Akiwa mwanaume mwelewa atazidisha bidii kutafuta sources nyengine za pesa ... mwanaume hasa ... rijali kabisa hawezi kupokea hela ya mwanamke ..... mwanamke kumpa hela yake ya mshahara .. mhh! sidhani kama ni kuwa thabit ama kumpa uhalisi wake ... mwengine ni mharibifu ... na hela usioifanyia kazi waweza kuzitumia utakavyo maana hujui uchungu wake ... mimi nadhani mugawane majukumu halafu umsaidie tu pale ambapo anaupungufu ... heshima ibaki palepale
lakini je? kiukweli unaamini/unadhani kumpa mshahara wako ili 'kusawazisha' mambo ndio suluhisho la kudumu?
Vipi inapokuja suala la kusaidia ndugu upande wa mume, ndugu upande wako (mke), na maamuzi kwa ujumla ndani ya nyumba yenu kuhusiana na matumizi ya fedha?.
kwa muda gani utaachia hali hii iendelee? ?
...nitaendelea as long as kipato chake hakitoshelezi mahitaji. Baada ya hapo sijajua itakuwaje
hapa point ni kwamba kwa sisi nimeprove kwamba :
1. Sio practical kwamba eti yeye awe kiongozi wa masuala ya fedha ambayo haipo mikoni mwake
2. Mimi kuchukua uongozi kifedha kwa sababu kipato chake ni kidogo kunampa insecurity, hali ambayo inaleta mushkeli na haimsaidii yeye wala mimi kama tuition ya Haika inavyoeleza hapo juu
Kwa jamii nyingi hasa za kiafrika, hata nyumbani Tanzania, bado inaonekana ni jukumu lako mume kutimiza kama si yote, basi kwa asilimia kubwa mahitaji ya mkeo na watoto, pamoja na nyumba kwa ujumla.
Wakati huo huo, wanawake wengi sasa sehemu mbali mbali duniani ikiwamo Tanzania, baadhi mmekuwa na uwezo mkubwa tu kifedha kuliko waume zenu.
mfano; Mke unakuwa na cheo kikubwa kuliko mumeo, mke unakuwa na mshahara mkubwa kuliko mume, au mke unakuwa na uwezo mkubwa kimaisha kuliko mumeo!
Huenda hili linatokana na haki sawa mnazozipata kwenye elimu, kazi, madaraka na hata wale mnaomudu kufanya biashara kubwa...
Je, mabadiliko haya yanaathari zipi katika ndoa, ...na je? njia zipi zinafaa kuepusha migogoro, ili mume nawe 'ujisikie/ajiskie ni mwanaume' nyumbani kwenu?
Ngoja na mimi nitoe yangu machache.....
Katika Dunia ya leo, Bi'mkubwa kuwa na kipato zaidi ya Bw'mkubwa ni kawaida kabisa. Hii ishu wala sio ya kuchanganyikiwa/kushangaa tena.
Sasa basi, migogoro mingi (ambayo pengine usababisha kwa sitwesheni mzima kuonekana kana kwamba tofauti ya kipato inamfanya Bw'mkubwa kuwa mdogo) uanzia pale matumizi ya Bw'mkubwa yasiyoeleweka yanapogundulika.
Kutokana na nyendo za Bw'mkubwa (hasa wa kibongo), utaona kwamba wana matumizi mengi ambayo ni ya kibinafsi (ulevi) au yenye kunufaisha watu wengine nje ya familia yake (vimada na marafiki). Matumizi haya huwa yapo, haijalishi nani ana kipato kikubwa.
Tofauti ni kwamba, kwenye familia ambayo Bw'mkubwa ndio mwenye kipato cha juu, Bi'mkubwa huwa ana kosa haki (ingawaje anatakiwa awe nayo) ya kuuliza kuhusu matumizi hayo.
Sasa kwenye familia ambayo mtiririko wa kipato uko tofauti na wa kiutamaduni, utakuta Bi'mkubwa anajikuta ana nguvu za haki za kuuliza kuhusu matumizi yote ya kifamilia na ya kibinafsi.
Na pindi Bw'mkubwa akishindwa kutoa maelezo yanayoeleweka, hapo ndipo cheche za migogoro zinapoanza.
Hatimaye, Bw'mkubwa kujiona kuwa ana onewa/nyanyaswa kwa sababu kipato chake kidogo.
Mwanaume kuwa rijali 100% ni ngumu kama ilivyo mwanamke kuwa mtii 100%
tukubali kukosa kidogo kila upande.
manake hapa mimi napata picha ya mwanaume rijali kiafrika ni yule ambaye maamuzi yote ya nyumbani anafanya yeye. mimi kama mwanamke sitamuweza.
Kwa ajira za sasa, kupanda na kushuka kwa kipato si kitu cha muda mrefu sana.
sisi tumeshawahi kusimamia nyumba kwa zamu mara kibao, ila tofauti ni kuwa yeye akiwa nazo anatoa kiasi fulani anaweka mahali/account naweza kuchuka bila kuombaomba kila saa, na mimi pia hivyo hivyo, ila uwazi katika jumla kuu ni muhimu.
Pia kwamba balance uliobaki nayo ni kwaajili ya personal use tu.
inahitaji kujitoa zaidi na TOTAL TRUST IN EACH OTHER. Ambayo nadhani kwa muelekeo wa hapa ni ndogo.
tution ya bure kwa kina dada (ambao bado bado) ukiua self confidence ya mumeo utamchukia mara moja. Jitahidi aweze kutembea kifua mbele humu duniani, hasa kwa rafiki zake na ndugu.
...ni kutokana na jinsi tunavyopangilia mipango yetu kwa kuzingatia priorities tulizojiwekea. Mfumo wetu huu umewakwaza familia zetu kwa pande zote mbili kwani wanashindwa kexercise authorities ambazo hawana lakini wanataka kujitwalia. Imechukua muda kuikubali hali hiyo, lakini sisi wawili tuko vizuri kabisa. All our money is owned jointly. All our properties owned jointly na our next of kin ni watoto wetu ambao wote ni wa kike, jambo ambalo baadhi ya wana ndugu hawalielewi kabisa.
...
...
4. Hili wala halihitaji kulisema: Ndo nyingi hasa kwa wenzetu 'walioendelea' zinavunjika kwa sababu ya mambo haya haya ya kubishana 'nani mkubwa' na 'nani mdogo'...taasisi nzima ya ndo imedhalilishwa kiasi kuwa sasa thamani yake haionekani tena..ukiangalia chanzo chake ni mambo haya haya!
Yani wakati wa uchumba, umfahamishe unachukuliaje fedha, majukumu ya kifedha, na mambo yote unayodhani ni muhimu kwako na mtazamo wako kifedha. Mtazame reaction yake ya maneno au matendo, bora kinga kuliko tiba -Haika
Off the track
Romance Without Finance Is Nuisance
Katika mahusiano especially madada na makaka wa kizazi cha dot.com, swala la finance na career linatuchukulia mda sana.
Its tough to balance the two especially kama kila mtu ana kazi yake ataogopa kuiacha na kumfuata mwenzake. Na maana siyo gurantee kwamba mtakuwa kituo kimoja cha kazi. Nimeshaona washkaji mpaka wanahonga kutafuta uhamisho wa wenzi wao, ikishindikana ndo hivyo..yanakuwa mapenzi ya mbali..na wote humu tunajua madhara yake..hawakawii wengine kukusaidia kutoa huduma on either side(kwa mwanamke na mwanaume)!....
Kikubwa ni Trust, but how?
KAzi ipo wandugu!