Philip Mpango: Hali ya Uchumi wa Taifa Mwaka 2019 na Tathimini wa Utekelezaji wa Bajeti kwa Nusu Mwaka wa Fedha 2019/20

Mbula!ndefu sana .
Ngoja nifute gari kwanza

CCM lazima waifanye ndefu ili tusisome yote. Nimetambua janja ya kina Polepole.

Ndiyo maana kila sehemu muhimu ya taarifa hii nimejaribu kuweka maandishi bold na rangi nyekundu kuwezesha usomaji wa kuruka ruka bila kukosa sehemu muhimu CCM hawataki tuzisome.
 
Mpango ni mtu wa hovyo anasema eti usfiri mgumu, sijui nini ....nchi ya viwandazi
 
Praise team
 
Mpango ni mtu wa hovyo anasema eti usfiri mgumu, sijui nini ....nchi ya viwandazi

Hapo anamaanisha Air Tanzania pia ni mzigo kwa serikali maana abiria wamepungua hawana uwezo wa kununua tickets pia hawasafiri tena nje ya maeneo yao hivyo wageni ktk mahoteli na guest house wamepotea kulinganisha na miaka ya nyuma awamu ya Jakaya Kikwete uchumi na biashara ulivyokuwa imara.
 
Mm sio praise team na wala sio mpinzani!! Ni mtu nayependa kujifunza!! Hayo ni maono yangu,ningependa kupata yakwako.. tunaelekezana na tutumie hoja ktika kufanya hìvo
He who remains neutral when there are oppressed and oppresors, he is an oppressor.
 
Ishara kamili kwa mtu aliyekwenda shule, na mtu anayejua anachokifanya.

Aya hii ina maana nzito, na bila shaka Waziri anatambua vizuri yote aliyotamka kwenye aya hii na kuyaamini kwa dhati ya moyo wake.
 
Very very fair observation.

Siku hizi hapa jamvini hatuna muda wa kuchambua kama ulivyofanya wewe, na hao wachache wanaopenda kufanya hivyo watauweka uchambuzi wao kisiasa, wakiegemea wanakosimamia katika siasa zao.

Hongera.
 
2019 wakulima wamekua discouraged kwa kiasi kikubwa kwahiyo wamelima kidogo ( ni chanzo kikubwa cha supply kuwa ndogo nchini)
Kama tungekuwa na takwimu za uhakika, hili unalosema hapa lingekuwa rahisi sana kulithibitisha.
Sasa sijui, kama kweli hata wizara husika wasiweze kujua jambo rahisi kama hili? Nawe hujasema ulipopata ushahidi wa jambo hili. Unazo takwimu zinazoonyesha wakulima kupunguza kilimo, au ni hisia zako tu ndizo zinazokutuma?

Je, hakuna sababu nyingine yoyote, kama utofauti wa hali ya hewa, n.k.?

Haya ni maoni tu, sio kwamba ninapinga ulichoandika hapo juu. Huenda hivyo ndivyo, lakini ushahidi bado haupo!
 
Ni kweli mkuu hayo ni maoni binafsi sina takwimu.

Ukisoma hiyo speech vizuri waziri amesema sababu ya ukuaji wa pato la Taifa kwa mwaka 2019 umechangiwa na baadhi ya mambo ntaandika machache.

1.uwekezezaji katika miundombinu( barabara , reli na airports)

2.kuimarika kwa huduma za usafirishaji

3.kuongezeka kwa shughuli za kilimo kuchangiwa na hali ya hewa nzuri.

.....
MFUMUKO WA BEI ZA VYAKULA
Waziri anasema sababu ni hizi

1. Changamoto za usafirishaji ( wakati mwanzon amesema hii sekta imemimarika na imechangia kukua kwa pato la Taifa)

2.changamoto ya miundombinu ya masoko

3. Uhaba wa chakula nchi jirani..( tuchukulie case ya mahindi ambapo price imepanda maradufu , na huku wakulima wamepigwa ban kuexport hili zao!!)

Sina Takwimu lakini hiyo ni simple relation ninayoweza nikaifanya wakulima wamekua discouraged kwa sababu ya hasara za mwaka 2018 na 17

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaheshimu sana michango kama hii ambayo ni dhahiri mchangiaji anao uelewa wa anachochangia. Tunaweza tukachambua haya uliyoweka hapa, kwa mfano hiyo namba tatu, na tusikubaliane moja kwa moja kwa kila kitu, lakini 'approach' uliyoichukua ni ya kuheshimiwa.

Ahsante mkuu, JF inaendelea kuvutia wengi wetu kwa michango kama huu wako.
 
January 7, 2020
Kisarawe, Pwani

Wakulima walia Ushuru lukuki zao la Korosho, wasema hii ni kuua zao hilo


Source: Azam TV
Huku zao la korosho likiuzwa Shs.800 kwa kilo lakini kuna ushuru wa aina nyingi mkulima anatakiwa kuulipa na hivyo kuwavunja moyo wakulima wa zao hili lililibatizwa 'Dhahabu' na serikali kutokana na kuwa zao namba moja linaloongoza kushangia akiba ya fedha za kigeni kwa nchi ya Tanzania.

Taarifa hii mbaya ni kinyume na ile ya Waziri wa Fedha Philip Mpango aliyoitoa siku chache zilizopitaya mbele ya waandishi wa habari ktk mkesha wa mwaka mpya 31/12/2919 kuwa serikali ina sera madhubuti iliyopunguza mzigo wa aina kibao za kodi kwa wananchi wanyonge.
 
7 Jan 2020
Tanga, Tanzania

Mafuriko yaleta changamoto treni za mizigo
Mbunge Adadi Rajab wa jimbo la Muheza kupitia CCM alifika kuona na kukagua uharibifu mkubwa uliotokana na mafuriko.

Naye meneja wa TRC alisema wanafanya juhudi kubwa kuwezesha Safari za treni ya mizigo kutoka Tanga na Mikoa ya Kaskazini zireje baada ya kusimama kwa siku kadhaa kutokana na reli kusombwa na maji eneo la Muheza kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha Mkoani humo.

Source: Azam TV
 
January 2, 2020

HALI YA USAFIRI WA BARABARA SEHEMU KOROFI KUSINI MWA TANZANIA

SELOUS EXPRESS Dar-Lindi-Songea Buti la Zungu Dar-Lindi-Mtwara Swahili express Dar-Lindi-Masasi

 
December 12, 2019

MKOA WA KIGOMA NDIO MKOA PEKEE AMBAO UMEBAKI BILA KUUNGANISHWA NA MIKOA MINGINE YA NCHI KWA BARABARA ZENYE KIWANG0 CHA LAMI,HALI HII IMEWAFANYA WANANCHI KUENDELEA KUTESEKA NA HALI HIYO HASA KATIKA KIPINDI CHA MASIKA KUTOKANA NA MAGARI KUKWAMA NA MENGINE KUPINDUKA KUTOKANA NA UBOVU WA BARABARA.

 
January 8, 2020

Bei za Nafaka, Mahindi , Mchele , Maharage zazidi kupanda maradufu - Walaji wasema

Bei ya Nafaka na Chakula zazidi kupaa. Azam TV wametembelea masoko maarufu ya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na hata Njombe ambapo ni mkoa unaotegemewa kuzalisha chakula kwa wingi kulisha sehemu zingine za Tanzania huko pia sokoni bei zimepanda sana.


Source: Azam TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…