Enzi hizo Pepe Kalle na Hidaya Khamis Masawe

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,655
20,988
Mnamo Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kufanya onesho katika jiji la Arusha. Walipowasili Arusha, walikodi taksi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamama Hidaya Khamis Massawe.

Wakiwa kwenye taksi wakawa wanazungumza kilingala wakimsifia dereva bila kujua kuwa kumbe bi. Hidaya (dereva teksi) alikuwa anakijua kilingala kwani kutokana na mihangaiko yake ya kimaisha huko Zaire (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Pepe Kalle akastaajabu sana kumsikia Hidaya anazungumza kilingala. Alipomaliza onesho lake Arusha, Pepe Kalle akajiapiza kurejea Tanzania kwa ajili ya Hidaya.

Mwaka uliofuata, 1992, Pepe Kalle akarudi kweli Tanzania Arusha na akatunga wimbo kwa ajili ya Hidaya. Mume wa Hidaya, Mzee Massawe, alipong'amua kuwa ule wimbo "Hidaya" umetungwa mahsusi kwa ajili ya mke wake, akamtaliki siku hiyo hiyo.

Hidaya Khamis Masawe alifariki mwaka 2021 Arusha, mtaa wa Kaloleni.

IMG_20240229_114947_096.jpg
 
WIMBO ULITAMBA SANA MIAKA HYO.cha ajabu pepe anafariki watu wengi pale arusha walienda kwa hidaya kumpa pole.hidaya anarudi toka nairobi anakuta umati wa watu kwake.alishangaa sna kifo cha pepe haikumshutua aliona kawaida.lakini baada xa pole nyng kupewa hidaya ndyo aliona uzito wa kifo hicho nakujihesabu km mwanafamilia wa pepe(mke)
 
Mnamo Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kufanya onesho katika jiji la Arusha. Walipowasili Arusha, walikodi taksi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamama Hidaya Khamis Massawe.

Wakiwa kwenye taksi wakawa wanazungumza kilingala wakimsifia dereva bila kujua kuwa kumbe bi. Hidaya (dereva teksi) alikuwa anakijua kilingala kwani kutokana na mihangaiko yake ya kimaisha huko Zaire (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Pepe Kalle akastaajabu sana kumsikia Hidaya anazungumza kilingala. Alipomaliza onesho lake Arusha, Pepe Kalle akajiapiza kurejea Tanzania kwa ajili ya Hidaya.

Mwaka uliofuata, 1992, Pepe Kalle akarudi kweli Tanzania Arusha na akatunga wimbo kwa ajili ya Hidaya. Mume wa Hidaya, Mzee Massawe, alipong'amua kuwa ule wimbo "Hidaya" umetungwa mahsusi kwa ajili ya mke wake, akamtaliki siku hiyo hiyo.

Hidaya Khamis Masawe alifariki mwaka 2021 Arusha, mtaa wa Kaloleni.

View attachment 2919945
Mengine sawa lakini Late Hidaya hakuwahi kuwa TAXI Driver hata siku moja.
Hidaya ni aina ya wanawake wanaopenda kujirusha sana hasa linapokuja swala la kuvuta raha kuanzia muziki na kutafuna mirungi.

Hidaya walikutana na Pepe Kalle Sabasaba Hotel kabla haijauzwa na Kikwete kwa waarabu.Katika onyesho hilo Bibie Hidaya alikuwepo na kumrusha roho sana Mzee Mzima Pepe yaliyoendela na mambo ya chumbani hatupaswi kuyajadili.

Sidhani kama Hidaya alikuwa na ndoa,nikimfahamu tangu enzi hizo akiishi katika nyumba ya Marehemu Hussein Tumbo Langara mitaa ya Kaloleni.

Hidaya kabla ya umauti alifiwa na Binti yake aliyekuwa akiishi UK.
 
Watu walio wengi hawajiui kama huo wimbo alimsifia hidaya was kaloleni....mpaka sisi wa R ndo tunajua...Hidaya alikuwa kisu miaka hiyo...
 
Mengine sawa lakini Late Hidaya hakuwahi kuwa TAXI Driver hata siku moja.
Hidaya ni aina ya wanawake wanaopenda kujirusha sana hasa linapokuja swala la kuvuta raha kuanzia muziki na kutafuna mirungi.

Hidaya walikutana na Pepe Kalle Sabasaba Hotel kabla haijauzwa na Kikwete kwa waarabu.Katika onyesho hilo Bibie Hidaya alikuwepo na kumrusha roho sana Mzee Mzima Pepe yaliyoendela na mambo ya chumbani hatupaswi kuyajadili.

Sidhani kama Hidaya alikuwa na ndoa,nikimfahamu tangu enzi hizo akiishi katika nyumba ya Marehemu Hussein Tumbo Langara mitaa ya Kaloleni.

Hidaya kabla ya umauti alifiwa na Binti yake aliyekuwa akiishi UK.
Unamjua vizuri hiyo Binti yake tulisoma naye Arusha Sec
 
Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kutumbuiza mkoani Arusha.

Baada ya kufika Arusha, walikodi teksi iliyokuwa ikiendeshwa na mwanamke aitwaye Hidaya Khamis Massawe. Wakiwa ndani ya teksi walianza kuongea kwa lugha ya Lingala wakimsifu dereva teksi kwa jinsi alivyokuwa mzuri. Hata hivyo, Hidaya (dereva teksi)

alikuwa anafahamu lingala kutokana na shughuli zake za kibiashara huko RD Congo. Pepe Kalle alishtuka sana baada ya kumsikia Hidaya akizungumza kwa lugha ya Lingala. Baada ya kumaliza shoo yao jijini Arusha, Pepe Kalle aliahidi kuwa atarejea Tanzania kwa Hidaya.

Mwaka uliofuata wa 1992, Pepe Kalle kweli alirudi Tanzania Arusha na kutunga wimbo wa Hidaya.

Mume wa Hidaya Mzee Massawe, baada ya kujua kuwa wimbo wa Hidaya alitungiwa mkewe aliamua kuachana naye na kumuacha siku hiyo hiyo.

Hidaya khamis masawe alifariki mwaka 2021 Arusha mtaa wa Kaloleni.

1709452177931.jpg
 
Back
Top Bottom