Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,850
Kwa jamii nyingi hasa za kiafrika, hata nyumbani Tanzania, bado inaonekana ni jukumu lako mume kutimiza kama si yote, basi kwa asilimia kubwa mahitaji ya mkeo na watoto, pamoja na nyumba kwa ujumla.
Wakati huo huo, wanawake wengi sasa sehemu mbali mbali duniani ikiwamo Tanzania, baadhi mmekuwa na uwezo mkubwa tu kifedha kuliko waume zenu.
mfano; Mke unakuwa na cheo kikubwa kuliko mumeo, mke unakuwa na mshahara mkubwa kuliko mume, au mke unakuwa na uwezo mkubwa kimaisha kuliko mumeo!
Huenda hili linatokana na haki sawa mnazozipata kwenye elimu, kazi, madaraka na hata wale mnaomudu kufanya biashara kubwa...
Je, mabadiliko haya yanaathari zipi katika ndoa, ...na je? njia zipi zinafaa kuepusha migogoro, ili mume nawe 'ujisikie/ajiskie ni mwanaume' nyumbani kwenu?