kubenea mwaga nondo zako humu jf tutazipeleka mitaani...
Hiyo ni kweli kabisaaaaaaaa.Sasa hivi hakuna tofauti kati ya vijiwe vya kahawa na vyombo vya habari vilivyobakia maana vyote vinatoa taarifa za habari[ambazo zimekwishaenea] na si habari ambazo hatuzifahamu.Wanaharakati,wanasiasa na wananchi wote ambao tunaamini kupata habari ni haki yetu ya msingi hatuna budi kuungana kulipigania MWANAHALISI.
Salaam wana Jf
kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na kutokuwa na gazeti mbadala ni pengo kubwa imefahamika.
Tanzania tunayo magazeti mengi ya siasa lakini mengi ya hayo magazeti yana nidham ya uoga.katika tukio la mauaji ya mwandishi RIP Daud mwangosi,pamoja na ushahidi wa picha uliopo magazeti yetu yaliyobaki hakuna hata moja lenye uthubutu wa kufanya uchunguzi na kuanika majina ya wale askari waliokuwa wakimpiga mwangosi.
Kuna habari zimeenea kwamba mwangosi alipigwa kwanza risasi akafa,akalipuliwa na bomu kuficha ushahidi wa risasi.magazeti yetu yameshindwa hata kuwahoji watu waliokuwa wanachungulia madirishani na kutupa habari za uhakika hapo ndipo naposema pengo la MWANAHALISI halizibiki.
Natoa wito kwa wanahabari,wanaharakati kufanya jambo fulani kuishinikiza serikali ilifungulie gazeti hilo kwani tunachopata sasa ni taarifa tu na sio habari za kiuchunguzi,vile vile na nyie wamiliki wa vyombo vya habari boresheni MAGAZETI yenu mtupe habari zinazokamilika,
mwisho WANAHARAKATI mlitoa siku saba kwa serikali kulifungulia MWANAHALISI je mmeishia wapi tupeni majibu mmetuacha njia panda,na wewe SAED KUBENEA mbona uko kimya sana au umeridhishwa na ukandamizaji huo?
Karibuni tujadili.
Jamani wana Jamvi kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kumesababisha wananchi tulio wengi tukose habari za ukweli na zilizofanyiwa utafiti wa kutosha, mfano kuanzia gazeti hili limefungiwa kuna matukio mengi yametokea na kutokana na kukosekana kwa chombo cha habari chenye uthubutu kama mwanahalisi wa kuandika habari kwa kina bila uoga kumetukosesha haki ya msingi sana
Tukumbuke kuwa karibia matukio yote mabaya na mazuri gazeti hili lilijitahidi sana kuweka mambo yote wazi. MFANO habari ya kutekwa na kuteswa kwa Dr ULIMBOKA ni gazeti hili lililojitahidi kuandika habari ile kwa uwazi na tukio hilo ndilo lilishindilia gazeti hilo kufungiwa kwa muda usiojulikana.
Wito wangu kwa serekali hii ya JK walifungulie gazeti hili ili kila kitu kiwekwe wazi,,,, mambo ya kuficha kwa dunia ya sasa hayapo tena na kila kitu kitajulikana tu.
Habari hizi ni miongoni mwa zilizoandikwa na gazeti hili kwa waliokuwa wasomaji wa makala za MWANAHALISI.................................................................................................................