Penzi lenye Maumivu

Mwanaume wa dizaini hii ni bora kuachana tu maana anabadilisha kyuma weee. Baada ya yule wa kwanza bado anaendelea kuhangaika. Mpaka kawa muuaji
 
Mwanaume wa dizaini hii ni bora kuachana tu maana anabadilisha kyuma weee. Baada ya yule wa kwanza bado anaendelea kuhangaika. Mpaka kawa muuaji
kua na mwanaume akaridhika na ww mmoja shukuru na kila aiku umuombee
 
Amen!huu ushauri unanihusu 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PENZI LENYE MAUMIVU-12
Mtunzi:Juma Hiza
Simu:0712988278
Nilimfikiria Nancy kuliko kawaida,akili yangu ilichanganyikiwa kwa muda huo, nilikuwa nikimuwaza yeye tu. Niliukumbuka uzuri aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu lakini ugonjwa wa Mama yake ukanifanya nizidi kuingiwa na huruma mara dufu. Nilimuhurumia mno! Wala hakukuwa kuna kipindi moyo wangu ulikuwa katika huruma kama kipindi hicho.
Iliwezekanaje katika hii dunia msichana mrembo kama Nancy aishi maisha ya kuteseka? Maisha yenye dhiki kiasi hicho? Nilijiuliza maswali ambayo yalizidi kunifanya nimuonee huruma.
Dhiki iliyokuwa imetawala katika maisha yake, ilimfanya aonekane kuwa mwanamke wa miaka hamsini wakati bado alikuwa msichana mbichi kabisa. Alikosa matunzo tu!
Sikutaka kupoteza muda hata kidogo, nilichokifanya nilienda mpaka nyumbani kwao Kigogo kumtembelea, huko alikuwa akiishi na Mama yake katika chumba kimoja walichopanga.
Mazingira ya chumba hicho kiukweli hayakuwa mazuri. Kilionekana kuwa kibovu, kilichakaa mno, kilifanania na banda la kufugia mbwa. Yaani kwa macho ya haraka haraka ukiwa nje huwezi kuamini kama ndani kuna binadamu wanaishi.
Nancy alinitambulisha kwa Mama yake kuwa mimi ni rafiki yake ambaye niliwahi kusoma naye shule moja miaka kadhaa iliyopita. Mama yake alitabasamu baada ya kusikia hivyo, akanipa mkono kisha akanikaribisha tena. Sauti yake ilitoka kwa shida lakini alijitahidi kuzungumza hivyohivyo.
Siku hiyo nilizungumza mambo mengi sana na Mama yake Nancy, ulikuwa ni mwanzo wa yeye kunifahamu, alifurahi mno kuniona. Nilimueleza mpango wangu wa kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na gharama zote ambazo zingehitajika zingekuwa juu yangu.Nilipokitazama kile chumba walichokuwa wakiishi, hakikuridhisha kuishi msichana kama Nancy ambaye tayari nilishampenda.Nilimueleza pia kuhusu nia yangu ya kutaka kuyabadilisha maisha yao, sikutaka waendelee kuishi maisha yale yenye dhiki.
Nilipomueleza hayo alishtuka, hakutaka kuamini kama kile nilichomueleza kwa wakati huo nilikimaanisha. Akabaki akinishangaa tu, ni kweli alikuwa na shida na hakujua ni kwa namna gani angeweza kuzitatua lakini maneno yangu hayakuonekana yakimuingia akilini.
Nilichokizungumza siku hiyo ndicho nilichokitekeleza.Nilifanya mpango wa kumpeleka Mama yake Nancy hospitalini ambapo aliweza kufanyiwa upasuaji wa uvimbe aliyokuwa nao tumboni na baadae kupona kabisa.
Sikutaka maisha yao yaendelee kubaki kuwa ni ya Kigogo tena katika kile chumba ambacho kilionekana kuchoka na kuchakaa. Niliwapangishia nyumba maeneo ya Sinza, ilikuwa ni nyumba kubwa ambayo ilikuwa na kila kitu walichokuwa wakikihitaji.
Hatimaye nikafanikiwa kuyabadilisha maisha yao kutoka kuishi Kigogo kwenye maisha yenye dhiki mpaka Sinza ambapo hakukuwa na shida tena. Kila walichokuwa wakikihitaji walikipata tena kwa wakati husika.
Mama Nancy alinishukuru sana, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kunilipa kama shukrani kwa msaada ambao niliutoa kwake. Kiukweli alikosa cha kunieleza, akabaki akiniambiakuwa yale yote niliyomtendea kama wema alimuachia Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye ambaye angeweza kunilipa.
