Pesa za EPA, na leo ni pesa za RADA kurejeshwa nchini

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Nimejiuliza mengi kuhusiana na hizo fedha zinazorejeshwa serikalini bila kupata jibu la matumizi yake. Je hizi fedha zinatumika kwa shughuli gani au kwa manufaa ya nani? Isije ikawa zinaingia mifukoni mwa wachache wajanja. Kama ndio hivyo sioni haja ya kuzirudisha nchini. Naomba mwenye kujua matumizi ya fedha hizo anijuze.

Ushauri wangu ni kuwa ili kuondoa dukuduku, fedha hizi zingeweza kutumika kujenga kipande cha kilomita kadhaa za barabara ili iwe ni kumbukumbu, hata mtu akiuliza jinsi fedha hizo zilivyotumika inakuwa rahisi kujibu. Mimi binafsi nina hamu ya kujua matumizi ya fedha hizo.

Mkereketwa wa kujua ukweli.
 
Nimesikia hii asubuhi taarifa ya habari kuwa zitatumika kununulia vitabu shule za msingi .ila babo wanajamii wanataraji kuona mabadiliko kwenye shule husika na ingekuwa vizuri kukawa na muda maalum ujulikane linapokuja suala la utekelezaji urasimu tunajua upo ila kwa swali hili ,tungependa urasimu upunguzwe kidogo .pia tunapongeza juhudi zilizofanywa na vitengo vya nje kurejesha kiasi hicho kingepotea hivi hivi
 
unawezakuta tayari zishafika arumeru kwani huko hela zima mwagwa kama mvua.magamba ni noma.hazitokidhi matakwa kama ilivyotarajiwa lazima zengwe litokee,nisuala la kusubiri na kuona alakini hakuna kitu hapo.
 
Back
Top Bottom