Pete za Ndoa

kwa yoyote alieoa na kuolewa na avae icho kitambulisho alichokikubali mwenyewe cku anajiingiza kwenye cub ya ndoa bila kulazimishwa na yoyote, lakini ndio hivyo tena kia mtu anazichukulia ki vyake, kwangu mie cjawahi kuivaa mwaka wa 6 sasa.

zinatushushia heshima kivipi?..mie cjawahi kuivua yangu aisee..

Kha!! hapa luv kweli umeingia choo cha kiume.
 
Hahahaha mpwa kumbe ndo maana unavaa mikono yote pete in case of any suspicious!

Mpwa imenitokea mara kadhaa warembo wananitosa kumbe sina pete..
Jamaa angu mmoja akanipa maufundi hayo kuwa ukiwa na pete ya ndoa ni dili kwa warembo maana anajua unapita tu kwa kudumisha mila
 
kwa yoyote alieoa na kuolewa na avae icho kitambulisho alichokikubali mwenyewe cku anajiingiza kwenye cub ya ndoa bila kulazimishwa na yoyote, lakini ndio hivyo tena kia mtu anazichukulia ki vyake, kwangu mie cjawahi kuivua mwaka wa 6 sasa.
....
 
Kuna shemeji yangu ni fundi umeme yeye amemwambia dada yangu hataki kuvaa pete kwa sababu ya nature ya kazi yake kwamba akivaa pete anaongeza hatari ya kupigwa na shoti ya umeme.
 
Nimeshuhudia mara kadhaa mabinti wakisema buzi lililo oa ndo lenyewe linachunika sasa hapo alama pekee ni pete.
Sisi ving'ang'anizi alafu uso wa mbuzi tukiangaliwa kwenye vidole patupu mrembo anaishia kusema wewe si wa type yangu.

Kuna wale wachununaji waliokubuhu hapa mjini, ole wako uwe umeoa halafu ajue una pesa. Lazima akufuate ofisini kuja kukuomba dau kubwa ili asimwambie mkeo.

Mzee mmoja tajiri na maarufu hapa mjini amewahi kutozwa Shs. 3m na demu, eti kisa hawakutumuia kinga na demu anasema amesikia huyo mzee ni mgonjwa. Na akamwambia kama unabisha nakwenda kumwambia mkeo na Shingongo na magazeti yake lazima wakurushe. Mzee akatoa hiyo pesa ili yaishe!
 
Kuna shemeji yangu ni fundi umeme yeye amemwambia dada yangu hataki kuvaa pete kwa sababu ya nature ya kazi yake kwamba akivaa pete anaongeza hatari ya kupigwa na shoti ya umeme.


Mwazani mangalie sna huyo shemeji yenu! Kama anampenda mkewe angeivaa na kuiua wakatu wa kazi anyway mie hata shingoni ningeitundika; ile kuwa nayo jirani ni raha!
 
umevua pete ye2?...nipo laaziz majukumu tu,haibiwi mtu hapa yaani jiamini 101% laaziz.

Siwezi kuvua pete yetu laazizi! Hata kama ningekuwa fundi wa kuchomelea vyuma, ningeivaa tu, bora nipigwe na shoti kuliko kuivua.
 
kutovaa pete kuna sababu nyingi
1. inakubana (baada ya kuoa/kuolewa umenenepa)
2. Imepotea hujapata hela ya kununua nyingine
3. Uamuzi tu wa mtu

mimi i dont care kuvaa kutovaa naona sawa tu ndoa iko moyoni sio kwenye pete, wangapi wanatoka nje na mapete mkononi, hivyo vitu ni tamaduni tu za nje tumeiga ndoa ni kichwa chako kinachukuliaje mie wife alipoteza yake, tukanunua nyingine nayo ikapotea na akakaa kama mwaka hivi sasa hivi amenunua nyingine ila mie wala sijali kuvaa au kutovaa ingawa mimi uwa navaa ingawa nikilala au kwenda kuoga naivua na siku nyingine uwa nasahau kuivaa
 
Pia niliwahi kusikia kuwa hizi nazo zinazovaliwa kama fashion zina maana yake kulingana na kidole pete ilipovaliwa lkn msimulizi pia alikosa maana. Lakini pia mbona nyingine zavaliwa miguuni jamani?
 
kuna wengine hawavai pete kwa sababu za fashion zaidi.

kuvaa pete ni passion kwao na wanapenda kupangilia pete na jewelery nyengine according to mavazi.

sasa leo una match black and silver .....ungependa kuvaa white gold accessories , unakuta unashindwa kisa pete ya ndoa ya yellow au pink gold!
 
Mimi mke wangu avae asivae hainisumbui provided she loves me. Mtu anaweza kuvaa hata ya thamani kama ile ya aliyovishwa Happiness Magesse-USD 70,000 na bado akawa kiwembe bin Kicheche. Pete ni kama mabati tu mimi naamini zaidi kwenye upendo wa dhati na sio lazima uwe demonstrated na pete kwenye vidole vyote 10.

Mpwa umeombwa na jopo uwe unavaa pete yako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom