Pesa za COVID-19 na ulafi wa Kiafrika

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,082
10,742
Mataifa ya Ulaya na Magharibi kwa ujumla hawataziachia nchi walizowahi kuzitawala na wana vyambo vingi vya kuendelea kuwanasa. Kila janga linalotokea hutoa fedha nyingi kujaribu kuonesha kuguswa na huruma zao.

Kwa hili huwa wanawanasa marais wa kiafrika kwa urahisi kabisa. Na jambo la kushangaza ni jinsi nchi hizo za wakoloni pamoja na kutokuwa na rasilimali nyingi lakini daima hawakaukiwi na mabilioni ya fehda kwa ajili ya ufadhili kwenye nchi za Kiafrika.

Mfano kwenye hili janga la Corona marais wa kiafrika wamedhihirisha kuwa si watu wa maana wa kuongoza watu wao.Wapo ambao wamehiari kuua uchumi wao kwa kuwazuia wananchi kufanya kazi ilimradi tu watangaze ongezeko la wanaokufa au kuumbukizwa na corona na wao wapokee misaada inayoitwa ya kupambana na corona.

Baada ya hapo hizo pesa kwa uroho hugawana wao kwa wao na wala haziendi kule zilikokusudiwa. Wakoloni nao wakishajua hivyo huendelea kuzidharau na kuzidhoofisha hizo nchi kwa kuziwekea vikwazo zaidi.
 
Japo umeandika haraka haraka sana ila nimevumulia kusoma, sasa koo limenikauka acha ninywe maji kidogo.

Tanzania tumepewa bilioni 70 na bila aibu tumepokea, kwa corona ipi!!
 
Tanzania tumepewa bilioni 70 na bila aibu tumepokea, kwa corona ipi!
Kama tulivyoonesha dunia kwamba hatuna corona na hata mikutano ya kampeni inajaa na hatusikia watu kuanguka kwa corona labda kwa joto kali, sasa ni kipi kilichoshindikana kusema hizo pesa hatuzitaki ziende labda Kenya ambako bado tatizo liko.
 
Hapa afrika hela zipo, sema wanatuibia hao wasimamizi wa hizo pesa. Wanajitahidi wabakii madarakani waendelee kuzipiga. Ukiona nguvu inayotumika kuchagua mayor wa jiji au mwenyekiti wa halmashauri unagundua kuna kitu kikubwa nyuma ya hiki cheo
viongozi wa chama kuomba hela kwenye mashirika ya umma, ukiwagomea unaondolewa faster
 
Kama tulivyoonesha dunia kwamba hatuna corona na hata mikutano ya kampeni inajaa na hatusikia watu kuanguka kwa corona labda kwa joto kali,sasa ni kipi kilichoshindikana kusema hizo pesa hatuzitaki ziende labda Kenya ambako bado tatizo liko.
Mkuu, , naomba nicheke kwanza.

Unatakiwa uelewe mzungu hana shida na hela. Ni kama ana hela isiyo isha. Ukijiuliza inatoka wapi hiyo ni topic nyingine ndefu. Ila siku zote mzungu ana shida na man power aka human resource aka utumwa. Na amefanikiwa.
 
Japo umeandika haraka haraka sana ila nimevumulia kusoma, sasa koo limenikauka acha ninywe maji kidogo.

Tanzania tumepewa bilioni 70 na bila aibu tumepokea, kwa corona ipi!!
Aisee, hivi sisi si tulimlilia Mungu na corona ikaondoka jamani! corona ipi tena tunayoenda kupambana nayo?
 
Tayari kuna fedha nyingine zinakuja kupambana na corona, wale wale wanaoitwa mabeberu wanatoa fedha kuja hapa hapa nchini na soon mtaona zikipokelewa na mzee baba au muwakilishi wake.

Tumebembelezwa kuitangazia dubia ndugu covid hayupo ila tunapokea fedhaaaa, cha ajabu baada ya kuzipokea zitaenda moja kwa moja kwenye yale mamiradi pendwa.
 
Kwani ukipokea fedha ya CORONA lazima uitumie kupambana na CORONA?? Akili kichwani, inakuja ya Corona sie tunatupia kwenye SGR, Inakuja ya ZIKA tunatupia kwenye Bwawa la Nyerere wakija kustuka na sie tunamiliki treni ya Umeme. Mabeberu Wananuuuuuuuuna na Vibaraka wao wao Wanabweeeeeeeeeeka! Jiwe gizani
 
Mkuu Ulitaka ziende kwenye mikono ya wachache kama walivyofanya Kenya? Jpm ni moja ya viongozi wasiokuwa na umimi,hakika anafaaa sana
 
Japo umeandika haraka haraka sana ila nimevumulia kusoma, sasa koo limenikauka acha ninywe maji kidogo.

Tanzania tumepewa bilioni 70 na bila aibu tumepokea, kwa corona ipi!!
hoja yako ina mantiki. Kwa hio mmepokea pesa ya mnaowaita MABEBERU? Na shida ya hawa jamaa mabeberu ukishachukua pesa yap lazima utume taarifa kwao jinsi ilivyosaidia kupambana na corona (ambayo haipo).
 
Kwani ukipokea fedha ya CORONA lazima uitumie kupambana na CORONA?? Akili kichwani, inakuja ya Corona sie tunatupia kwenye SGR, Inakuja ya ZIKA tunatupia kwenye Bwawa la Nyerere wakija kustuka na sie tunamiliki treni ya Umeme. Mabeberu Wananuuuuuuuuna na Vibaraka wao wao Wanabweeeeeeeeeeka! Jiwe gizani
👇
We ukienda hotel unalipiwa tu
 
Mkuu, , naomba nicheke kwanza.

Unatakiwa uelewe mzungu hana shida na hela. Ni kama ana hela isiyo isha. Ukijiuliza inatoka wapi hiyo ni topic nyingine ndefu. Ila siku zote mzungu ana shida na man power aka human resource aka utumwa. Na amefanikiwa.
kuna rafiki angu anafanya kazi bank aliwahi nambia wazungu wanatengeza pesa kulingana na mahitaji yao lakini sisi tunatengeza kulingana na uchumi wetu, means wao wanazo pesa zilizo nje ya system ya uchumi wao zinazowawezesha kutimiza matakwa yao
 
Back
Top Bottom