Hii habari inasikitisha sana. Ningependa Baba Askofu mkuu Pengo aweke hii habari vizuri. Mtumishi wa Mungu akituhumiwa inatisha sana tena tuhuhuma zenyewe zikiwa ni mbaya kama hizi za biashara za madawa ya kulevya.
Akiwa na kazi ya kueneze neno la Mungu, kusema ukweli, na kutetea ukweli hata ikimpasa kufa kama Yesu Kristu, Pengo alipaswa kusema kusema ni nani wanaotumhumu, walimtuhumu wapi, na kwa nini wamtuhumu. Kwanini atajwe yeye, ni mazingira gani yanafanya mpaka atajwe. Je ni kweli wanataka kumyamazisha na kwa nini wamnyamazishe?? Tuhuma za madawa ya kulevya ni nzito anatakiwa kutoa ufafanunuzi.
Tuhuma hizi zinachanganya sana wanakondoo wa Kanisa katoliki.
Baba Askofu weka mambo wazi ili waumini wajue ukweli, ili upande unaotoa tuhuma nao uje kuthibitisha au kukanusha.
Mpaka 2015 Tanzania hakuna kanisa wala msikiti itakuwa uwanja wa vita kati ya wanasiasa wanaotaka madaraka na yeyote anawazuia. Ila makanisa yanatisha yanashiriki na wahuni, wezi, watuhumiwa, majambazi, wahujumu na wala Rushwa. Makanisa na misikiti yanatumia makundi ya watuhumiwa kuchangisha fedha za kazi za Mungu. Kwenye watuhumiwa hawa kwa sababu wana fedha wapo wala rushwa, wauza unga, matapeli nk. Ukishiriki na mwizi na wewe ni mwizi, ukishiriki na mla rushwa na wewe ni mla rushwa, ukishiriki na mbakaji na wewe umebaka.