Picha: DK. Slaa aivuruga CCM Ruvuma

Picha: DK. Slaa aivuruga CCM Ruvuma

Unaonekana dhahiri unatumika vibaya na macdm, umekunywa sumu ya m4c hadi ukaathrika ubongo. Endelea kushabikia kwenye hamna, aibu kuu inakuja 2015. Siasa za kujaza watu mkutanoni halafu ukavimba kichwa kuwa nakubalika hazitoi taswira sahihi. Muulize Mrema na Mtikira hawa waliwahi kujaza watu misili ya sisimizi, Mwisho wa siku chali.
asante kwa ujumbe unaolingana na ubongo wako, hebu tuma salaam kwa watu watatu ukianza na prof. Anna Tibaijuka MB, anayetembea na masufuria ya pilao ili mikutano yake 'ipendeze' masisiem yametuharibia prof. wetu jamani!
 
kuna chama kinanichesha sana.
Baba waziri wa fedha mwana naibu waziri wa fedha.Malima
Baba katibu mkuu wa chama mtoto naobi waziri wa mawasiliano. Makamba
Baba Rais TZ mtoto waziri wa ulinzi. Mwinyi.
Baba rais Zanzibar, mtoto Raiswa Zanzibar. Karume. Just few to mention. Mnatarajia nchi hii itatoka na uongozi huu wa kifamilia?. Chadema Mungu azidi kuwapa mbinu nyingi Taanzania imechoka.
 
kuna chama kinanichesha sana.
Baba waziri wa fedha mwana naibu waziri wa fedha.Malima
Baba katibu mkuu wa chama mtoto naobi waziri wa mawasiliano. Makamba
Baba Rais TZ mtoto waziri wa ulinzi. Mwinyi.
Baba rais Zanzibar, mtoto Raiswa Zanzibar. Karume. Just few to mention. Mnatarajia nchi hii itatoka na uongozi huu wa kifamilia?. Chadema Mungu azidi kuwapa mbinu nyingi Taanzania imechoka.
 
Songea/Tanga. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema kuwa chama hicho kitachukua uamuzi mgumu ikiwa wabunge wa CCM watajikita katika kulinda masilahi yao kwenye Bunge Maalumu la Katiba kinyume na maoni ya wananchi.Alisema hayo jana katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga kwenye siku ya kwanza ya Operesheni Pamoja Daima. Katika operesheni hiyo, ambapo aliruka kwa helikopta katika sehemu mbalimbali, alihutubia mikutano katika maeneo ya Mbamba Bay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo na Songea Mjini.

Akiongozana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Dk Slaa aliwaonya wabunge wa CCM kutotumia wingi wao bungeni kutetea masilahi ya chama chao. "Kamwe wasithubutu kwani Chadema itachukua uamuzi mgumu ambao kwa sasa si vizuri kuutaja," alisema Slaa.

Alionya akisema ni lazima wabunge watoe maoni ambayo yana masilahi ya wananchi wote na siyo vyama.

Daftari la wapigakura

Katika hatua nyingine, alisema Chadema itasusia kura ya maoni iwapo daftari la wapiga kura halitaboreshwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba.

Alisema kwa sasa chama hicho kinasambaza fomu maalumu nchi nzima kwa ajili ya watu wasio na vitambulisho vya kupiga kura wajiorodheshe.

"Kuna maelfu ya watu waliopoteza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wengine wamefikia umri wa kupiga kura lakini Serikali haioni suala hilo kuwa ni muhimu," alisema.

Alisema uchunguzi wa chama hicho umebaini watu zaidi ya 5,000,000 hawana vitambulisho vya kupigia kura japokuwa tayari wamefikia umri wa kupiga kura.

Ili kuhakikisha Bunge la Katiba linakuwa na manufaa, Dk Slaa aliwataka wananchi kufuatilia mjadala juu ya Katiba Mpya kwa makini ili kuwabaini wabunge wasioitakia nchi hii mema.

Alisema wabunge wa namna hiyo wamepanga kutengeneza Katiba ya viongozi badala ya katiba ya wananchi.

Baadaye katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Matarawe mjini Songea mvua kubwa ilinyesha, lakini wananchi waliofurika hawakujali kunyeshewa badala yake walionyesha shauku ya kuendelea kumsikiliza Dk Slaa.Mawaziri Mizigo
Kwa upande wake, Msigwa alisema CCM wana deni la kujieleza mbele ya wananchi kwa sababu walitangaza mawaziri mizigo lakini Rais Jakaya Kikwete bado ameendelea kuwaweka kwenye Baraza la Mawaziri.

"Kinana (Abdulrahman, Katibu Mkuu wa CCM) na Nape (Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi) walikuja kwenu na kutaja majina ya mawaziri mizigo, walikuwa wanadanganya, si mnaona wale waliowataja wameteuliwa tena? Chama hicho siyo makini," alisema Msigwa.

Alidai kuwa kwa sasa CCM imegawanyika na kila kiongozi anatoa kauli yake kulingana na anavyojisikia na wala hazingatii vikao.

Alisema mparaganyiko uliopo ndani ya CCM kwa sasa ndio utakaosaidia Chadema kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

‘Washambulia' Tanga

Naye, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu akisindikizwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana Chadema, John Heche, Katibu wa Vijana, Deo Munisi na Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa ‘walishambulia' baadhi ya wilaya za Mkoa wa Tanga.

Lissu alifanya mikutano katika Wilaya za Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga huku wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kuharakisha mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

"Rais Kikwete alipokea Rasimu ya Pili ya Katiba, lakini katika mazungumzo yake mbalimbali hakuzungumzia mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura...Serikali iharakishe maboresho, kwani litakapokuja suala la kura ya maoni wengi watashindwa kupiga kura.

"Na kilio cha wananchi kitaonekana itakapotokea wakashindwa kupiga kura," alisema Lissu, ambaye akiwa Wilaya ya Tanga, alifanya mikutano katika Kijiji cha Lwanda, Kata ya Kiomoni ambako Mwanaisha Omari anawania udiwani wa kata hiyo.

Source; MWANANCHI
 
kuna chama kinanichesha sana.
Baba waziri wa fedha mwana naibu waziri wa fedha.Malima
Baba katibu mkuu wa chama mtoto naobi waziri wa mawasiliano. Makamba
Baba Rais TZ mtoto waziri wa ulinzi. Mwinyi.
Baba rais Zanzibar, mtoto Raiswa Zanzibar. Karume. Just few to mention. Mnatarajia nchi hii itatoka na uongozi huu wa kifamilia?. Chadema Mungu azidi kuwapa mbinu nyingi Taanzania imechoka.
Sio bure utakuwa msukule,hivi Mbowe na Mtei wanamhusiano gani? lakini Slaa na Rose kamili walishawahi kuwa nani vile? kabla hatujaangalia familia ya Ndesamburo wala Lissu ndani ya CDM na ile nyumba ndogo ya mzee wa Dubai mama FreeLady
 
Vijana ndio watakomboa taifa hili,,tusisahau kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la wapiga kura mda ukiwadia
 
Sio bure utakuwa msukule,hivi Mbowe na Mtei wanamhusiano gani? lakini Slaa na Rose kamili walishawahi kuwa nani vile? kabla hatujaangalia familia ya Ndesamburo wala Lissu ndani ya CDM na ile nyumba ndogo ya mzee wa Dubai mama FreeLady
yOUR OPINIONS ARE ALWAYS NONSENSE!!
 
Jamani mlio karibu na timu ya mh slaa mwambieni afike jimboni peramiho kummaliza yule waziri wa diploma ya uualimu,kule hakubaliki.
Peoples'''''''''''''''
 
safi sana cdm hakuna kulala naona mzee wa usingizi kanda ya ziwa kaanza kuogopa kivuli chake
 
Wapi wapi yule muuza migebuka Zitto Zuberi Kabwe aka ZZK anayejiona ni maarufu kuliko chama; wapambe wake mwambieni atakufa yeye; CDM ni moto chini mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom