Penzi la Mbosnia likauwa………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Penzi la Mbosnia likauwa………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 30, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni siku ya Ijumaa ya Julai 21, 1995, Nicholas Tucker, afisa wa cheo cha juu katika jeshi la anga la nchini Uingereza akiwa na mkewe aitwae Carol, alikuwa akiendesha gari lake aina ya Ford Fiesta, kurejea nyumbani wakitokea kwenye mghahawa mmoja uliojulikana kwa jina la Red Lion Pub ulioko katika kijiji cha ICKlingham katika mji wa Sufffolk nchini Uingereza.

  Tucker alikuwa akiishi katika eneo la RAF Honnington, eneo ambalo ndipo yalipo makazi ya askari wa kikosi cha anga cha nchi hiyo. Wakati wakikaribia daraja, Tucker aliona kitu kama mnyama akikatiza barabarani, mara ghafla katika hali ya kumkwepa yule mnyama ambaye alikuja kujulikana baadae kwamba alikuwa ni Panda, gari yake ilipoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni. Kwa mujibu wa mvuvi mmoja aliyekuwa jirani na eneo la tukio alisema kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa nne na nusu usiku, ndipo aliposikia mkwaruzo wa tairi la gari kama vile linapoteza mwelekeo au kufungwa breki za ghafla.Alipofika kwenye eneo a ajali alikuta gari aina ya ford Fiesta ikiwa imezama mtoni.

  Akisaidiana na watu wengine walifanikwa kumtoa Tucker ndani ya gari lakini akiwa amepoteza fahamu huku akivuja damu kichwani kutokana na jeraha alilolipata kwenye ajali hiyo. Baadae Polisi walifahamishwa na walipofika ndipo walipouona mwili wa mke wa Tucker, Carol ukiwa unaelea chini ya daraja. Wafanyakazi wa huduma ya kwanza walijaribu kumpa msaada ili kuokoa maisha yake, lakini hawakufanikiwa na hivyo kutangaza rasmi kwamba Carol alifariki pale pale kwenye eneo la ajali.
  Tucker ambaye naye kama mkewe alipatiwa huduma ya kwanza palepale kwenye eneo la ajali alirejewa na fahamu, na kwa mujibu wa maelezo yake wakati akihojiwa na askari wa usalama barabarani alisema kwamba, alikuwa akimkwepa mnyama aina ya Panda ambaye aliiingia ghafla barabarani na hakujua kwamba alikuwa jirani na daraja na ndipo aliposhtukia anatumbukia mtoni.

  Maelezo ya Tucker kuhusiana na ajali ile yalichukuliwa kama yalivyo. Hata hivyo, siku iliyofuata baada ya askari wazoefu wa usalama barabarani kufika kwenye eneo la ajali, walikuja kugundua kwamba, ajali ile haikutokea katika mazingira ambayo Tucker alielezea na
  hapo ndipo askari wa upelelezi walipoanza kuangalia maisha ya ndoa ya Tucker na mkewe Carol ili kujua kama ile ajali ilisababishwa na Tucker kwa makusudi au la. Wakati huohuo mwili wa mkewe ulipelekwa kwa wataalamu ili kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua sababu hasa ya kifo chake. Kwa haraka Polisi walikuja kugundua kwamba, si siku nyingi kabla ya ile ajali kutokea Tucker alikuwa amekata bima katika makampuni tofauti tofauti yenye thamani ya kiasi cha dola 200,000 ambazo andelipwa iwapo yeye Tucker au mkewe Carol angetokea mmojawapo angefariki kwa ajali.

  Hata hivyo, askari wa upelelezi walipochunguza zaidi uhusiano wa Tucker na mkewe Carol walikuja kugundua matatizo makubwa yaliyoikumba ndoa yao katika siku za karibuni Taarifa zilionesha kwamba Nicholas Tucker ambaye alikuwa na umri wa miaka 44 wakati huo, alikuwa ameishi na mkewe Carol wa miaka 20 huku wakiwa wamefanikiwa kupata watoto kadhaa. Katika kipindi cha mwanzo cha ndoa yao inasemekana ilikuwa ni imara yenye upendo na amani, wakati huo Carol alikuwa ni mwembamba na mwenye umbo la kuvutia hasa. Hata hivyo baada ya kuzaa, Carol alianza kunenepa ghafla na kuwa na mwili wa tipwa tipwa kiasi cha kufikia uzito wa kilo 95.

  Hapo ndipo ladha ya upendo wa awali ilipotea na tendo la ndoa kuwa la baridi. Ingawa watoto wao walishakuwa wakubwa, lakini kwa upande wa wazazi wao mapenzi yao yalipungua kwa kiasi kikubwa. Historia inaonyesha kwamba, Tucker alikuwa ni mtalaamu wa silaha za Nyukilia, Baiolojia na silaha za Kemikali katika jeshi la anga la nchini Uingereza. Katika kipindi cha miaka 27 alichotumikia jeshi, alifanikiwa kutumikia katika nchi za Ujerumani. Cyprus, Belize, Ireland Kaskazini na hata katika vita ya Ghuba mnamo mwaka 1994.

  Wakati ajali inamkuta alikuwa ndiyo amerejea nchini mwake akitokea nchini Bosnia alikokuwa amekwenda kikazi na alikuwa amekaa kwa takribani miezi sita na alikuwa yupo katika kipindi cha kustaafu rasmi ambapo angelipwa mafao yake yote ikiwa na pamoja na kutunikiwa nishani ya juu ya ya heshima. Taarifa zinaonyesha kwamba mnamo Januari 1995, Tucker aliteuliwa na umoja wa mataifa kuwa mjumbe wa amani nchini Bosnia ambapo alipangiwa kufanya shughuli hiyo katika mji wa Krajina. Alipofika katika kituo chake cha kazi, Tucker alipewa mkalimani ambaye atafuatana naye katika kipindi chote ambacho angekaa Bosnia. Mkalimani huyo hakuwa mwingine bali binti mbichi wa Kibosnia aliyejulikana kwa jina la Dijana Dudukovic. Binti huyu ambaye alikuwa na miaka 21 wakati huo alikuwa ni mzuri kwa vipimo vya kimwili. Wakati Tucker anavutiwa na binti huyu kiasi cha kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, lakini kwa upande wa Dijana alikuwa anamuona Tucker kama Passport yake ya kumtoa katika eneo lile la vita la Bosnia.

  Alishafanya majaribio kadhaa ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wajumbe kadhaa wa amani waliowahi kutumwa nchini humo ili aweze kuondoka nao baada ya muda wao wa kuwepo nchini Bosnia kwisha, lakini hakufanikiwa. Baada ya kumpata Tucker aliona huo ndio wakati muafaka wa kuitumia nafasi ile, kwani kwa muda mfupi aliweza kumlewesha Tucker kwa mapenzi motomoto, ambayo hakuwa akiyapata kutoka kwa mke wake, hadi baba wa watu akachanganyikiwa. Kwa muda mfupi, Dijana alikuwa amemshika Tucker hasa na hata ilipofika Mei 1995, Tucker alirejea likizo nyumbani kwao nchini Uingereza ambapo aliwaonyesha wafanyakazi wenzake picha nyingi alizopiga akiwa na Dijana wakiwa katika maeneo tofauti ya starehe nchini Bosnia.

  Likizo yake ilipoisha Tucker alirejea nchini Bosinia ili kuendelea na kazi yake, hata hivyo lilikuwa ni jambo la muda tu, kwani miongoni mwa zile picha ambazo aliwaachia rafiki zake, alizopiga na Dijana zilifika mikononi mwa mkewe. Kitendo cha mkewe kuona zile picha kilimuudhu sana kiasi cha kumuandikia mumewe barua kumweleza hisia zake. Kwa maneno yake mwenyewe Carol aliandika. ‘Nimekasirishwa sana na picha nilizoziona ambazo umepiga na binti wa Ki-Bosnia mkiwa katika mikao ya kimapenzi. Mke yeyote angekasirishwa na hilo.' Pamoja na kuandikiwa barua ya kuonywa na mkewe, lakini Tucker aliendelea na uhusiano wa kimapenzi na Dijana tena bila kificho, na kuna wakati alikuwa akiandamana naye hadi London nchini uingereza, akiwa ameenda kule kikazi ambapo inasemekana Tucker alishawahi kuaomba aongezwe miezi miwili ya kukaa nchini Bosnia, ombi ambalo lilikataliwa mwanzoni mwa Julai 1995.Tucker alirejea nchini Uingereza na kuripoti katika kituo chake cha kazi akijiandaa kustaafu.

  Nyumbani kwake alikuta hali si shwari kwani alikuta ndoa yake ina ufa mkubwa. Baada ya kukaa kwa siku kadhaa huku kukiwa hakuna maelewano mazuri na mkewe, Tucker alimshauri mkewe watoke kwa matembezi ya usiku na kupata chakula cha usiku nje ya nyumbani ili wamalize tofauti zao. Ingawa mkewe alikuwa amekasirishwa na tabia za mumewe lakini alikubali wafikie suluhu kwani hakuwa tayari kuivunja ndoa yake iliyodumu miaka 20. Hivyo mnamo Julai 21, 1995. Tucker na mkewe Carol waliondoka wakiwa na gari lao wakielekea Icklingham, ili kwenda kupata chakula cha usiku, na wakati wakirejea nyumbani ndipo walipopata ajali. Kwa mujibu wa vipimo vilivyochukuliwa kutoka kwenye eneo la ajali, vilionesha kwamba, mwendo wa gari la Tucker kabla ya kupata ajali ulikuwa ni kilometa 18 kwa saa, mwendo ambao ulielezwa na wataalamu hao kuwa ni vigumu gari kupoteza mwelekeo hata kama linakwepa kitu.


  Mnamo Agosti 18, 1995, Tucker alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mkewe. Saa kadhaa baada ya kukamatwa, Tucker alikimbizwa Hospitalini kwa matibabu ya msongeko aliyoyapata ghafla baada ya kukamatwa. Hata hivyo baada ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la kumuua mkewe, Tucker aliachiwa kwa dhamana. Kwa kipindi cha siku chache tangu kuachiwa Tucker aliwasiliana na mshauri wa kitengo cha uhamiaji nchini Uingereza ili kupata taarifa zitakazomwezesha Dijana kuingia Uingereza kama mkimbizi wa kisiasa. Baada ya hapo alikwenda kwenye kampuni moja ya wakala wa ukatishaji ticket za ndege ambapo kwa kutumia jina la mtu mweingine alimkatia Dijana tiketi ya ndege itakayo muwezesha kusafiri kutoka mji wa Belgrade nchini Yugoslavia hadi Zurchi nchini Uswizi, ambapo angefikia kwa mmoja wa rafiki zake Tucker na kuishi kwa muda kabla ya kuhamia nchini Uingereza na kuungana na Tucker.

  Mnamo November 17, 1997 ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu Tucker kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana, kesi yake ilianza kusikilizwa katika mahakama ya Norwich Crown ambapo Tucker alikanusha kuhusika kwa namna yoyote kumuua mkewe.
  Muendesha mashtaka, David Stokes aliiambia mahakama kwamba, Tucker aliingiza gari lake kwa makusudi mtoni, kisha akamkaba mkewe na kumzamisha kwenye maji iliionekane kama alikufa kutokana na ajali. Alisema lengo la Tucker kupanga na kuteleza mauaji ya mkewe ni kutokana na yeye Tucker kuzama kwenye penzi haramu la binti wa Ki-Bbsnia. Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kubainisha kwamba, mwezi mmoja kabla ya kumuua mke wake Tucker alimuombea Dijana visa ya kuingia nchini Uingereza akiwa kama mgeni wake na bila ya hata mkewe na familia yake kufahamu, Tucker alikaa na Dijana kwa wiki moja wakitumia katika klabu ya jeshi la Anga iliyopo katika jiji la London.

  Na hata aliporejea nchini Uingereza baada ya kumaliza mkataba wake nchini Bosnia, Tucker alimfanyia mpango Dijana wa kuishi Zurich nchini Switzerland na katika kipindi hicho, alikuwa akimpigia simu kila siku, ikiwamo hata siku ambayo mkewe alifariki.
  Mashaidi wengine walioitwa walikuwa ni wataalamu wa usalama wa barabarani walio chunguza ile ajali ambao walithibitisha mahakama kwamba ajali ile ilikuwa ya kupangwa ili kuficha mauaji ya mkewe. Naye mtoto wake mwenyewe wa kumzaa aliyejulikana kwa jina la Vanessa, akitoa ushahidi wake alieleza mahakama jinsi ndoa ya wazazi wake ilivyoingia kwenye majaribu makubwa mara baada ya baba yao kwenda nchini Bosnia.Hata hivyo upande wa mashtaka ulishindwa kumuita Dijana Dudukovic mahakamani ili kutoa ushahidi wake kwa kuwa wakati huo alikuwa amekwisha kuolewa na mwanaume mwingine raia wa Switzerland na alikuwa akiishi nchini humo.

  Dijana alikataa katakata kwenda nchini Uingereza kutoa ushahidi wake, lakini katika maelezo aliyo yatoa kupitia vyombo vya habari , Dijana alisema, ‘najuta kwanini nilikutana na mtu huyu ( Tucker) maisha yangu yameathiriwa sana, sikuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tucker na wala sikuwahi kumshauri amuuwe mkewe kwa ajili yangu, nilikuja kufahamu kuhusu kifo cha mkewe baada ya yeye Tucker kunipigia simu.'
  Katika utetezi wake Tucker alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dijana, na alikiri kumualika Dijana nchini Uingereza kutokana na mke wake kumkatalia kutoka naye kwa matembezi ya mwisho wa Juma.

  Kwa maneno yake mwenyewe Tucker aliieleza mahakama ‘niliwahi kufanya mapenzi na Dijana mara mbili tu na hatukuwahi kuwa na mazungumzo ya kuwa na uhusiano wa kudumu kati yetu' Hata hivyo upo utata uliojitokeza mahakamani kuhusiana na ripoti iliyowasilishwa na wataalamu walioufanyia uchunguzi mwili wa Carol. Katika ripoti hiyo Dk. Cary na Dk. Harrison walikiri kutokuwepo alama au mikwaruzo kwenye shingo ya Carol inayoonesha kwamba alinyongwa au kuzamishwa kwa makusudi. Kutokana na maelezo ya wataalamu hao wawili waliotoa mahakamani, ilidhihirisha kwamba kulikuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa Tucker alimuua mkewe kwa kumnyonga na kumzamisha majini mara baada ya ajali.

  Utata mwingine ulijitokeza na ushahidi uliotolewa na mvuvi aliyekuwa jirani na eneo la tukio. Katika ushahidi wake, mvuvi huyo alikiri kutosikia kishindo cha mtu kutapatapa katika maji kama vile anazamishwa. Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo kwenye eneo la ajali, inasemekana kwamba ajali ilitokea majira ya saa 4.30 usiku, umbali mfupi tu kutoka kwenye mgahawa husika. Hata ivyo Ankara (bill) ya malipo ya chakula ilionesha kwamba ilifungwa mahesabu saa tatu na dakika ishirini za usiku, wakati Tucker alikiri kwamba alikaa kwenye mgahawa hadi saa 4 za usiku kabla ya kuondoka na kupata ajali. Utata mwingine ukajitokeza kwamba ilikuaje watu wafike kwenye mgahawa, tena kwa lengo kupata mlo wa usiku na kumaliza tofauti zao , lakini watumie saa moja tu kupata milo yote mitatu pamoja na kahawa?Je kuna uwezekano kwamba watumishi wa ule mgahawa walifunga hesabu ya Ankara yake muda mrefu kabla ya Tucker na mkewe hawajamaliza kula? Huu nao ukawa ni utata mwingine.

  Lakini hata hivyo ilikuja kujulikana kwamba yupo mtu aliye walipia Ankara yao kwenye muda wa saa nne na dakika kumi na moja muda ambao inasemekana Alishaondoka kwenye mgahawa huo. Swali lingine lililo jitokeza ni, je, kuna uwezekano wa Tucker kumuuwa mkewe Carol kabla ya kufika kwenye eneo la ajali hivyo kutengeneza ile ajali ili kuficha ukweli wa kifo cha mkewe? Lakini kama Tucker na mkewe waliondoka kwenye mgahawa majira ya saa nne na dakika kumi na moja usiku, je muda huo ungetosha, Tucker kumuuwa mkewe kwa kumnyonga shingoni bila ya kuacha alama zozote shingoni na kasha kuendesha gari hadi kwenye daraja na kusababisha ajali kwa makusudi ili kuficha mauaji hayo?
  Ukweli ni kwamba kesi hii iliibua maswali mengi sana ambayo yalileta ubishi wa kisheria pale mahakamani. Hata hivyo mnamo Disemba 5, 1997 baada ya wikimbili za kuendesha kesi hiyo, Jopo la majaji wa mahakama hiyo walifikia uamuzi wa kumtia Nicolas Tucker Hatiani kwa kosa la kumuua mkewe Carol Tucker kwa makusudi.

  Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa saba, Muheshimiwa Jaji Elizabeth Cage alimhukumu Nicolas Tucker kifungo cha maisha.
  Hata hivyo, Turker alifanya majaribio kadhaa ya kukata rufaa bila mafanikio, lakini mnamo mwaka 2008, Nicholas Turker aliachiwa huru na sasa anaishi na mchumba wake Jenny Peackock katika mji wa Thetford. Na tangu aachiwe amekuwa akifanya juhudi kubwa ili kusafisha jina lake.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Naomba nianze kuprint hizi vitu.
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii ni kwa ajili ya kufungia mwaka, ni vyema ukaisoma ukiwa nyumbani huku ukipata Juis Briid, Khahawa au Chai
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Storry nzuri sana, hapo ndo inaonyesha vipi wanaume hawatumii akili wakisha owa.

  Aaa yule mwimbaji hajakosea aliyeimba ile nyimbo ya Tamaaa mbayaa....Big up @ 20%.
   
 5. a

  ammah JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  very interesting....
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kuna mengi ya kujifunza kwa kweli........
   
 7. M

  Myn17 Senior Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii imetulia,thanks
   
 8. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It s very interesting, but hy kesi ilikuwa ngumu sana kuifanyia maamuzi..., Nimejaribu kuisoma tena na tena bado sijaona mazingira ya kuwa Turker alimuua mkewe
   
 9. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nimekumbuka kisa cha yule Mhindi na ajali za kutengeneza enzi za Nyerere.
  Storry nzuri, interesting.
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nimekumbuka kisa cha yule Mhindi na ajali za kutengeneza enzi za Nyerere. Ingawa siyo penzi Mbosnia ndilo chanzo, chanzo ni migogoro ya ndani ndo ilizaa penzi la Mbosnia.
  Storry nzuri, interesting.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  I love crime investigation and watch them all the time.
  Sasa dingi, inakuwaje wanashindwa kuthibitisha means ya kifo cha mwanamke? Manake kwa postmortem kama mtu kanyongwa ingebidi mishipa ionekane kukatwa na struggling kwenye shingo. Kama alikufa kwa maji mapafu yangejaa maji.
  The guy had a motive to kill ( angepata money from insurance, na pia anagepoteza hela kwenye divorce). Evidence inapoint kwake na ingekuwa conclusive kwa kuangalia postmortem na barabara.
   
 12. paty

  paty JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,256
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  duh , kweli soo ,:A S embarassed:
   
 13. huzayma

  huzayma Senior Member

  #13
  Jan 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmoja ajitolee kunisamaraizia tafadhali duh! imenishinda ndefu.:eyebrows::eyebrows:
   
 14. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Narudi baadae mara baada ya kuisoma tena hii kesi na kuangalaia sheria za kiingereza zinasemaje kwa tatizo kama hili
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Tamaa mbaya .
   
 16. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Mi nitaisoma kesho kwa umakini kwa kuwa hapa niko resi mbaya...labda waniprintie
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu, mimi ni mgonjwa sana crime investigation, nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa mingi sana ya kesi kama hizi ambazo zimejaa utata. hiyo huwa inanipa changamoto ya kuchemsha bongo. nimeona nishirikiane na wana JF wenzangu ili tutafakari nakujifunza kwa pamoja...... wenzetu wako more advanced katika mambo ya kiuchunguzi, lakini kuna wakati unaweza kuona makosa ya kiuchunguzi ambayo yanazua maswali mengi kuliko majibu.

  Nitaendelea kuwawekea visa hivi kwa kadiri muda utakavyoniruhusu
   
 18. d

  dashy Member

  #18
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  heeee kwakweli imenshnda kusoma eeeeh maneno meeeeeng khaaaa
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,090
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi hongera sana kwa story nzuri,
  je ni ya ukweli au umetunga tu,
  kweli unatisha kama nini, hongera sana,

  Mimi ambapo sikuupenda ni hapa tu

  "Hata hivyo baada ya kuzaa, Carol alianza kunenepa ghafla na kuwa na mwili wa tipwa tipwa kiasi cha kufikia uzito wa kilo 95. Hapo ndipo ladha ya upendo wa awali ilipotea na tendo la ndoa kuwa la baridi"

  Hapa ni kama umetuchana sana sisi wanawake mkuu.
   
Loading...