..kwi kwi kwi...so mke na mumewe wanalogana!!
wee jamaa upo humu?!!
kama mnapendana(mnaaminiana) hamna tatizo lakini kama mnaishi kwa mtego ni sababu ya janga hiyo.....hebu vuta taswira mke anakuwa Ambassador, au waziri....au mkurugenzi mkuu kwenye shirika lenu...
Ni sifa kwako mume au ni majanga? mwekundu tafadhali bana, heheh
Roho hii ni mbaya mkuu kama ya kichawi tu...nipo mkuu Kivumah...habari ya siku
Low self esteem inajitokeza kwa mifumo tofauti tofauti. Ukiwa na mwenza wa aina hiyo, ni kumsaidia kujitambua thamani yake binafsi (bila mali, uzuri, wala sifa yeyote). Akishajua ana thamani basi hawezi ona shida mwenza ukimzidi kitu chochote.
Hii mpya kwangu.
Ila kama ipo,basi hao wanao fanya hivo nahisi ndo
wale utaskia kamuua mwenzi wake,.....ili arithi mali.
Ingawa sitaki kuamini kama kuna kitu kama hicho.
Mwisho wa ubaya ni aibu.
Wanaume wengi unakuta wanapata wasiwasi wenza wao wakifanulikiwa kwa kuogopa revenge. Wanasema pata hela mkeo akijue tabia yako. Unakuta wakati mwanaume ana hela masimango kwa mke na nduguze hayapungui. Sasa anajionea huyu mama akipata upenyo si atanilipishia? Kama hatishiki tena kodi ya nyumba si nae ataanza kunirudia usiku wa manane?
Sababu nyingine ni pale ambapo mapenzi yanaendeshwa kwa nguvu ya fedha. Kuna mwenza anamwaga hela tu na kusahau misingi ya uhusiano kama vile sex, emotional support na hata kujaliana na kuonueshana upendo. Sasa kama mwenza ilibidi atoe huduma hizo kwa sababu ya utegemezi, akifanikiwa si utamsikia bombani?
Mbu bana. . . kwani hujui ule msemo usemao 'maskini akipata ndio utajua tabia zake halisi' ?!Kuna watu makucha yao hung'arishwa kwa mafanikio.
Hali kama hiyo inapotokea kwa wanandoa (sio ndugu/rafiki) kunaweza kusababishwa na WIVU ila nadhani WOGA/WASIWASI na KUTOKUJIAMINI au hata kutokumwamini mwenzi ndio zaidi.
Kuna watu ambao wanaishi maisha waishiyo kwasababu tu mifuko haijatuna, kuna watu wametulia kwenye ndoa zao na pia watu wengine ni(au tuseme wana-act) humble kwasababu hiyo hiyo.
Kwahiyo inapotokea hali kama hiyo uwezekano ni kwamba mume/mke anaweza akawa anafurahia kabisa tena sana tu mafanikio ya mume/mke wake lakini mafikio hayo hayo yanamletea WOGA, WASIWASI na KUTOKUJIAMINI ndani ya ndoa yake.
Woga wa kunyanyapaliwa, woga wa kuanza kudharauliwa na kuonekana hufai tena (mwenzio amepanda daraja), woga wa yeye kuanza kufanya mambo ambayo hakuwa anaweza kuyafanya kutokana na kipato chake mf. kulewa, woga wa kutafutiwa 'replacement' inayoendana na mafanikio ya mwenzi n.k
Muhimu ni kumwaminisha mtu wa aina hiyo kwamba hutobadilishwa na mafanikio hayo bali maisha yenu pamoja ndio yatakayobadilika for the better. Mtoe woga na wasiwasi ajue kwamba yeye ndie wako wa moyoni no matter how succesful you get. Asipoonyesha kuchangamka na kufurahia pamoja na wewe baada ya hapo basi huyo hana jema. Chuki, wivu na gubu ndio zake.
- kimsaidia kujitambua-
Ohh yeah, so la mwanzo ni kujikubalisha mwenzio 'hajitambui' la pili kumkubalisha 'ajitambue' kwamba ana mapungufu....
A good starting point Kongosho
Unachoulizia wewe Mbu kwa mtizamo wangu jibu lake Ni Jealousy, ambayo ni the most dangerously feeling, Jealousy creates insecurity. Insecurity creates hatred, and hatred kills softly.......hahaha, truth hurts!
Enhee, ulitaka kusema nini vile
Maana "secrets" imo katikati ya mstari!
Mbu ni kweli, kwa mfano, kuna wanaume ambao hawataki kabisa mwanamke wake atongezwe na wanaume wengine.
Lakini ni kawaida kwa mwanamke kutongozwa awe ana mwanaume or not. In fact, ina-boost confidence ya mwanamke.
Baadhi ya wanaume are not used to this, wengine wana insecurity, wengine are just too possessive, wapo ambao wana psychological problems, being obsessive au ujinga tuu.
kuna wapenzi ambao wakipata mafanikio ndio jeuri dharau na kiburi kinazidi.... kama mwanaume unakuta harudi hata nyumbani.. amani inatoweka na hakuna upendo. unategemea mafanikio yake mwenza wake atayafurahia? nani atafurahi kuona mpenzi wake ana kazi nzuri analipwa vizuri lakini haioni hata sh kumi yake!!! sio tu roho mbaya... unaambiwa ukitaka kujua tabia ya mtu subiri apate pesa au cheo. lol