Pepe aliwezaje, wengine wanashindwaje?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,916
1697616263630.jpg

Huwezi kusoma maisha ya aliyepata kuwa Rais wa Uruguay kuanznia 2010-2015, José Mujica, na ukaacha kushangaa hulka ya viongozi (hasa wa Afrika).

Jose au maarufu kama “Pepe”, kabla ya kuukwaa urais, alipigana msituni mpaka kuikomboa nchi toka utawala wa kididkteta; alipata kuiingiza kwenye wizi wa kuibia benki ili kufadhili harakati za ukombozi. Alikamatwa na kutoroka jela mara nne,alipigwa risasi mara sita na kuponea chupuchupu, aliteswa na kufungwa miaka myiaka isiyopungua 13!

Kwa rekodi ya kujitoa muhanga namna hiyo, Pepe angeweza kuwa mtu wa ngebe na maisha ya fahari baada ya kuupata urais. Labda, kama Mugabe, angekatalia madarakani kwa kisingizio cha kupigana msituni. Au, kama tulivyopata kusikia toka kwa mwanasiasa mmoja huko Zanzibar, Pepe angeweza kutamba kuwa chama kilicholeta mapinduzi hakiwezi kutolewa kwa makaratasi. Pepe hakufanya hivyo. Kwa namna ya kushangaza, aliendelea kuishi maisha ya kawaida kwenye nyumba ndogo ya mkewe shambani mwao akisusia kasiri la Ikulu na huduma zake zote. Aliendelea kusafiri kwa gari yake ya siku zote, VW mgongo wa kobe, badala ya kujinunulia Benzi au VX kama watawala wengi wa nchi masikini. Mara zote lijiendesha mwenyewe na hakuongozana na msafara wowote!

Falsafa ya Pepe inawataka viongozi kuishi kama kundi la raia walio wengi na si kama kundi la wachache waliobahatika. Anapinga uongozi wa kisiasa kuwa kazi ya anasa, pesa na tija bali mapenzi kwa nchi na moyo wa kujitolea. Jose hushangaa jinsi tunavyochanganya mambo na kufikiri kuwa tunawachagua watu ili wakawe wafalme wa kuishi kwenye makasri na kutembea kwenye mazuria mekundu; wanaopaswa kuishi maisha ya kula bata zaidi huku wakihudumiwa na wafanyakazi lukuki na kumiminiwa sifa na mapambio ya kila siku. Maisha ya namna hii, kwa maoni ya Pepe, huwataliki au kuwatenga kabisa viongozi na wananchi wao.

Ni rahisi kwa mtu kujinasibu kama mtetezi wa masikini na wanyonge huku akiendelea kuishi maisha ya kifahari, akisindikizwa na msafara wa magari 20 na helkopta juu. Pepe, alisaidia wanyonge kwa vitendo kwa kutoa asilimia 90 ya mshahara wake kusaidi watu masikini katika kipindi chote cha urais wake. kiongozi wa namna hii anaweza asifanikiwe kuleta maendeleo ya kuonekana kwenye macho kama wengi wetu tunavyotamani siku hizi, lakini ni kiongozi wa namna hii tu anayeweza kuleta chachu ya uadilifu katika—sifa ya muhimu kuliko jambo lolote katika ujenzi wa jamii ya maana!

Akiwajibu wale wanaomwita “Rais masikini” kuwahi kutokea, Pepe huwaambia kuwa “hawajui tafsiri ya neno utajiri!”.
 
View attachment 2785189
Huwezi kusoma maisha ya aliyepata kuwa Rais wa Uruguay kuanznia 2010-2015, José Mujica, na ukaacha kushangaa hulka ya viongozi (hasa wa Afrika).
imu kuliko jambo lolote katika ujenzi wa jamii ya maana!

Akiwajibu wale wanaomwita “Rais masikini” kuwahi kutokea, Pepe huwaambia kuwa “hawajui tafsiri ya neno utajiri!”.

Hata huyu ni mmoja wa watu hao:

images (4).jpeg
 
Back
Top Bottom