakutoshi, unapaswa kujua pia namna ya kutenda katika roho.
 
Back
Top Bottom