Pesa kikwazo cha Demokrasia

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,537
5,618
Nilileta huu uzi wiki jana kuhusu kazi tulokuwa nimedhamiria kuifanya ya kukusanya maoni ya wakazi wa Kigamboni abayo imekamilika leo.

Uzi wenyewe ni huu:
Taarifa Kwa Umma: Fact Finding Mission-Jimbo la Kigamboni
Baada ya kufanya stadi yangu kwa siku tatu tangu jumapili ya tarehe 9 August mpaka tarehe 11agosti Haya ndio yaliyojiri

Kwanza tulifanikiwa kufika KATA zote za Wilaya ya Kigamboni pamoja itaa kadhaa ikiwamo
Pemba Mnazi,Buyuni,Kimbiji,Kidagaa,Avic town,Cheka,Dege,Malimbika,Gezaulole,Kibugumo,Mji mwema,Vijibweni,Kibada,Mji mwema,Feri n.k.

Tulifanikiwa kuzungumza na jumla ya Wakazi 3000 wa Kigamboni moja kwa moja ambapo tulizingumza nao kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo jamii,uchumi,siasa,maendeleo na uwajibikaji.

Hata hivyo jambo moja ambalo nimeliweka katika uzi huu ni kuhusu SUALA la gharama za uchaguzi kuwa Kikwazo cha ushiriki katika uongozi,Vijana wengi wenye sifa na utayari wa kuwa viongozi walishindwa kushiriki katika nafasi za uongozi kwa sababu ya kukosa kipato.Kwa mujibu wa Utafiti huu vijana hawa ambao wengi wana changamoto nyingi wakipewa uwezeshaji wa kifedha na kiuongozi wanaweza kusimama na kuwa viongozi.

Kwa kuwa kama sehemu ya mkakati tulilenga kuwaiinua vijana hawa basi tumeandaa mkakati wa haraka wa kuwawezesha vijana hawa kushiriki katika uchaguzi huu kama wagombea katika uchaguzi huu.

Sisi kama taasisi tutawapa mafunzo,miongozo,ushauri wa kitaalam pamoja na usimamizi katika kuhakikisha kwamba wnashiriki kikamilifua katika uchaguzi huu na kushinda.Vijana hawa wako tayari kusimama na kugombea uongozi kwa tiketi ya chama chochote cha siasa na kwa uwezo wao wanaamini kabisa kwamba watashinda.

Nimeleta suala hili humu jukwaani kwa sababu mbili.Kwanza ni kujadili juu namna commoditization of politics inavyoathiri ndoto za vijana kuwa viongozi na pili ni kuwaalika wadau wa mabadiliko na maendeleo ambao wameguswa kwa namna moja au nyingine kutoa support kwa vijana hawa ili waweze kushiriki katika uchaguzi huu.

Tayari tumechukua majina ya vija 20 ambao wako tayari kugombea nafasi za uongozi,udiwani na ubunge kwa nafasi za jimbo/kata na viti maalum.Tayari tuko katika mazungumzo na moja wapo ya chama cha upinzani cha siasa hapa nchini ili kiwapokeaa vijana hawa na kuwadhamini ili wapate kugoombea nafasi ya uongozi.Tunachohitaji kutoka kwa wadau kwanza ni maoni kuhusu mpango huu tulio nao iwapo unaweza kufanyika pia katika majimbo.

Pili ni kuomba michango ya kifedha ili kuwawezesha vijana hawa kugombea nafasi za uongozi,Ubunge,udiwani katika uchaguzi huu.Gharama za ushiriki wao katika kapeni hizi zimewekwa kuwa kati ya TZS MILIONO 1 hadi 2.5 kwa kila mgombea kwa kutegemea ukubwa wa kata na idadi ya wapiga kura.Hivyo niwaombe wadau wa mabadiliko kama sio washabiki wa kusindikiza basi mtuunge mkono katika hatua hii ili tuwawezeshe vijana hawa kushiriki katika uchaguzi huu.

Iwapo ungependa kumpa sapoti kijana yoyote kwa nafasi yoyote tafadhali tuwasiliane kwa email:mbungekigamboni20.Unaweza pia kuchangia kiasi kidogo kama vile gharama za kuchukua fomu za Ubunge na udiwani ambazo ni TZS 50,000 kwa kila mgombea,gharama za kutengeneze promotion items ambazo ni TZS 300,000 hadi 500,000 kwa kila mgombea.Gharama za spika kwa ajili ya PA,ambazo zina wastani wa bei wa kati yz TZS 180,000 hadi TZS 350,000.Gharama za usafiri na huduma za stationeries ambazo ni anuai.

Iwapo ungependa kuwachangia vijana hawa tafadhali tuwasiliane kwa emai: mbungekigamboni20@gmail.com au PM

Hii ni shughuli NOBLE kwa wapenda mabadiliko.Natumaini itapokelewa vyema na watu kujitoa kwa uzalendo
 
Back
Top Bottom