Kipindi hicho Nancy tayari nilishamuachisha kazi ya uhudumu wa baa, sikutaka aendelee kuifanya tena kazi hiyo ambayo ilikuwa na changamoto lukuki, kama tatizo lilikuwa ni pesa tu nilikuwa nazo na nilikuwa nikimpa kiasi chochote alichokuwa akikitaka.
Nilimgharamia kwa kila kitu, sikutaka kumuona akiteseka. Naweza kusema nilikuwa ni mtu pekee ambaye nilifanikiwa kuirudisha furaha yake ambayo ilikuwa imepotea kipindi cha nyuma.
“Kelvin sijui nikushukuru vipi, umekuwa msaada mkubwa sana katika maisha yangu. Kiukweli nashindwa kuelezea ila nakushukuru sana tena sana,” aliniambia Nancy.
“Usijali ni jambo la kawaida mbona,” nilimwambia.
“Hapana kwako linaweza kuwa ni la kawaida lakini kwangu naliona ni kubwa mno, haikuwa rahisi kuamini kama kuna siku nitakuwa na furaha tena,” aliniambia.
“Kwanini?”
“Niliipoteza furaha yangu, nilikata tamaa lakini tangu nilipokutana na wewe umekuwa mtu pekee uliyeyapigania maisha yangu, Kelvin wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”
“Nancy sijui nikwambie nini ila kiukweli hata mimi sielewi kwanini nimekuwa na moyo wa huruma kiasi hiki, nimekusaidia ingawa sijawahi kukufahamu hapo kabla,” nilimwambia.
Kumbuka mpaka kufikia wakati huo nilikuwa bado sijamtongoza Nancy, sikumtamkia neon lolote la mapenzi kabisa. Nilifanya mambo yote kama kumsaidia lakini kuna kitu nilitarajia kukipata hivyo sikutaka kutumia nguvu nyingi sana.
Alinisimulia historia yake ya mapenzi. Mapenzi yalikuwa yamempa maumivu makali sana katika moyo wake, hakuyaamini tena, aliyachukia mno. Alipokuwa akinieleza hayo machozi yalikuwa yakimdondoka mashavuni mwake.
Aliwahi kula kiapo kwamba katika maisha yake asingekuja kupenda ama kujihusisha na mahusiano ya kimapenzina mwanaume yoyote yule lakini tangu alipokutana na mimi kiapo chake hicho kilianza kukosa nguvu.
Mambo ambayo nilikuwa nimemfanyia yalikuwa ni makubwa mno, hakujua ni kwa vipi alitakiwa kunilipa. Kila siku ndiyo swali lake kubwa ambalo alikuwa akiniuliza lakini jibu langu lilikuwa ni lile lile kwamba nilifanya yale yote kama kuonyesha kuguswa kwa kile kilichokuwa kimemtokea.
Unajua niliamua kujifanya msamaria mwema kwasababu nilifahamu hata iweje ni lazima Nancy angekuwa wangu tu. Ukaribu ambao nilikuwa nao kwake na jinsi ambavyo Mama yake alivyokuwa akinipenda isingekuwa ni kazi ngumu mimi kuwa naye.
Baada ya kupita wiki tatu tangu nilipoweza kumsaidia Mama yake pamoja na kuwatoa katika maisha ya dhiki, siku moja Nancy alinipigia simu na kuniambia kwamba alihitaji tuonane sehemu fulani kwani alikuwa na mazungumzo muhimu sana na mimi.
“Mazungumzo ya kheri ama ya shari?” nilimuuliza huku nikitabasamu.
“Ya kheri kuna kitu nataka kukwambia,” alinijibu kisha tukapanga kukutana katika mgahawa wa KFC uliyokuwepo pale Mlimani City. Ndani ya masaa sita tukawa tayari tupo ndani ya mgahawa huo. Nancy ndiye aliyenikuta, nikampokea kwa kumbato kisha akaketi na mazungumzo yetu kuanza.
Alipendeza sana siku hiyo, alikuwa amevalia sketi fupi ambayo ilipanda mpaka juu ya mapaja. Nilimsifia lakini kutokana na aibu ambazo alikuwa nazo hakuweza kuitikia.
Hilo halikuwa tatizo, nilichoamua kumwambia ni kwamba tayari nilikuwa mbele yake kwa wakati huo na nilikuwa nikimsikiliza.
“Kelvin,” aliniita kana kwamba hakuwa akilifahamu jina langu. Alikuwa ni mwenye wasiwasi mno.
“Niambie,” nilisema kisha nikawa makini kumsikiliza.
“Kuna kitu nataka kukueleza lakini nafsi yangu inasita, sijui utanifikiria vipi lakini kiukweli nimeshindwa kujizuia,” aliniambia.
“Ni kitu gani hicho ambacho unashindwa kunieleza?” nilimuuliza huku nikijifanya sielewi ni nini ambacho alitaka kunieleza.
Nilimpa kazi ngumu mno ya kutafuta ujasiri wa kunieleza kile ambacho alihitaji nikifahamu. Baada ya kumaliza kuuzunguka mmbuyu mwisho ndipo aliweza kunieleza kwamba alinipenda na alinihitaji sana.
Kwa jinsi alivyokuwa akinieleza Nancy, aliniona kuwa ni mtu mwema sana, niliyejawa na roho ya huruma, kitendo cha kunitamkia kwamba alinipenda na kuhitaji niwe naye kimapenzi aliamini kwa asilimia kubwa kwamba nisingeweza kumjeruhi moyo wake ambao tayari ulikuwa kwenye maumivu ya kuumizwa.
Muda ambao Nancy alikuwa akinieleza hayo hakujua kama nilikuwa nina mke na mtoto ambaye sikuwa nikiwajali, niliwachukia na kuwafanyia unyama wa kila aina.
Simu yangu ilikuwa ikiita, mke wangu ndiye alikuwa akinipigia. Sikuipokea simu yake, nilichoamua kukifanya niliikata na kuendelea kuzungumza na Nancy.
“Mbona umekata simu?” aliniuliza huku akionekana kushangaa.
“Hana umuhimu kama wewe, tuendelee,” nilimwambiakisha akatabasamu.
Sikutaka kujifanya mgumu sana kwamba kitendo cha Nancy kuniambia ananipenda nimkatalie kwa kuwa nilioa. Hilo halikutokea. Nilimkubalia ombi lake kisha tukawa wapenzi.
Nancy alifurahi sana, hakuamini kama ombi lake lingefanikiwa.Hilo ndilo nilihitaji kuliona, nilitengeneza mazingira ya kuonekana mwema kiasi kwamba hata kama ningeendelea na mchezo wangu wa kumsaliti ingekuwa ni vigumu kuamini kwani tayari aliniona kuwa kama Malaika.
Wakati Nancy alipokuwa ni mwenye furaha na kujiona ni mwenye bahati kufanikiwa kuwa na mimi, upande wa piliLillian hakuwa ni mwenye furaha kabisa. Maumivu kwake yalikuwa kama muendelezo wa Tamthiliya ambayo haikujulikana mwisho wake ni upi hasa.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumapili mahali hapahapa
 
PENZI LENYE MAUMIVU-13
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278
“Umetoka wapi mume wangu?” lilikuwa ni swali la kwanza kuniuliza Lillian, niliporudi nyumbani siku hiyo majira ya usiku.
“Na mbona nilikuwa nakupigia simu zangu hupokei vipi una tatizo gani?” aliniuliza lakini sikumjibu kitu, nilimpita kama sikumsikia, nikaingia bafuni kuoga, nilipomaliza nikavaa mavazi ya kulalia kisha nikapanda kitandani.
“Subiri kwanza Kevi mbona sikuelewi una nini lakini?” aliniuliza.
“Kuhusu nini?” nilimuuliza kwa ghadhabu, uso nilikuwa nimeukunja.
“Chakula kipo tayari mezani,” aliniambia.
“Hapana sijisikii kula leo.”
“Mume wangu.”
“Nimesema sijisikii kul leo,” nilimwambia kisha nikageuka upande wa pili, nikajifunika shuka gubigubi.
Jibu hilo lilimshtua sana Lillian, kilichomuumiza zaidi ni kitendo cha mimi kumpa mgongo na kumpuuzia. Hazikupita dakika nyingi nikamsikia akianza kulia.Sikumuuliza hata hali ya Brighton ambaye alikuwa amelala muda huo,nilichoamua kukifanya nikauchapa usingizi wa hatari.
Unajua sisi wanaume tunapopata mafanikio kidogo tu huwa tuna kawaida moja. Huwa tunaamini sana katika maamuzi. Muda mwingine tunapoamua kuchukua maamuzi huwa tunajiona tupo sahihi pasipo kujua kuwandani ya hayo hayo maamuzi tunayoyachukua kuna mtu mwingine tunamuumiza tena maumivu yasiyosimulika.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu. Nilikuwa nina mafanikio makubwa sana katikamaisha yangu hata nilipoamua kutembea na wasichana wengine bado nilijiona kuwa sahihi.
Kuna usemi usemao kuwa mbele ya mafanikio ya mwanaume siku zote nyuma yake yupo mwanamke shupavu lakini kwangu haikuwa hivyo. Mbele ya mafanikio yangu nyuma yake kulikuwa kuna mwanamke ambaye kila siku alikuwa ni mtu wa kulia.
****
Siku iliyofuata nilichelewa kuamka, niliposhtuka kutoka usingizi sikumuona mke wangu wala mwanangu, nikaamini moja kwa moja waliamka kabla yangu.
Nilipotazama pembeni ya kitanda nilioa nguo ambazo aliniandalia mke wangu kwa ajili ya kuvaa siku hiyo. Nilitabasamu tabasamu la kumaanisha kuwa ni kama vile alijisumbua kwani sikuwa nikimpenda hata kidogo.
Niliamka na kwenda bafuni kuoga, nilipomaliza nilirudi nikavaa zile nguo alizoziandaa mke wangu. Dadika chache baada ya kumaliza kuvaa mara aliingia mke wangu chumbani, akakuta nikimalizia kufunga kifungo cha mwisho cha shati.
“Wow umependeza sana mume wangu,” aliniambia huku akinitolea tabasamu pana.
“Asante,” nilimwambia lakini sikutaka kumuonyesha tabasamu hata la uongo.
Hilo hakujali kwani alishanizoea kuwa katika hali hiyo, alichoamua ni kuniambia kwamba chai ilikuwa tayari kwa muda huo hivyo nilitakiwa kwenda kunywa.
Aliponiambia hivyo nilikataa, nilisingizia kuwa bize siku hiyo hivyo nisingeweza kunywa chai hasa kwa muda kama ule ambao nilikuwa nimechelewa.
Kutokana na udhaifu mkubwa aliyokuwa nao mke wangu alishindwa kunizuia nisiondoke, ilibidi akubaliane na kile nilichomueleza japokuwa hakikuwa na ukweli.
Muda ambao nilikuwa nikimuaga Lillian kwamba nilikuwa nikienda kuweka mambo yangu sawa ya kibiashara. Niliwasiliana na Nancy, nikamwambia kwamba asubuhi ya siku hiyo nilihitaji kunywa chai ya nyumbani hivyo nilimwambia aniandalie mambo mazuri.
Nancy alifurahi sana baada kumwambia hivyo, ukizingatia kwamba penzi ndiyo kwanza lilikuwa jipya alifanya kila alichoweza ilimradi azidi kunikoleza.
Baada ya masaa kadhaa kupita, hatimaye niliweza kufika Sinza kwenye ile nyumba niliyompangishia Nancy pamoja na Mama yake. Nilikaribishwa ndani kama mfalme, Mama yake Nancy muda wote alikuwa akitabasamu tu.
Mpaka kufikia muda huo Mama yake Nancy alikuwa hafahamu lolote kuhusu uhusiano wetu wa kimapenzi. Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilibaki kuwa ni siri yetu.
Baada ya kumaliza kunywa chai, mazungumzo yalianza. Nancy alishindwa kujizuia. Ilibidi amueleze mama yake ukweli kuhusu uhusiano wetu. Mama yake Nancy ni kama vile alitarajia kusikia kitu kama kile kikitokea kwani hata pale ambapo Nancy alipoamua kumueleza hakuonekana akishtuka kabisa.
Pamoja na umalaya wangu wote lakini Nancy ndiye msichana pekee niliyempenda mpaka kufikia hatua nikapanga kumuoakabisa ukitofautisha na wasichana wengine ambao nilitembea nao na mwisho wa siku nikawaacha na maumivu makali yasiyosimulika.
Licha ya kwamba dini yangu haikuruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja lakini nilipanga kumuoa Nancy, hapa ni baada ya Mama yake kuniuliza juu ya mipango yangu kwa mwanaye.
Wazo lililonijia kichwani mwangu lilikuwa ni kwenda kumfukuza Lillian, niliamini kwa kufanya hivyo ni lazima mpango wangu wa kwenda kumuoa Nancy ungefanikiwa tena bila kipingamizi chochote.
“Nimekuvumilia vya kutosha leo lazima nikufuze nyumbani kwangu,” nilijisema wakati nilipokuwa ndani ya gari nikirudi nyumbani. Nilikuwa nimedhamiria kwenda kumfukuza mke wangu.
Nilipofika Bamaga kabla sijakata kona kushoto kuelekea Mwenge, dakika chache tangu nilipoingia katika barabara hiyo ghafla! Nilipata ajali mbaya sana. Lorilililokuwa linatokea upande wa kulia lilifeli breki baada ya taa nyekundu kuwaka. Lilikuja na kunigonga upande wa kulia wa ubavuni mwa gari yangu.
Nakumbuka gari yangu ilipinduka mara tatu mpaka kuingia mtaroni na baada ya hapo sikukumbuka tena kilichotokea, nilikumbwa na usingizi wa nusu kifo
 
ukufe tu kwakwel

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…