PICHA: Compare and contrast - Mwanza and Morgoro

daah, aibu sana kwa chama tawala kua na wa2 wachache hivyo,bila wasanii na buku 5 tano watu waliopewa kuudhuria hapo wasingemuona m2.../
RIP CCM 2015
 
Diamond angepewa ukatibu mkuu wa ccm kwani ameshangiliwa kuliko hata mgeni Rasmi Bw.KINANA
 

Pale tulikaa tukisikiliza
Wenye udadisi waliuliza
Kwa kuwa mengi yalituliza
Ni vigumu kueleza

Miili ilitusisimka
Uwanja ulichangamka
Tulisimama tuliamka
Kwa ari isiyomithilika

Saa ya ukombozi ni sasa
Tunawaka kwa msasa
Kamwe hatuwezi susa
Pamoja na vyao visa

Yu pamoja nasi
 

Umeongea fact mkuu!!
 
Ule wa Mwanza ulihudhuriwa na watanzania wakati pale Morogoro walikuwepo wanaCCM. Kwa maneno mengine kule Mwanza wahudhuriaji walijialika, wakati kule Moro wahudhuriaji walialikwa wakambiwa na mavazi yawapasayo kuvaa.
 

Namba 5: walioenda mkutano wa ccm walienda kucheck show
 

Si unafiki ila ni ukweli wangu huwa napenda sana kupata michango ya Sumu, Chili, Zemarco, Bungeni, Utaifa kwenza, na wengineo ambao siwezi kuorodhesha wote list ndefu sana. jamani wako wapi mbona siwaoni?. Au TCRA wamekata mawasiliano? Hebu nisaidieni mwenzenu siwezi lala bila kuona michango yenu.
 
hivi katibu mkuu wa chadema alikuwepo mwanza?
Katibu mkuu yuko Dodoma. Mwanza yupo Lissu na wabunge wenzake walionyimwa haki yao bungeni. Sijui katibu mkuu angekuwepo Mwanza ingekuwaje. Nimeiskia hotuba ya Kinana online ingawa ilikuwa inakata sana. Sasa hivi wako defensive. hawana hoja, na hiyo ni a political plus for CDM, endeleeni kuwa offensive, they'll throw the towel.
 
hapo umenena mkuu mana hata shetani ataitwa mradi anaongeza mtaji. sijui huyomsanii kabanwa na choo kibwa!
 
Hapo Kwa CCM ni show ya Diamond au mkutano wa CCM?, Uenda watu walivutiwa na Diamond
 
Hivi mwanadiwani nikuulize kitu kidogo, hizi picha zenye watu wamevaa nguo za kijani walikuwa wanatengeneza video ya wimbo gani wa Diamond?
 
domo dimond kumbe ni Gamba.

Dogo kwa Domo sijui kama kuna Mtanzania anaemfikia! Nadhani ikianzishwa mashindano ya Wenye Midomo Mikubwa Duniani huyu Diamonddomo atashinda na kutuletea Medali ya Dhahabu!!

Huyu Dogo anachofanya kitakuja kumgarimu,! kukubali kwake kutumiwa na Chama na Serikali inayoibia wanachi Kukusanya watoto wetu ktk Mikutano ya siasa, ili ionekane kwamba Watanzania bado wana Imani na Wezi hawa wa Mali za Umma ni Dhambi itakayo mtafuna yeye na Kizazi chake kuanzia Uzao wa kwanza hadi wa Nne!!

Ktk Biblia Takatifu Mungu anasema kwamba Usivisujudie wala Kuvitumikia kwa kuwa mimi ni Bwana Mungu wako,ni Mungu mwenye Wivu Nawapatiliza Wana "MAOVU"ya baba zao! Hata Kizazi cha tatu na cha Nne cha wanichukizao!

Swala la Mkutano upi umejaza watu, hilo sio jambo la kuzungumzia kwani Upande mmoja uwanja ulijazwa na watoto walioenda kuangalia Shoo ya DOMO DIAMOND!! Na wenzake wengine wa Mipasho!!
lakini pia Waliokua watu wazima ni wale waliopewa buku daladala na Sharti ya kuvaa Yale Masare yao yaliyonifanya kuacha siku hizi kula Mboga za Majani kwa ajili ya Ukijani!!

Upande wa pili pamoja na kuwa hakukuwepo na Kina Domo diamond, lakini uwanja ulitapika ......na wazungumzaji walikua ni wabunge tu! Wakati wenzao wazungumzaji walikua Viongozi wakuu wa Chama!!

Hii ndio picha halisi kwamba Safari ya Kumuondoa Mkoloni Mweusi[CCM] inakaribia mwisho!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…