Shishye
JF-Expert Member
- Feb 26, 2009
- 269
- 1
Huku tunakokwenda hakufai. Nitatoa mfano.
Mie kama mtoto wa kiislam sitakiwi kula nguruwe, dini inasema ni haramu. Kuacha kwangu kula nguruwe sio kwa sababu niko allergic nayo, au ninaumwa. The decision is completely based on on faith kwamba nikila kiti moto ninapata dhambi. I stopped reasoning about manufaa ya kiti moto like bei yake rahisi kuliko mbuzi, au ng'ombe, pia kiti moto kina protein za kutosha. Hizo zote faida za kiti moto sizifikirii kwa sababu naogopa Jehanamu. Essentially my faith has hijacked my own reasoning power.
My point is, hawa viongozi wa dini wakianza kuongelea siasa--they are subliminally imposing faith mandate for their waumini to follow what they are preaching, in this time sio Yohana mtakatifu tena bali ni siasa. Wakatoliki are soon going to give up their reasoning power and vote for whoever Kardinali Pengo is endorsing between those lines. Not because they want to, but because Pengo said that is what GOD and Jesus wants to. That is what Waraka is intentionally supposed to be interpreted na waumini.
It is a very dangerous trajectory for our country because once the debate is shifted to udini, the risks for conflict will increase and we are already masikini--the last thing we want is people to be voting in 2010 because of dini au ukabila. Unfortunately when shit hit the fan kardinali Pengo anakwenda zake Vatican kutulia na kutuachia msala nchini kwetu.
Ya Kaisari muachie Kaisari Kardinali Pengo, huko unakotupeleka hatutaki.
Mfano wa kiti moto sio relevant. Waraka wa kanisa hauko dini-specific. Kama utakuwa umeusoma utaona unazungumzia kuwa na viongozi waadilifu. Shida yetu ni kuwa tunapenda sana kurukia mambo juu juu na kufanya conclusions based on who said what! Nani zaidi ya fisadi asiyekubaliana na ukweli kwamba nchi yetu imekosa uongozi adilifu? Hakuna popote katika waraka panapoelezea dini ya mtu mwadilifu. Kinachozungumziwa hapa ni wasifu wake.
Kama waraka, mwongoze, or any other document itakuwa ina-influence wananchi kumchagua kiongozi wa dini au dhehebu fulani, jua kwamba document hiyo na wanayoieneza ni wapotoshaji. Lakini kama inatuelimisha kuhusu sifa za watu safi wa kutuongoza jinsi ya kutawala raslimali zetu ili zitufae kwa usawa, hiyo document imechelewa sana kutufikia. Mimi siwezi kusema eti huu usanii ulioko kwenye utawala wa sasa unasababishwa na dini? Hata kidogo. Ni uongozi mbovu tu. Kama ndivyo tunahitaji nini basi? Dini bora zaidi? Hata kidogo! Tunahitaji viongozi wasafi, imara, shupavu wa kutawala na kuongoza kwa dira.
Hata kabla ya Pengo kusema tulishajua kuwa nchi imeoza. Itakuwa ni kujifanya vipofu kufanya ufisadi wetu mitaani huko halafu jumapili/ijumaa tunavaa suti/kanzu zetu na kujifanya tuko kanisani eti tunaabudu. Kidini tunaamini wenzetu tunaoishi nao ndio sura na mfano wa Mungu, kumbe ufisadi tunaowafanyia wenzetu tunamfanyia Mungu halafu tunajifanya tunampenda, si ndio unafiki huo? Sasa Pengo akilikemea hilo kuna ubaya gani?Maisha yetu ni pamoja na shughuli za siasa. Dini inaongoza maisha yetu yote. Hivyo siasa ni subset tu ya dini ingawaje iko huru kujiendesha yenyewe. Infact, uadilifu, upendo, kupenda usawa, huruma, na yote mazuri hutoka kwa roho wa Mungu. Kiongozi mwenye sifa hizo lazima awe mwumini wa dini fulani. Kama hana dini, ni wachache sana utakuta wenye ubinadamu.
Nchi imeoza, someni waraka na muufanyie kazi kwa manufaa ya nchi. Acheni ubinafsi, watu wanateseka na umaskini, wanakufa kwa kukosa huduma muhimu kwa sababu ya wachache kujilimbikizia utajiri - ndio ufisadi huo.
Hivi mbona hamkupinga wakati viongozi wa dini walipomfagilia Kikwete alipochaguliwa kuwa ni chaguo la Mungu? Chaguo la Mungu limebadilika baada ya mtumishi kushindwa kuwatumikia watu wake sasa hamtaki tena kuupokea ufunuo huo, kulikoni??