Philip Mpango: Hali ya Uchumi wa Taifa Mwaka 2019 na Tathimini wa Utekelezaji wa Bajeti kwa Nusu Mwaka wa Fedha 2019/20

Mbula!ndefu sana .
Ngoja nifute gari kwanza

CCM lazima waifanye ndefu ili tusisome yote. Nimetambua janja ya kina Polepole.

Ndiyo maana kila sehemu muhimu ya taarifa hii nimejaribu kuweka maandishi bold na rangi nyekundu kuwezesha usomaji wa kuruka ruka bila kukosa sehemu muhimu CCM hawataki tuzisome.
 
Difference ya 2.0% -2018 had 6.7% 2019 kwa mazao ya chakula ni kubwa sana.

Reason anazozitoa waziri hazina uhalisia.

Kwanza anasema ni uhaba wa chakula kwa nchi jilani mean while wanatupiga ban wananchi kuuza chakula nje.

Pili,
Changamoto za usafirishaji ..wakati kwenye paragraph ya kwanza amesema kukua kwa uchumi wetu 2019 umechangiwa sana na ukuaji wa sekta ya usafirishaji( kwenye mfumuko wa bei anadai bei zimepanda sabab ya hizo changamoto)...

Wanaficha uhalisia ni wazi wakulima walikata tamaa kutokana na hasara waliokula kwa kupiga ban baadhi ya mazao kuuzwa nje , wakalazimika kuuza ndani kwa bei ya chini..

2019 wakulima wamekua discouraged kwa kiasi kikubwa kwahiyo wamelima kidogo ( ni chanzo kikubwa cha supply kuwa ndogo nchini)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpango ni mtu wa hovyo anasema eti usfiri mgumu, sijui nini ....nchi ya viwandazi
 
Japo kuna takwimu za kupika.. lakini kuna observation nimefanya!! Mosi, utitiri wa kodi ulikuepo hata kabla ya awamu hii ila kodi hizo hazikusimamiwa bali kulikuwa na loophole ya watu kukwepa kodi.Pili ni umadhubuti wa shilingi ya Tanzania katika awamu hii, kutoka mwaka 2010-2015 Shiliing ilishuka thamani kutoka sh 1500 per USD mpaka Tsh 2157 perUSD. Lakini toka 2015 mpaka leo Shilling imekuwa himilivu kwa kiasi kikubwa maana kwa sasa inabadilishwa kwa 2291per USD. Tatu mfumuko wa bei umekuwa maintained katika hali nzuri.. ni mwaka huu tu ambapo chakula kimepanda bei kwa kiasi kikubwa. Pesa hamna lakini watu wanakula na kweza kuishi.Nne bado tuna protectionism policy kubwa sana.Sheria zimebana sana hii inapelekea ugumu katika kuwekeza na kuendeleza biashara! FLEXIBILITY n muhimu sana katika kukuza uchumi na naamin hwatarudia makosa kama ya korosho na mazao ya chakula!! .. I stand to be lectured!!
Praise team
 
Mpango ni mtu wa hovyo anasema eti usfiri mgumu, sijui nini ....nchi ya viwandazi

Hapo anamaanisha Air Tanzania pia ni mzigo kwa serikali maana abiria wamepungua hawana uwezo wa kununua tickets pia hawasafiri tena nje ya maeneo yao hivyo wageni ktk mahoteli na guest house wamepotea kulinganisha na miaka ya nyuma awamu ya Jakaya Kikwete uchumi na biashara ulivyokuwa imara.
 
Mm sio praise team na wala sio mpinzani!! Ni mtu nayependa kujifunza!! Hayo ni maono yangu,ningependa kupata yakwako.. tunaelekezana na tutumie hoja ktika kufanya hìvo
He who remains neutral when there are oppressed and oppresors, he is an oppressor.
 
(4). Napenda kuwaahidi Watanzania kwamba, kwa msaada wa Mungu, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana na watumishi wenzangu katika Wizara na Serikali nzima, ili kutoa mchango mzuri katika kuijenga Tanzania mpya. Ndugu Waandishi wa Habari, Ninyi ndiyo kiungo kati ya Serikali na wananchi katika kuwafikishia sera, mipango, mikakati na taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio ya Serikali katika kuwapelekea maendeleo na juu ya fursa zilizopo katika sekta binafsi. Ninyi pia ndio mnaoleta mrejesho Serikalini kuhusu maoni, ushauri na dukuduku za wananchi. Vilevile, ninyi mnawakilisha sekta ambayo ni miongoni mwa sekta tano zinazokua kwa viwango vikubwa. Katika mwaka 2018 sekta ya habari na mawasiliano ilikua kwa kiwango cha 9.1% na 10.7% kwa kipindi cha Januari-Juni 2019.
Ishara kamili kwa mtu aliyekwenda shule, na mtu anayejua anachokifanya.

Aya hii ina maana nzito, na bila shaka Waziri anatambua vizuri yote aliyotamka kwenye aya hii na kuyaamini kwa dhati ya moyo wake.
 
Japo kuna takwimu za kupika.. lakini kuna observation nimefanya!! Mosi, utitiri wa kodi ulikuepo hata kabla ya awamu hii ila kodi hizo hazikusimamiwa bali kulikuwa na loophole ya watu kukwepa kodi.Pili ni umadhubuti wa shilingi ya Tanzania katika awamu hii, kutoka mwaka 2010-2015 Shiliing ilishuka thamani kutoka sh 1500 per USD mpaka Tsh 2157 perUSD. Lakini toka 2015 mpaka leo Shilling imekuwa himilivu kwa kiasi kikubwa maana kwa sasa inabadilishwa kwa 2291per USD. Tatu mfumuko wa bei umekuwa maintained katika hali nzuri.. ni mwaka huu tu ambapo chakula kimepanda bei kwa kiasi kikubwa. Pesa hamna lakini watu wanakula na kweza kuishi.Nne bado tuna protectionism policy kubwa sana.Sheria zimebana sana hii inapelekea ugumu katika kuwekeza na kuendeleza biashara! FLEXIBILITY n muhimu sana katika kukuza uchumi na naamin hwatarudia makosa kama ya korosho na mazao ya chakula!! .. I stand to be lectured!!
Very very fair observation.

Siku hizi hapa jamvini hatuna muda wa kuchambua kama ulivyofanya wewe, na hao wachache wanaopenda kufanya hivyo watauweka uchambuzi wao kisiasa, wakiegemea wanakosimamia katika siasa zao.

Hongera.
 
2019 wakulima wamekua discouraged kwa kiasi kikubwa kwahiyo wamelima kidogo ( ni chanzo kikubwa cha supply kuwa ndogo nchini)
Kama tungekuwa na takwimu za uhakika, hili unalosema hapa lingekuwa rahisi sana kulithibitisha.
Sasa sijui, kama kweli hata wizara husika wasiweze kujua jambo rahisi kama hili? Nawe hujasema ulipopata ushahidi wa jambo hili. Unazo takwimu zinazoonyesha wakulima kupunguza kilimo, au ni hisia zako tu ndizo zinazokutuma?

Je, hakuna sababu nyingine yoyote, kama utofauti wa hali ya hewa, n.k.?

Haya ni maoni tu, sio kwamba ninapinga ulichoandika hapo juu. Huenda hivyo ndivyo, lakini ushahidi bado haupo!
 
Ni kweli mkuu hayo ni maoni binafsi sina takwimu.

Ukisoma hiyo speech vizuri waziri amesema sababu ya ukuaji wa pato la Taifa kwa mwaka 2019 umechangiwa na baadhi ya mambo ntaandika machache.

1.uwekezezaji katika miundombinu( barabara , reli na airports)

2.kuimarika kwa huduma za usafirishaji

3.kuongezeka kwa shughuli za kilimo kuchangiwa na hali ya hewa nzuri.

.....
MFUMUKO WA BEI ZA VYAKULA
Waziri anasema sababu ni hizi

1. Changamoto za usafirishaji ( wakati mwanzon amesema hii sekta imemimarika na imechangia kukua kwa pato la Taifa)

2.changamoto ya miundombinu ya masoko

3. Uhaba wa chakula nchi jirani..( tuchukulie case ya mahindi ambapo price imepanda maradufu , na huku wakulima wamepigwa ban kuexport hili zao!!)

Sina Takwimu lakini hiyo ni simple relation ninayoweza nikaifanya wakulima wamekua discouraged kwa sababu ya hasara za mwaka 2018 na 17

Ninaheshimu sana michango kama hii ambayo ni dhahiri mchangiaji anao uelewa wa anachochangia. Tunaweza tukachambua haya uliyoweka hapa, kwa mfano hiyo namba tatu, na tusikubaliane moja kwa moja kwa kila kitu, lakini 'approach' uliyoichukua ni ya kuheshimiwa.

Ahsante mkuu, JF inaendelea kuvutia wengi wetu kwa michango kama huu wako.
 
January 7, 2020
Kisarawe, Pwani

Wakulima walia Ushuru lukuki zao la Korosho, wasema hii ni kuua zao hilo

Source: Azam TV
Huku zao la korosho likiuzwa Shs.800 kwa kilo lakini kuna ushuru wa aina nyingi mkulima anatakiwa kuulipa na hivyo kuwavunja moyo wakulima wa zao hili lililibatizwa 'Dhahabu' na serikali kutokana na kuwa zao namba moja linaloongoza kushangia akiba ya fedha za kigeni kwa nchi ya Tanzania.

Taarifa hii mbaya ni kinyume na ile ya Waziri wa Fedha Philip Mpango aliyoitoa siku chache zilizopitaya mbele ya waandishi wa habari ktk mkesha wa mwaka mpya 31/12/2919 kuwa serikali ina sera madhubuti iliyopunguza mzigo wa aina kibao za kodi kwa wananchi wanyonge.
 
7 Jan 2020
Tanga, Tanzania

Mafuriko yaleta changamoto treni za mizigo
Mbunge Adadi Rajab wa jimbo la Muheza kupitia CCM alifika kuona na kukagua uharibifu mkubwa uliotokana na mafuriko.

Naye meneja wa TRC alisema wanafanya juhudi kubwa kuwezesha Safari za treni ya mizigo kutoka Tanga na Mikoa ya Kaskazini zireje baada ya kusimama kwa siku kadhaa kutokana na reli kusombwa na maji eneo la Muheza kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha Mkoani humo.

Source: Azam TV
 
January 2, 2020

HALI YA USAFIRI WA BARABARA SEHEMU KOROFI KUSINI MWA TANZANIA

SELOUS EXPRESS Dar-Lindi-Songea Buti la Zungu Dar-Lindi-Mtwara Swahili express Dar-Lindi-Masasi

December 12, 2019

MKOA WA KIGOMA NDIO MKOA PEKEE AMBAO UMEBAKI BILA KUUNGANISHWA NA MIKOA MINGINE YA NCHI KWA BARABARA ZENYE KIWANG0 CHA LAMI,HALI HII IMEWAFANYA WANANCHI KUENDELEA KUTESEKA NA HALI HIYO HASA KATIKA KIPINDI CHA MASIKA KUTOKANA NA MAGARI KUKWAMA NA MENGINE KUPINDUKA KUTOKANA NA UBOVU WA BARABARA.

January 8, 2020

Bei za Nafaka, Mahindi , Mchele , Maharage zazidi kupanda maradufu - Walaji wasema

Bei ya Nafaka na Chakula zazidi kupaa. Azam TV wametembelea masoko maarufu ya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na hata Njombe ambapo ni mkoa unaotegemewa kuzalisha chakula kwa wingi kulisha sehemu zingine za Tanzania huko pia sokoni bei zimepanda sana.

Source: Azam TV
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom