Petition: Tumshtaki Pinda

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,511
11,271
Wakuu,

Katika pita pita yangu hapa JF leo nimekutana na hii taarifa kuhusu Pinda akiwa anahutubia huko Kagera. Kwa mujibu wa maelezo yake (kulingana na habari) inajidhihirisha wazi kuwa anajaribu kuwa-intimidate watu ili waiache haki yao ya kikatiba ya kuandamana. Kutokana na ukweli kwamba haya maandamano yalipata kibali na Baraka zote kutoka Polisi (chombo cha dola) basi Pinda hakutakiwa kutoa maneno ya vitisho kiasi hicho. Pia kutokana na vitisho hivi, ni dhahiri kuwa itafika kipindi Polisi (kwa kufuata amri kutoka Juu) itasitisha kuendelea kutoa vibali na kwa mantiki hiyo kusababisha uvunjifu wa amani iwapo raia watakaidi. Hii ni kauli inayodhihirisha wazi tabia ya viongozi wetu kupenda kuburuza raia wao kwa kutumia vyombo vya Dola.

Kwa mantiki hiyo basi, nimepata wazo kwamba inawezekana kabisa kuanzisha utaratibu wa kumshtaki huyu mtu kwenye Mahakama za kimataifa kwa ku-violate haki za Binadamu kulingana na Universal Declaration of Human Rights (1948).

Wataalamu wa sheria hapa JF mnaombwa kutoa mwongozo juu ya hili.

Wakuu wangu, naomba kuwasilisha hoja.
 
Well, unaona hata barua wanazoandika akina Tendwa kwa Chadema. Haziko specific hivyo CCM imeamua kwa dhati kutumia dola kudhibiti matakwa ya wananchi na taratibu Kikwete na Serikali yake yanaanza kuonesha dalili mbaya za udikteta. Wanajisogeza karibu sana na The Hegue.

Ngoja tusubiri michango ya wanasheria ili nasi tuchangie sahihi zetu.
 
Naunga mkono hoja mkuu. Watatue matatizo yetu watanzania siyo kututishia nyau kudai haki zetu! Uongozi waliutaka wenyewe!
 
YOUR RIGHT.Mr Hocambo katega sikio Tanzania

Mkuu tusisubiri mpaka Ocampo atuhurumie, tuanze wenyewe.

Well, unaona hata barua wanazoandika akina Tendwa kwa Chadema. Haziko specific hivyo CCM imeamua kwa dhati kutumia dola kudhibiti matakwa ya wananchi na taratibu Kikwete na Serikali yake yanaanza kuonesha dalili mbaya za udikteta. Wanajisogeza karibu sana na The Hegue.

Ngoja tusubiri michango ya wanasheria ili nasi tuchangie sahihi zetu.

Mkuu nadhani hata wanasheria wa CHADEMA wanaweza kutumia hizo barua kama ushaidi na kulipeleka mbele zaidi hili suala.. Haki za watu zinabakwa hapa.
 
Unataka kumshtaki kisiasa au kisheria? Kama ni ni kisiasa then, umeiweka sredi panapotakiwa.
 
Wanachemsha sana ,tena isisubiriwe vielelezo vya mipango yao na maneno yao vipelekwe mapema .....
 
Hili ni wazo jema. Ni Tanzania pekee ambalo ni Taifa la viongozi wanaodharau wananchi wake. Hii ni kwa sababu kila wakionesha dharau zao kwa wananchi tunakaa kimya. Ni lazima ifeke mahali viongozi wajiulize ni nini kitatokea ikiwa watasema au kufanya kwa nanna fulani.Chukulia maneno ya Polisi wapige tu wananchi ingetoleaw na mtu wa rank ya waziri mkuu Kenya, Uingereza, Marekani, Japan hakika kesho yake kibarua hakuna. Wananchi wangeandamana mpaka atoke. Tanzania sijui kuna shida gani?
 
Unataka kumshtaki kisiasa au kisheria? Kama ni ni kisiasa then, umeiweka sredi panapotakiwa.

Pinda ni Mwanasheria au Mwanasiasa...?????
Je Pinda alipoapa kuifuata katiba ya Tanzania....aliapa kama mwanasheria au mwanasiasa...!
Any answer litasaidia thred hii ikae jukwaa lipi.
 
Ile kesi iliyofunguliwa ya akina BI KIJO BISIMBA MBONA HAIANZI KUNGURUMA TUMUONE AKIMWAGA CHOZI MAHAKAMANI??
 
amri ya pinda imemgusa shekh ponda na waislam wote nchini. tutajibu mapigo, kuanzia dua na mengineyo
 
Pinda ni Mwanasheria au Mwanasiasa...?????
Je Pinda alipoapa kuifuata katiba ya Tanzania....aliapa kama mwanasheria au mwanasiasa...!
Any answer litasaidia thred hii ikae jukwaa lipi.

Poa basi utapata ushauri wa kisiasa hapa jinsi ya kumshitaki Pinda.
 
Hivi haki ya kuandamana ndiyo haki kuu hapa Tanzania? Hakuna haki nyingine maana sasa naona harakati zetu zimekuwa ni kulaumu polisi kuzuia maandamano kila lkukicha, wanaoathirika na maandamano hawana haki? wanaoathirika na chuki zinazoenezwa na viongozi wa dini hawana haki/wanasiasa hawana haki? Haki ni lazima itendwe na serikali tu? haki yangu ya kuishi bila kuathiriwa na uchafuzi wa hali ya usalama inalindwaje? Nimlalamikie nani? nikiilalamikia serikali ikachukua hatua inalaumiwa na kushambuliwa!! niende wapi?

Ni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom