Penzi lenye Maumivu

Nimeandika hadithi Facebook kwa miaka Mitano, unakwenda mwaka wa sita sasa. Katika kipindi chote hicho nilikuwa najitolea, kujitangaza na hata kuwaburudisha wale watu wanaojisikia upweke kukaa nyumbani katika hali ya ukimya.
Lakini pia nimefanya hivyo kwa sababu nilitaka kuwafundisha watu kuhusu ulimwengu wasioujua kabisa, ulimwengu ambao watu wengi wangependa sana kuishi.
Ni safari ndefu mno, tena kipindi hicho kukiwa hakuna hata wasomaji lakini bado nilipambana mpaka kufikia leo hii. Nilishadharauliwa humu, nikapuuziwa na kutukana lakini sikukoma kwa kuwa nilijua kile kilichokuwa ndani yangu.
Leo ninapokatisha simulizi fulani haimaanishi nimechoka kuandika, wakati mwingine ninafanya hivyo ili uone thamani ya mwandishi, ili moyo wako kidogo uumie, halafu uone kwamba ila jamaa anafanya kazi kubwa mno.
Leo ukipewa chakula, ukala, hutoona thamani ya yule anayekupa chakula, kwa sababu tu kila siku unashiba. Ila mtu huyo akuache kwa siku mbili asikupe chakula, na siku akaja kukupa, ni lazima utamuona kuwa mtu wa thamani kuliko wote katika dunia hii. Ndivyo ilivyo kwa waandishi.
Wengine wanahisi kuandika ni jambo jepesi mno, haipo hivyo. Mbaya zaidi wengine wanawadharau waandishi, kisa anaandika mitandaoni, au kisa tu ni mwandishi mdogo, ndugu zangu, kuandika ni wito, kipaji. Wangapi walikuwa wakiandika lakini sasa hivi wamepotea? Kama hauna wito wa kufanya kazi hii, nimeandika hadithi kipindi chote hicho lengo lilikuwa mtu akiuliza kuhusu waandishi wa mitandaoni, jina langu liwe kwenye tano bora.
Nimeikatisha hadithi ya PENZI LENYE MAUMIVU. Ni makusudi kwa kuwa nataka kuitolea kitabu kama mlivyoomba. Wale ambao wanasema iendelezee jua hao hawana huruma na wewe, ni watu wasiothamini kile kilichokuwa ndani yako. Mtu yeyote anayemthamini mwandishi, asingesema kitu kama hicho.
Nitaanza hadithi mpya, nadhani leo, kesho au keshokutwa. Tuendelee kuwa pamoja. Hiyo haitokatwa, itaendelea mpaka mwisho. Watu wote nitahitaji mtuunge mkono waandishi, jueni wanafanya kazi kubwa ambayo wewe huwezi kuifanya kwa kuwa huiwezi. Hebu thamini hata muda wao, thamini kila kitu kuhusu wao kwa kuwa wanarisk mambo mengi kwa ajili yako.
Tukumbuke kuwa kitabu cha PENZI LENYE MAUMIVU bado kinaandaliwa na kitakuwa sokoni hivi karibuni...tuendelee kusubiri.🙏
Juma Hiza Stories.✍🏿
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom