Picha: Baada ya Mnyika kukoswa na bomu mkutano unaendelea

Picha: Baada ya Mnyika kukoswa na bomu mkutano unaendelea

Tatizo la CCM na polisi yao wameshafika mahali hata mbinu za kutengeneza hujuma zimewaishia. Huku sasa ni kuumbuka tena!
 
aiseee.......nini hiki, lakn mbona picha haioneshi dalili ya kuoigwa kwa bomu?

Picha inayoonesha TOYOTA lililozungukwa na watu ndiko mahali ambako mkutano ungalifanyika mara ya kwanza!
Na kwa sababu tulihamia mahali pengine (UBUNGO), ndo hizo picha zenye watu walio wengi mkuu!
 
hayo mabomu ndio yanayowaongezea Chadema umaarufu, yaani CCM bana...kama kuongoza nchi kazi hata kampeni za kupata kula nazo mshindwe mwe! mimi mpaka sasa najiuliza Shonza na Mwampamba mliwapeleka Arusha kufanya nini??? mnawapeleka wasaliti kwenye kambi ya upinzani halafu mnategemea kushinda kweli kweli!!!! Sasa hivi mkitaka kuendelea mabomu na kina Shonza weka pembeni, rudieni ile list ya ahadi mlizotoa kwa wananchi mkianza na ile ya maisha bora kwa...halafu msilale mpaka mzifanyie kazi. Magamba choma moto sio mnavua gamba face mask na gamba kikofia huku gamba koti limekaa vyema mwilini tena limemechishwa na suruali na viatu, safisha uozo wote...hapo mtakonga nyoyo zetu.
 
Aliyekusabishia migao ni Nyerere na vibaraka wake aliowaachia nchi, Kikwete anabadili hilo na ushahidi mpaka mBarack Hussein Obama kautangaza, hujui hilo? kuna Mikataba ya kufua na kusambaa umeme zaidi ya aliyoifanya Kikwete toka nchi hii ipate Uhuru? Mikataba itayozalisha zaidi ya MW 3,000 imesha sainiwa na imeshaanza, uko wapi wewe?

Ku-SIGN na Kutekeleza ni mambo mawili MPISHANO!
Hasa katika nchi za mafisadi
 
Pole Kamanda Mnyika, na Mtanzania mwenzetu Thomas Jerome aliyeumizwa na bomu. Poleni sana.

Nadhani walitaka kufanya kama walivyofanya kwa Mwangosi. Mungu amewalindeni.

Viongozi wa CCM walitangaza kwamba CHADEMA mwisho wake mwaka huu wa 2013. Hatukuelewa itakuwaje mwisho wake. Ile video ya Mwigulu ikaonekana kama ndio ilikusudiwa kuleta mwisho wa CHADEMA lakini badala yake karibu ilete mwisho wa CCM.

Sasa nadhani wameamua kuua wananchi wafuasi wa CHADEMA kwa mabomu ya polisi ndiyo iwe namna yao ya kuufanya huu mwaka uwe mwisho wa CHADEMA. Kama polisi aliyesimamia jaribio la mauaji angefanikiwa, naye angepandishwa cheo kama Kamuhanda.

Tuwe macho sana, na lazima CHADEMA wajilinde wenyewe. Msipofanya hivyo atawalinda nani? Polisi? Mbona wana mkakati wa kuwaua?

Nduli Idi Amin alishangaza sana watu kwa tabia yake ya kuuwa wananchi. Naona NDULI CCM ana mpango wa kumpiku Amin.
 
Msiotaka ukweli mnaufaham tu na kuna siku mtaukubali tu hata kama hamtakiri midomoni mwenu.
 
Back
Top Bottom