deogan
JF-Expert Member
- Sep 7, 2011
- 399
- 46
Hapo kipindi cha nyuma simu zenye maumbo makubwa hazikuwa zinapendwa na watu wengi, zilikua zikichukuliwa kama kero hasa sababu kubwa nyingi kuwa ni vimeo za kichina.
Ila kwa sasa makampuni ya simu yamekuwa yakitoa simu zenye maumbo makubwa na siku zinavyoenda zinazidi kuwa na maumbo makubwa.
Zaidi, tablet nazo zimekuwa zikitumika kama simu hasa zile zinazoingia line.
Kama inavyojulikana kiwango cha chini cha tablet ni ile yenye kioo cha inchi 7, kutokana na hilo simu zenye kioo kinachokaribia usawa huo zimekuwa zikiitwa phablet, kipimo kinachotumika sanasana ni simu ya Samsung galaxy Note II yenye kioo cha inchi 5.5 ambayo ilitanguliwa na Note I yenye kioo cha inchi 5.3 japo haiongelei sana kama phablet.
Kutokana na hayo kiwango cha display ya inchi 5 kimekuwa kawaida kwenye zimu baada ya kutoka HTC butterfly na nyinginezo ikiwemo Samsung galaxy s4 ambayo sasa inaonekana ni kawaida.
Zaidi, sasa kuna simu (phablet) zenye kioo zaidi ya inchi 5.5 hivyo kupunguza zaidi tofauti iliyopo kati ya simu na tablet ikiwemo Samsung Galaxy Mega 6.3 yenye kioo cha incho 6.3 hivyo kuifanya iwe na tofauti ya inchi 0.7 kufikia kiwango cha chini cha kioo cha tablet (inchi 7).
Wewe unaona imekaaje kuwa na phablet?
Kiwango chako cha ukubwa wa simu ni kipi?