Picha: Balozi kallaghe awawaaga wanariadha wetu kwa matumaini ya olimpiki 2016

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mh+Balozi+akibadilishana+mawazo+na+wageni+waalikwa.jpg


Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau wa Michezo aliowaalika ubalozini hapo wakati wa kuiga timu ya Tanzania ya Olimpiki.

Mambo+ya+msosi.jpg

Msosi wa nguvu mezani.

Mh Balozi akikabidhiwa tuzo maalum na mkuu wa msafara Hassan Jarufu iliyotoka katika kamati ya Michezo ya Olimpiki.

Mwanariadha Zakia Mrisho akiongea machache na waandishi wa habari.



Selemani Kidunda, Frank Eyembe na Zakia Mrisho wakila pozi.



wakati wa kubadilishana mawazo .


Mh Balozi na maafisa wa ubalozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo, wasaidizi wa Olimpiki pamoja na makocha wao.

Na Freddy Macha

Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe amewapongeza wanamichezo wetu walioiwakilisha nchi katika Olimpiki kwa nidhamu ya hali ya juu na kuwataka wasivunjike moyo kwani sio sisi tu tuliokosa medali.

“Wanamichezo wetu wameonyesha tabia bora kinyume na watu wa nchi nyingine waliofanya mambo ya aibu sana. Lazima tuwapongeze kwa kufikia viwango na kuibeba bendera ya Tanzania,”alisema.

Akiongea katika tafrija ndogo kuwaaga wanamichezo saba, maofisa na makocha wao, Balozi Kallaghe alisisitiza kwamba tusiwalaumu wanamichezo kwa kushindwa kwani kuna mataifa mengi yaliyokosa medali.

Tafrija hiyo ilihudhuhuriwa na maofisa wote wa Ubalozi, wanahabari London na Balozi wa Rwanda Uingereza, mheshimiwa Ernest Rwamucyo.


Kitakwimu ni asili mia kumi tu ya washiriki 10,500 waliocheza michezo 26 (toka mataifa 204) wakapata medali. “Kuna mataifa tajiri kama Ujerumani, Australia na India ambayo hayakufanya vizuri na pia wenzetu Afrika mfano Kenya na Ethiopia ambao hawakuridhika au kufikia nafasi waliyozoea miaka iliyopita.”

Balozi aliitaja nchi ya Wafilipino (Philippines) yenye watu Milioni 93 ambayo ilikuwa na wachezaji 11 na haikuambulia kitu.

Kidesturi toka 1936, Wafilipino wamekuwa wakishinda medali katika mchezo wa ngumi.“Lazima tujiulize maswali ili kufanikiwa mashindano yajayo na kujitayarisha ndiyo msingi.

Vipaji vingi vipo Tanzania. Tujaribu kuangalia na kujiuliza wapi vilipo vianzio vya kuendeleza michezo yetu kutoka ngazi za chini maana uwezo wa kushinda tunao. ”


Akipigiwa makofi balozi alimtaja mkimbiaji maarufu wa Uingereza mwenye asili ya Kisomali, Mohammed “Mo” Farah aliyefanya vibaya sana Olimpiki ya 2008, China. “Baada ya kushindwa kabisa Beijing, Mo Farah alijilaumu na kulia sana; ila hakuvunjika moyo; alirudi akajiandaa vizuri na matokeo yake mwaka huu kashinda medali mbili za dhahabu.”

Naye mkuu wa msafara Bwana Hassan Jarufu aliushukuru ubalozi wetu Uingereza kwa ukaribisho mzuri uliohakikisha kwamba wanamichezo wako sawa toka walipowasili hapa majuma mawili kabla ya Olimpiki. Aliwataja pia wasaidizi wenyeji wa Uingereza, Alison Cochrane, Steve Wiseall na Lesley Shayler aliyewahi kuitembelea Bongo na kuipenda sana.“Hawa wamekuwa wenyeji wetu wazuri sana,” alisema.

Bwana Jarufu alifahamisha kwamba wanamichezo wetu shurti kupongezwa kwa kujitahidi kufanya shughuli hii bila ajira au kazi maalum.

“Kwa mfano wakimbiaji wa mbio za marathon wanatakiwa kiafya wakimbie mara nne tu kwa mwaka kusudi wawe tayari kwa mashindano makubwa, lakini kutokana na kukosa ajira au msaada wa kifedha wanalazimika kushindana mara nyingi zaidi ili waishi.

Na si ajabu ukamsikia mmoja mmoja akilalamika kashindwa mashindano makubwa kama Olimpiki kutokana na majeruhi fulani mwilini.”


Katika michuano ya siku ya mwisho Jumapili wanariadha watatu, Faustin Mussa, Samson Ramadhan na Mohammed Msondiki Ikoki walishiriki mbio za marathon na hawakupata medali yeyote. Mshindi alitoka Uganda Stephen Kiprotich akifuatiwa na Wakenya: Abel Kirui na Wilson Kiprotich.


Posted by MUHIDIN MICHUZI at Tuesday, August 14, 2012




 

Na Bado Nchi inawafanyia Bye Bye Party; Mtu aliyefanya Vizuri ni Zakia Mrisho aliyeshika nafasi ya 66; aibu aibu

wanaogopa kufanya Mazoezi Hanang sehemu zenye baridi kama Wakenya na Waganda... Wanafanyia Dar...

Hatutafika kokote Angalia hilo kundi; Maboxer hawajui style za kupata points wanaondolewa kirahisi; na Vijapani

Vyembamba, Vitanzania Vinaonekana Vikubwa lakini Vijapani vinajua how to get the points ni aibu unaangalia mpaka

Unataka kuivunja hiyo television yako; hawa viongozi wetu hawayajui haya? Wana Madegree Au ukisha kaa kwenye

desk hapo wizarani nchini basi unasahau kila kitu? Kulikuwa na Boxing ya Wanawake sijui kwanini hawakuleta Wanawake

Wetu...
 
hawa masifuri hata mimi mbio hawaniwezi....hawa hata kufukuza kuku tu wanaweza kushindwa....sijui wanakula kitimoto au ndo midebwedo!wanakera kweli, bora hata wasingeenda kuliko kwenda afu wanatuletea fezea.....uganda kuna gold, kenya ndo usiseme....tz mkia.
 
Wa marathon walifanya vizuri no. 33 na 66, hiyo namba 33 ni nzuri sana msione hivyo dakika 9 tu nyuma ya mshindi, nadhani tukijipanga vizuri katika selection tunaweza tukapeleka watu wengi Brazil hasa kwenye michezo mingine tusinganganie kukimbia na boxing tu.
 
Watalii,
How is London, kuna joto au baridi?
mvua inanyesha?
aisee karibu sana.
 
Hizo Kamba zinazonin'inia shingoni nilifikiri ni medali, kumbe vitambulisho vya Olympic! WaTanzania hatujitambui. Halafu wanafanyiwa party ya nini!? Kesho tutaletewa Invoice kutoka ubalozini kwamba hiyo party iligharimu £ 30,000.
Daah! Inauma kuwa MTANZANIA.
 
Ninaungana na Watanzania wenzagu katika kuvunjika moyo na matokeo ya wanamichezo wetu kwenye mashindano ya kimataifa - Inakera sana. Lakini tukumbuke kuwa hata kama Tanzania itaendelea "kunyolewa" katika fani zote za michezo, bado michezo duniani itaendelea na vizazi vyetu vitaendelea kuwapo. Kwa hivyo, pamoja na kulaumu ambako ni haki yetu, ningependa tujadili pia kwa kujenga juu ya hali ya michezo nchini, kwa kuzingatia (baadhi ya) yafuatayo:
1. Tunakosea wapi? 2. Tufanye nini?
Kwa kufanya hivyo, hata kama mawazo na ushauri wetu utakuwa kama kumpigia mbuzi gitaa, lakini pengine ipo siku wahusika wakayaona na kuyatumia. Tusilaumu tu, tupendekeze pia nini cha kufanya, tutakuwa tumekitendea haki kizazi chetu.

Baadhi ya wadau wa michezo nchini wameto maoni yao kwenye makala hii hapa, na wewe ninakukaribisha utoe maoni yako:
Tanzania iahirishe kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa, wachambuzi wa michezo wasema
Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Agosti 14, 2012
Tanzania inapaswa kuchukua mapumziko ya muda na kusitisha ushiriki wake katika Michezo ya Olimpiki ili kukiandaa kwa ufanisi kizazi kipya kijacho cha wanamichezo, wachambuzi wa michezo wasema.
tanzania-olympic-london-340_227.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe (wa katikati mwenye suti) akiwa na wawakilishi wa Tanzania wa Michezo ya Olimpiki ya London 2012. [Picha kwa heshima ya Kamati ya Olimpiki ya Tanzania]

Katika michezo ya Olimpiki ya London, iliyomalizika Jumapili (tarehe 12 Agosti), wanariadha saba wa Tanzania waliiwakilisha Tanzania, na hakuna hata mmoja aliyeshinda medali. Tanzania imeshinda medali mbili katika mashindano ya Olimpiki, zote huko Moscow mwaka 1980.

Faustine Mussa na Samson Ramadhani walishiriki katika mbio za marathoni za wanaume lakini walishindwa kupanda jukwaa la zawadi. Mussa alimaliza nafasi ya 33 alitumia muda wa saa 2, dakika 17 na sekunde 39, wakati Ramadhani alimaliza wa 66 kwa muda wa saa 2 dakika 24, sekunde 53. Mwanamarathoni wa tatu, Mohamed Ikoki Msandeki, alijitoa kwenye mashindano siku moja, kwa kusema alikuwa mgonjwa.

Mkimbiaji wa mbio za kati Zakia Mrisho alimaliza wa 16 katika mbio za mita 5,000 kwa kutumia muda wa dakika 15 na sekunde 39.58. Naye mwogeleaji Ammaar Ghadiyali alitokea wa tatu katika kundi lake na mwogeleaji Magdalena Moshi alitokea wa 7 katika kundi , lakini wote walishindwa kuendelea zaidi. Bondia Suleiman Kidunda alipoteza raundi zote tatu kwenye mashindano ya uzito wa wastani.

Matayarisho mabovu na ukosefu wa uongozi
Mwandishi wa habari za michezo Grace Hoka anasema michezo ya Tanzania inahitaji kugeuzwa kabisa kiasi kwamba serikali ingesitisha ushiriki wa kimataifa katika michezo yote kwa muda wa amiaka 10 ili kukuza michezo ipasavyo nchini na kutoa mafunzo makubwa kwa wanariadha wenye kuleta matumaini.
"Tunapaswa kuzifumua timu zote za taifa, mashirika yote ya michezo ya taifa na kila kitu kinachohusiana na michezo na kuanza kuwafunza watoto wadogo. Baada ya miaka 10, tutakuwa na timu nzuri kuliko wakati wowote," Hoka aliiambia Sabahi.

Anasema matayarisho mabovu ya wanariadha na ukosefu wa uongozi kutoka kwa mameneja katika mashirika ya michezo ndio sababu kubwa ya utendaji wa Tanzania wa kuvunja moyo katika michezo ya Olimpiki mwaka huu.
Anasema serikali ingechukua uongozi kutoka mashirika ya michezo, hata kama ni kwa muda, kama ilivyofanya kwa timu ya taifa ya mpira tangu mwaka 2007.

Zaidi ya hayo, alisema hata kama itakuwa ghali zaidi, wakimbiaji wa marathoni wanapaswa kufanya mazoezi huko Arusha au Mbeya, ambako kuna mwinuko wa juu kuliko ilivyo Dar es Salaam.

Wanamichezo wa Tanzania wanaonekana wenye akili za kushiriki tu katika michezo ya Olimpiki, na wala sio kushinda, anasema Cyprian Maro, mkuu wa elimu ya viungo na sayansi ya michezo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
"Nadhani suluhisho pekee ni kuzigeuza mashirika ya michezo, kuwapatia mafunzo kizazi kipya na kurejea kujiunga tena na mashindano ya kimataifa baada ya miaka nane," Maro aliiambia Sabahi.

Maro alisema serikali imejaribu kuipiga jeki michezo kupitia mabadiliko ya sera.

Mwaka 2008, serikali ilirejesha michezo katika mtaala wa shule za umma, baada ya kuusimamisha mwaka 1990. Pia inagharimia programu za maalumu za miaka miwili katika vyuo 11 kuandaa walimu wa elimu ya viungo na makocha katika shule za sekondari. Shule za umma huajiri wahitimu kutoka mpango wa mafunzo mara moja baada ya wao kupata mafunzo ya stashahada.

Hata hivyo, juhudi hizi hazioneshi kwa mafanikio ya timu kwa sababu mashirika ya michezo, kama vile Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) na Chama cha Wanariadha cha Tanzania, hawasimamii vyema mafunzo ya wanamichezo.
Maro alisema mashirika ya michezo pia yanahitaji kupewa mafunzo ili kuwa na stadi zinazofaa za uendeshaji.
"Uwezo wa viongozi wa mashirika ya michezo ni mdogo sana," aliiambia Sabahi. "Wanaweza wakaweka rekodi za riadha na masumbwi, lakini hii haitoshi. Lazima wawe na uwezo wa kuandika mapendekezo ya gharama na kupanga michezo, badala ya kungojea serikali."

Msaada zaidi wa serikali uhitajika
Katibu Mkuu wa TOC Juma Ikangaa, mshindi wa medali ya fedha katika marathoni ya Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 1982, aliilaumu serikali kwa kutowekeza katika michezo, na kusema kuwa mengi yanahitajika kufanywa ikiwa Tanzania ina ndoto za mafanikio.

Alisema serikali haitoi msaada unaohitajika kwa TOC ili kuwatayarisha wanariadha kwa viwango vinavyokubalika.
"Hatuwezi kuwa na programu bila ya pesa. [Kambi za mafunzo zinahitaji] pesa na hizi lazima zitoke serikalini kama ilivyo kwa nchi nyengine," Ikangaa alisema.

Alisema wafadhili watakuja mara pale michezo yatakuwa na mafanikio , kwa hivyo serikali inahitaji kuwekeza mtaji wa awali.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Amos Makala alielezea majuto ya serikali kwa utendaji wa wanariadha wa Tanzania katika Olimpiki, lakini aliwahamasisha Watanzania kucheza michezo zaidi ili kuwa na fursa bora kwenye michezo siku za usoni.

"Bila ya shaka, matokeo ni mabaya, lakini hatupaswi kuvunjika moyo," Makala aliiambia Sabahi. "Tujipange ili kushiriki katika michezo mingi zaidi kuliko tulivyofanya mara hii. Tujaribu michezo mengine zaidi ya riadha, kuogelea na ndondi."
Makala alisema Watanzania wana vipaji na wanaweza kufanya vizuri zaidi katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 huko Brazili ikiwa watafanya mafunzo na ikiwa TOC itapangwa bora zaidi.

"Ninawataka Waanzania wawe wabunifu ili kuweza kupata medali zaidi katika michezo ijayo," alisema. [Chanzo: Tanzania iahirishe kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa, wachambuzi wa michezo wasema - Sabahionline.com
 

Na Bado Nchi inawafanyia Bye Bye Party; Mtu aliyefanya Vizuri ni Zakia Mrisho aliyeshika nafasi ya 66; aibu aibu

wanaogopa kufanya Mazoezi Hanang sehemu zenye baridi kama Wakenya na Waganda... Wanafanyia Dar...

Hatutafika kokote Angalia hilo kundi; Maboxer hawajui style za kupata points wanaondolewa kirahisi; na Vijapani

Vyembamba, Vitanzania Vinaonekana Vikubwa lakini Vijapani vinajua how to get the points ni aibu unaangalia mpaka

Unataka kuivunja hiyo television yako; hawa viongozi wetu hawayajui haya? Wana Madegree Au ukisha kaa kwenye

desk hapo wizarani nchini basi unasahau kila kitu? Kulikuwa na Boxing ya Wanawake sijui kwanini hawakuleta Wanawake

Wetu...

Mzee mabondia wa kike. Hiyo television ungeibeba kichwani ukaivunjie mabwe pande???? Aibu tupu! tuombe uzima labda hiyo 2016 tutaweza
 
312914_4560360490843_301684079_n.jpg


london oyeeeeeeeeee

297674_4560341570370_1310644265_n.jpg


walijitenga? nasikia huyu dogo baba yake alihonga akapata nafasi ya kwenda kuchezea maji landani......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom