Peremende zenye bangi zauzwa mitaani

Peremende zenye bangi zauzwa mitaani

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Wizara ya afya nchini Kenya imetoa orodha ya Peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi, huenda zimesambazwa hadi Tanzania.

Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashangaza wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba ya maabara ya Serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu, keki na maandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Licha ya watoto kuzipenda bidhaa hizo, Serikali inataka vipigwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kuziuza.

Kupitia kwa barua kwenda kwa wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha Maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidhaa hizo zinaweza kupatikana.

Chanzo: BBC
 
Hapa kazi ipo, yaani hao jamaa wanataka kuuwa kizazin kijacho. Lakini utaona GTZ itakavyokawia ku react.
 
Sasa mbona hizo peremende n.k havijatajwa kwa majina watu tukachukua tahadhari mapema?
 
ujukue tena tahadhar jaman..baada ya kuzitafuta ule ili upate stimu..hahaa ushawahi kula mayai yaliyokaangiwa bange?matam hayooo uje utest one day...
 
Kwani ukila bangi ina madhara gani mbona kwetu majani ya bangi ni mboga?
 
au ndo zile pipi kali TROPICAL? wamezifanyia REMIX?
 
ujukue tena tahadhar jaman..baada ya kuzitafuta ule ili upate stimu..hahaa ushawahi kula mayai yaliyokaangiwa bange?matam hayooo uje utest one day...

Uwiiiiiii charty hufai kwakweli!
 
Last edited by a moderator:
Wabongo bana, kwa hiyo mnaona bangi ni mbayaa kushinda ngono holela na matusi!!!

Hivi huo mmea uliwakosea nini. Mbona hayajatajwa madhara ya kula chakula chenye bangi, refer Wahehe.

Cc Mphamvu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu platozoom chochote unachokitumia kama kinakubadilisha kwa namna yeyote tambua hicho ni kilevi, usiingieze mambo yanayohusu maslahi ya wananchi na mambo binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Hapa kazi ipo, yaani hao jamaa wanataka kuuwa kizazin kijacho. Lakini utaona GTZ itakavyokawia ku react.

Wakumbushe na wazizi pia waharakishe ku react. Hapo ndio tutafanikiwa haraka
 
Mwanangu zinauzwa pale lumumba we huwaon wakina stroke na lizabon wanavyoonges kibangebange hymu
ujukue tena tahadhar jaman..baada ya kuzitafuta ule ili upate stimu..hahaa ushawahi kula mayai yaliyokaangiwa bange?matam hayooo uje utest one day...
 
Wizara ya afya nchini Kenya imetoa orodha ya Peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi, huenda zimesambazwa hadi Tanzania.

Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashangaza wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba ya maabara ya Serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu, keki na maandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Licha ya watoto kuzipenda bidhaa hizo, Serikali inataka vipigwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kuziuza.

Kupitia kwa barua kwenda kwa wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha Maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidhaa hizo zinaweza kupatikana.

Chanzo: BBC

aiseeee sasa ninepata picha kamili.kumbeeeeee
ndo maana kuna viongozi wasomi wakubwa sana huwa wanatoa kauli tata na kutoa maamuzi ya kibange bange!!!!!.
na nimekuwa nikijiuliza tatizo ni nn?.
aaaa sasa nimeelewa yamkini ni watumiaji wakubwa wa pipi hizi.maana yake ni kuwa tunaidadi kubwa ya wavuta bange wasiojijua kubwa sana.
km mamuzi na kauli yabao la mkono!hii ni bange pipi.au ile ya laptop na 500m kwa waalimu nayo ni bange pipi na ile ya yule jamaa alohama ukawa na sababu akasema eti anasutwa na nafsi ile nayo ni bange pipi.
hata hii ya kusema lowasa ....ni bange pipi nayo.
 
Back
Top Bottom