Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Wiyau

Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
17
Reaction score
45
Ilitokea ghafla katika barabara ya Makongolosi kuelekea Rungwa mkoani Mbeya. Ghafla kwenye kona mnyama simba kakutwa kajipumzisha katikati ya barabara eneo la pori la simba.

Wakati magari yakiwa yamesimama, mara Bodaboda akatokea na bila kujua akataka kuyapita kwa kasi (kuchepuka) ndipo alipokutana uso kwa uso na mnyama huyo hatari. Hata hivyo aliweza kugeuka na kukimbia wakati na simba naye akanyanyuka na kuingia porini.


Simba na Boda Boda 1.jpg Simba na Boda Boda 2.jpg Simba na Boda Boda 3.jpg
 
Da nimecheka sana kwi kwi kwi kwi kwi na hapo inaonekana hawa jamaa kwenye gari walimuonya asimame ila kwa akili za boda boda angejalibu kupita hapa alafu mziki wake angeuona.

Kuna siku tulikua ngorongoro sasa simba walikua wamelala barabarani jamaa mmoja na landcruiser yake alamkanyaga mkia simba mmoja da chamoto alikiona cruiser ilipigwa kofi moja mlango wote kwisha ha ha ha ha
 
Hapa ningekuwa mimi ningezimia aisee maana muoga kinyama, mnyama mwenyewe simba!! Nilishawahi kukutana na kitimoto pori asubuhi asubuhi saa 12 wakati nakusanya kuni za kupika chai,

siku hiyo nakumbuka miguu iliishiwa nguvu nikaanguka chini bahati nzuri nilikuwa na ba'mdogo wangu akapiga ukunga ndio noah akasepa.
 
dah aisee fanya umtumie iyo maana alikuwa anacheza na kifo kweupee
 
Hizi pikipiki za kichina huwa zinazimaga ghafla..! halafu ukipiga kick zinagoma for no apparent reason..! bahati yake halikutokea hilo.., angevunja kioo cha gari lako ajifiche humo..! ahahahahahahah..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom