Pete ya ndoa ina nafasi gani kwenye ndoa?

Pete ya ndoa ina nafasi gani kwenye ndoa?

Kennedy

Platinum Member
Joined
Dec 28, 2011
Posts
61,627
Reaction score
74,474
Salam Wana MMU.

Baadhi ya wanandoa baada ya kufunga ndoa na kukaa miaka kadhaa na wengine hata bila kukaa sana kuna hii shida huwa inajitokeza:-

Baadhi wamekuwa wakipoteza Pete zao za ndoa kwa namna mbalimbali,ambazo kila mmoja anajua mwenyewe .

Baada ya kupoteza Pete ndoa huwa haivunjiki isipokuwa kuna baadhi ya wanandoa huamua kuvaa pete yoyote kidoleni kukamilisha zoezi la ishara kuwa ameowa/kuolewa !

Je? Mtu asipovaa hiyo pete ya ndoa huwa wanahisi nini? Ni kama ndoa haipo ama vp?

Karibuni kwa michango na hisia zenu kwania njema tu ya kuelimishana.
 
wazazi wangu wako pamoja mpaka leo hii na bado wanaishi kwa furaha na wala hawana pete za ndoa vidoleni mwao, so nafikiri suala la kuvaa pete ya ndoa kwa muda mrefu au mfupi hutegemea na mvaaji na mapendezi yake juu ya pete, wengine kukaa na pete kidoleni kunawadisract na hivyo kupoteza au kuivua muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi Zima la ndoa na wengine asili yao tu hupenda kuvaa pete vidoleni mwao na hivyo kujikuta wakidumu na pete zao kwa muda mrefu, kwa maoni yangu.
 
Ndoa ni ndo tu, pete ni ishara ya upendo na uamnifu. Hii kitu historia yake ipo hadi kwenye biblia sikumbuki ni kitabu gani. Kwa sababu moyo upo kushoto na pete huvaliwa upande huohuo kuonesha upendo toka moyoni.
 
Pete inaondoa usumbufu mkubwa sana mtu anaoweza kuupata kwa wanaume au wanawake malaya wanaoheshimu ndoa za watu kwasababu wanapoona umevaa pete wanaogopa kujaribu kukutongoza.

Mimi pia nakumbuka wakati natafuta mchumba nilikuwa nikikutana na msichana kama ana pete nilikuwa sijaribu kumtongoza kabisa, ila kama hana pete na amenivutia nitatafuta njia yoyote nijaribu kutupa ndoano yangu.

Pete ni ishara tu yakuonyesha kwamba uko ndani ya ndoa, unapoivua inakuwa vigumu mtu kujua kwa haraka kama umeoa au umeolewa.
 
Sipendi kuvaa pete ya aina yoyote sasa sijui hiyo ya ndoa itakuaje nahisi nitaivaa siku ya harusi tu
 
kama asili yake pete ina maana sana katika ndoa.

Ni ishara ya commitment kwa mume au mke wako na heshima kwa ndoa yenu. Unfortunately siku hizi wanandoa walio wengi hawazithamini inavyotakiwa ndo maana haya yanatokea.

Wengne wanachepuka anavua anaweka pemben anagegedwa na mchepuko akimaliza anavaa tena au wengne anagegedwa nayo kidoleni!
 
ndoa sio pete bali ni moyo wako mmkuu na matendo yale kuishi kama wanandoa.

pete ni ishara tu kuwa umeoa ila wapo wanaochepuka nazo hta guest house

maana halisi ya pete kwangu siijui

Uvaaji pete tumerithishwa utamaduni wa kizungu uliokuja sambamba na kuenea kwa dini, lakini historia inatuambia waafrika hatukua na utaratibu huo lakini ndoa zilifungwa na kuheshimiwa.

Binafsi ninachojua ndoa ni moyo unaofungamana kwa wawili walioamua kuwa mume na mke. Hizi ishara za nje pengine hudanganya na hadaa tu maana michepuko mingi utaona wanazo hizo pete na bila haya huku wakijuana kila mmoja ana wake lakini wanaendesha mazoezi ya michepuko.

Mimeshuhudia kuna wale ambao hawana mazoea ya kuvaa hizi tpete lakini wako ngangali kwenye kuheshimu ndoa zao kwa vile kuheshimu ndoa ni moyo wa mtu wala si pete.
 
Soma kitabu cha Mwanzo 24 kuna stori nzuri sana apo utapata kitu kuhusu Pete na Ndoa.
ndoa sio pete bali ni moyo wako mmkuu na matendo yale kuishi kama wanandoa.

pete ni ishara tu kuwa umeoa ila wapo wanaochepuka nazo hta guest house

maana halisi ya pete kwangu siijui
 
Pete inaondoa usumbufu mkubwa sana mtu anaoweza kuupata kwa wanaume au wanawake malaya wanaoheshimu ndoa za watu kwasababu wanapoona umevaa pete wanaogopa kujaribu kukutongoza.

Mimi pia nakumbuka wakati natafuta mchumba nilikuwa nikikutana na msichana kama ana pete nilikuwa sijaribu kumtongoza kabisa, ila kama hana pete na amenivutia nitatafuta njia yoyote nijaribu kutupa ndoano yangu.

Pete ni ishara tu yakuonyesha kwamba uko ndani ya ndoa, unapoivua inakuwa vigumu mtu kujua kwa haraka kama umeoa au umeolewa.

Nisingefikiria kwamba pete ni kinga ya usalama wa ndoa. Hata asiye mwanandoa ambaye ni single mwenendo mwema ni ishara ya tabia na ustahimilivu katika maisha yake kwa pamoja humjengea heshima kwa jamii.

Kutongozwa au kutongoza kunategemea mazingira ya mtongozwa au mtongozaji anavyaojiweka. Tumeshuhudia hapa watu wanaleta mada kwamba anashindwa kutongoza na kuomba ushauri namna gani afanye, maana yake mtu anayetongoza ni hulka hata awe na mke au mpenzi ataendelea na mazoea ya kujaribia kila anayemvutia machoni kumtongoza, hiyo ni sawa na mvuta sigara hujaribia kila aina ya sigara aone zinavayotofautiana.

Huko makazini wamejaa wenye pete na ndiko michuepuko imeshamiri, kama pete ni kinga hayo yanatokeaje? Kuna walio very smart and attractive katu hawatongozi au kutongozwa sababu behavior you inawafanya watongozaji kupata kigugumizi na kusitisha makusudia hayo kwa vile mwenye kutongozwa hajaweka mazingira ya kuingilika kirahisi, wanabaki kusindikizwa kwa macho tu kwa tamanio la moyoni.

Niliandika hapa JF kwenye mada fulani kuwa niliwahi kufuatwa na mke wa mtu akiwa na malengo ya kuchepukia kwangu, lakini alipofika nyumbani kwangu na kuona sina nafasi inayomfanya afanye mchepuko na maongezi kuwa ya kawaida wala kutoonyesha dalili ya kumjengea mazingira au mwanya wa kunitamkia nisiyopenda alipata kigugumizi na kuishia kutuliza mzuka aliokuwa nao na wala hakuthubutu kunitamkia cho chote ingawa alisomeka hivyo alipoingia nyumbani kwangu kunitembela.

Ukweli mazingira ya michepuko tunayaandaa wenyewe tusisingizie pete ndio kinga.
 
hata zile za uchumba zimeisha thaman siku hzi. Unaweza mvalisha mtu hata ya tanzanite gram10 lakin haithamin, anaenda kwa mchepuko wake anapgwa tu
 
Usijali hata mimi ni hatari kwa namna nilivyokumis

Mambo mengine ni poa

Umepungua wewe tu hapa!

nilikumiss sana ....nafurahi kusikia kwako....

majukumu yaliibana nikafkiri ntakuona kanisani ila ikashindikana..
napambana na maisha paroko
 
Soma kitabu cha Mwanzo 24 kuna stori nzuri sana apo utapata kitu kuhusu Pete na Ndoa.

Kumbuka Biblia imejengeka katika utamaduni wa kiyahudi na kurahi utamaduni wa kiarabu huku asili zao zikiwa zinazoshabihiana. Tungeangalia utamaduni wa kiafrika na je kutovaa pete kunaathiri ndoa? Kwa nini wazee wetu na mababu zetu hawakuvaa pete na ndoa zao zilidumu zaidi kuliko sisi tunaovaa pete lakini ndoa zipozipo tu na takalaka ni kama mtindo wa maisha?
 
Back
Top Bottom