Ni neema na baraka za Mungu Tanzania imebarikiwa kua na kiongozi mbeba maono ya waTanzania wo ambae mstahimilivu na mwenye subra kama Dr.Samia Suluhu Hassn, licha ya chuki na upotoshaji unaoelekezwa dhidi yake na wanasiasa waliopoteza uelekeo wakiungana na viongozi wa dini kwasababu Dr.Samia Suluhu Hassani sio wa dini yao na pengine kwasababu ni kiongozi shupavu mwananmke.
Dhamira na nia njema ya mbeba maono huyu wa waTanzania, ndio haswa chimbuko la uongozi wake madhubuti wa kisayansi dhidi ya wahubiri chuki na wachochea uhasama dhidi ya serikali yake sikivu ya CCM anayoiongoza.
Dr.Samia Suluhu Hassan ni mnyenyekevu na msikivu wa kiwango cha juu mno katika historia ya nchi yetu, hasa anapotekeleza majukumu yake muhimu sana ya kuwatumikia wananchi na waTanzania wote kwa ujumla. Hapajawahi kutokea kiongozi mstahimilivu mwenye subra, hekima na busara kama huyu wa Tanzania kwa sasa.
Kama taifa yafaa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya huyu mama Dr.Samia, na kuzidi kumuombea kwa Mungu aendelee kumjalia afya njema na maono zaidi katika kuwatumikia na kuwaletea waTanzania maendeleo.
Msingi wa uongozi wake imara na usio tetereka, umejengwa katika falsafa yake mwenyewe ya maridhiano, mageuzi, ukarabati na ustahimilivu. Msingi wa falsafa hii ndiyo imeiliunganisha Taifa letu kutoka kwenye migawanyiko na hatimae kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwengu kutoka kujitenga.
Na matokeo yake uchumi wetu unaimarika, huduma za kijamii ni za uhakika zaidi na hali ya kisiasa ikizidi kuboreshwa siku hadi siku kuelekea uchaguzi mkuu wa october2025.
Hekima na Busara za Rais Dr.Samia Suluhu Hassan, daima zimekua tiba na dawa ya mikwamo na changamoto ndogo ndogo za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa nchi yetu, licha ya hujuma, kelele za chuki za kidini, msukumo wa mataifa ya nje kwa kutumia vibaraka wao ndani ya vyama vya siasa na madhehebu ya kidini, kujaribu kuhujumu na kuvuruga jitihada za mtukufu Rais za kuimarisha umoja na amani ya waTanzania. Ni fahari kwa kila mTanzania mzalendo kujivunia umahiri wa Dr.Samia Suluhu Hassan katika kusimama imara katika nafasi yake ya urais, huku akiwatumikia waTanzania kwa weledi wa kiwango cha juu sana na serikali yake sikivu ya ccm.🐒
Well done Dr.Samia Suluhu Hassan
God Bless You Mama. By chawa mwandamizi...