PICHA: Dr. Slaa atoa pole kwa familia ya marehemu Mwangosi

DAMU ISIYO NA HATIA, HAITOMWAGIKA BURE
IKIWA SOTE TULIUMBWA NA MUNGU, hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mwingine
DAMU YA MWANGOSI I JUU YA VICHWA VYA CCM SASA NA HATA MILELE, MUNGU WA KISASI, ATAMLIPIA MWANGOSI HAPAHAPA DUNIANI
MUNGU SI MWANADAMU HATA ADHIHAKIWE KATIKA SHERIA ZAKE, YEYE AMESEMA, AUAYE KWA UPANGA, ATAKUFA KWA UPANGA, NA LAANA YAKE I JUU YAKE MPAKA KIZAZI CHA SABA
REST IN PEACE THE HERO, DAUDI MWANGOSI
 
a9.jpg


Mti huu ni kumbukumbu kwamba umetutoka kimwili lakini ungali nasi kiroho hadi tutakapoungana nawe katika makazi ya Baba wa milele.

6.jpg


07.jpg

Dr. Slaa alipofika kwenye msiba wa familia ya hayati Daud Mwangosi kuwapo pole.

06.jpg


Mjane wa Daud Mwangosi, ameacha mjane na watoto wanne.

a1.jpg


Mtoto wa hayati Daud Mwangosi akimsalimia Dr. Slaa kwa uchungu alipofika kuwapa pole.

Picha kwa hisani ya Mjengwa blog

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Umetangulia mbele ya haki na sisi tunakuja nyuma yako. RIP Kamanda.
 
Candid scope;
Alieyefurahia umwagaji damu huu ni Dr. Slaa peke yake! Yeye ndiye aliushinikiza kwa manufaa yake kisiasa, ufungamane usifungamane huo ni mpango wako ukweli; huyo maseiah wenu ndiye kinara wa vurugu hizi, kabla hamjajiingiza kwenye huo ukombozi angalieni familia zenu zinazowategemea, Nyerere alishapigania uhuru wa nchi hii mabadiliko yanaweza kufanyika bila vurugu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Chama
Gongo la mboto DSM,
KuLiko Rais wetu anavyopenda mambo ya kumwaga damu na visasi angalia jinsi alivyokuwa anataka kumjeruhi prof mahalu achilia mbali dr ulimboka na babu seya
 
DAMU ISIYO NA HATIA, HAITOMWAGIKA BURE
IKIWA SOTE TULIUMBWA NA MUNGU, hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mwingine
DAMU YA MWANGOSI I JUU YA VICHWA VYA CCM SASA NA HATA MILELE, MUNGU WA KISASI, ATAMLIPIA MWANGOSI HAPAHAPA DUNIANI
MUNGU SI MWANADAMU HATA ADHIHAKIWE KATIKA SHERIA ZAKE, YEYE AMESEMA, AUAYE KWA UPANGA, ATAKUFA KWA UPANGA, NA LAANA YAKE I JUU YAKE MPAKA KIZAZI CHA SABA
REST IN PEACE THE HERO, DAUDI MWANGOSI

Amina!
 

a1.jpg


Mtoto wa hayati Daud Mwangosi akimsalimia Dr. Slaa kwa uchungu alipofika kuwapa pole.

Picha kwa hisani ya Mjengwa blog
Mtoto kama huyu hawezi kusahau kilichomtokea mzazi wake na hata waliotenda mabaya juu yake,mungu ampe nguvu kijana huyu ili aweze kuwa kiongozi wa nchi hii na afanye kile alichofanyiwa baba yake angali akiwa mdogo
 
KuLiko Rais wetu anavyopenda mambo ya kumwaga damu na visasi angalia jinsi alivyokuwa anataka kumjeruhi prof mahalu achilia mbali dr ulimboka na babu seya

Kamanda Precise Pangolin
Kwanza nitumie vipimo na saizi ya viatu nataka nikutumi pamba ya nguvu; na boot kali upendeze achana na kakhi za kushonesha kwa fundi John; makamanda hamuelweleki serikali ikiwashtaki wahujumu uchumi kelele isiposhtaki kelele, na kuhakikishia kama raisi angetaka Mahalu awe jela leo hii angekuwa jela, lakini ni kwasababu ni mtu anayeheshimu misingi ya demokrasia.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Chadema kama chama wachukuweni hao watoto muwasomeshe mpaka chuo kikuu, pamoja na kumuangalia mjane, mzazi wao kafa ndani ya harakati za kisiasa za Chadema

Umekosea!! Alikuwa akitimiza majukumu yake kama mwandishi,hivi yule polisi naye akifa uta demand cdm imgharimie?
 
Mkuu Ritz
Angalia picha utaona wenye majonzi ya kweli na wanafiki waliokwenda kutafuta picha za magazeti; Dr. Slaa anaona hata aibu kuingalia kamera kwasababu ya dhambi unafiki inamsuta, masikini kama watoto uyatima kwa tamaa za kisiasa inasikitisha sana. R.I.P Mwangosi

Chama
Gongo la mboto DSM
Aisee!

:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:..............:mvutaji::mvutaji:........:confused3:
 
Policcm ndio wenye huruma?
Watu wanajijenga kisiasa kwa kupitia maafa ya wenzao, hii yote ni show tu, Slaa hana huruma na hiyo familia. Anapita hapo, anapigwa picha halafu anasahau yote. Tatizo lenu hamjui tabia ya wanasiasa. Yule kijana wa moro ilikuwaje? ahadi kibao lakini hakuna msaaada wowote kutoka CDM zaidi ya longo longo.
 
Hata kama watauwa watu wote walio ndani ya harakati naamini watazaliwa wengine watakao endeleza harakati na kustawisha mbegu ya mabadiliko.

Mabadiliko yangekuwa yanazuilika kwa mtutu wa bunduki hosein mubarak angefaulu na sasa angekuwa yu ngali madarakani. Ifike hatua ccm wajue kuwa kuwatumia polisi waue hakuta weza kuwaokoa na anguko maana hasira ndio zinazidi kwa wananchi wa kawaida. Huyo mtoto wa marehemu pamoja na mama yake naamini hawawezi kupigia kura serikali iliyo uwa kiongozi wa nyumba (baba).
 
Jeshi letu la polisi limefikia mahala pabaya mno linadiriki kumua kikatili mwandishi wa habari asiye na hatia mbele ya waandishi wenzie, mbele ya camera, mbele ya wananchi mbele ya RPC tena mchana kweupe...kwa hali hii unahitaji kuwa na ya akili ya kijuha kukanusha kuwa hawakumfanyia ukatili na unyama Dk. Ulimboka.
 
Nikiropoka yaliyopo moyoni yaweza yakachochea uvunjifu wa amani...ila chuki niliyonayo dhidi ya polis haina kipimo...Polis wameua.....Mungu angalia damu ya Mwangosi inavyokulilia...Mungu walipe walichopanda
 
Maomivu yakizidi furaha imekaribia,ccm zama zenu zimekwisha jiandaeni kuwa chama cha upinzani.
 
Hivi hizi rambi rambi za CDM zimekakaaje? mbona muuza magazeti wa Moro hata ubani chama hakikutoa zaidi ya kushuhudia party after maandamano kwa mchungaji Msigwa makamanda na toothpicks wakijichokonoa mbuzi.
 
Back
Top Bottom