chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,379
- 24,929
Watu 26 wamenusurika kifo 19 kati yao wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku saba kati yao wametibiwa na kuruhusiwa baada ya basi mali ya kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mindu nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Wakizungumza na ITV katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wanakopatiwa matibabu majeruhi wa ajali hiyo wameeleza ajali hiyo ilivyotokea huku wakieleza chanzo chake ni utelezi wa mvua zilizokuwa zinanyesha katika eneo hilo.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrichi Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva na kufuatia uzembe huo amemfutia leseni ya udereva huku akishikiliwa kwa mahojiano na baadaye atafikishwa mahakamani ili iwefundisho kwa madereva wengine.