Pengo la Mwanahalisi laonekana matukio ya mauaji.

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,084
Salaam wana Jf

kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na kutokuwa na gazeti mbadala ni pengo kubwa imefahamika.

Tanzania tunayo magazeti mengi ya siasa lakini mengi ya hayo magazeti yana nidham ya uoga.katika tukio la mauaji ya mwandishi RIP Daud mwangosi,pamoja na ushahidi wa picha uliopo magazeti yetu yaliyobaki hakuna hata moja lenye uthubutu wa kufanya uchunguzi na kuanika majina ya wale askari waliokuwa wakimpiga mwangosi.

Kuna habari zimeenea kwamba mwangosi alipigwa kwanza risasi akafa,akalipuliwa na bomu kuficha ushahidi wa risasi.magazeti yetu yameshindwa hata kuwahoji watu waliokuwa wanachungulia madirishani na kutupa habari za uhakika hapo ndipo naposema pengo la MWANAHALISI halizibiki.

Natoa wito kwa wanahabari,wanaharakati kufanya jambo fulani kuishinikiza serikali ilifungulie gazeti hilo kwani tunachopata sasa ni taarifa tu na sio habari za kiuchunguzi,vile vile na nyie wamiliki wa vyombo vya habari boresheni MAGAZETI yenu mtupe habari zinazokamilika,

mwisho WANAHARAKATI mlitoa siku saba kwa serikali kulifungulia MWANAHALISI je mmeishia wapi tupeni majibu mmetuacha njia panda,na wewe SAED KUBENEA mbona uko kimya sana au umeridhishwa na ukandamizaji huo?

Karibuni tujadili.
 
Kubenea asajili gazeti lingine,tutamuunga mkono,Mwanahalisi lingekuwepo lingewataja wauaji wa kamanda Daudi Mwangosi.
 
Tujiulize sote kwamba MWANAHALISI liliondolewa sokoni ili kufanyike kitu gani hapa katikati???

Hadi si ya leo watu tungekua hadi na minutes za vikao vilivyopanga Dr Slaa auawe huku wengine wakiwa nje ya nchi ili wanapotua tu uwanja wa ndege nao waanze na MACHOZI YA MAMBA huku wakijua kuwa lengo la lile kundi mojawapo la MAFISADI papa na chipukizi watakua wanasheherekea.

Kamwe Mabadiliko muda wake ukifika huwezi kuyazuia hata kwa ndege aina ya B52 ya Wamarekani achilia mbali hizo silaha zilizotoka Iran zilizozagaa mikononi mwao GREENGUARDS hadi hivi sasa bila usajili.

Gazeti la MwanaHalisi hakika Umma wa Tanzania tunakumisi kwa namna ambayo haina kifani!!!
 
Mwanahalisi lingetujulisha hata nini kilikuwa nyuma ya pazia, wengi wengekuwa wameshaumbuka sana
 
Kukosekana kwa gazeti la MWANAHALISI hivi sasa kunajionyesha sana sawa na kukosekana kwa namba 9 katika timu.
 
Nahisi ni mkakati mahususi wa serikali kulipoteza kabisa gazeti hilo ili waweze kutenda uovu kwa watanzania.
 
saed hawezi kuweka habari hapa anatumia pesa na muda kutafuta habari return inahitajika

woote tunaopenda haki tuandamane kushinikiza hili

tukiishia kulalamika haina maana hata kidogo

hawajalifungia gazeti la mwanahalisi wamemfungia Kubenea coz kabla ya kuja kwa Kubenea gazeti kidogo lilidorora na wakati habari ya Dr.Ulimboka ilikuwa hot cake

ila alivyorudi tu makala zake mbili za.front page wakaamua kumfungia

naamini wameshindwa kumuua thus way hili limetokea
 
Hiyo ni kweli kabisaaaaaaaa.Sasa hivi hakuna tofauti kati ya vijiwe vya kahawa na vyombo vya habari vilivyobakia maana vyote vinatoa taarifa za habari[ambazo zimekwishaenea] na si habari ambazo hatuzifahamu.Wanaharakati,wanasiasa na wananchi wote ambao tunaamini kupata habari ni haki yetu ya msingi hatuna budi kuungana kulipigania MWANAHALISI.
 
kweli mkuu inakera sana habari umeiona kwenye Tv then unaikuta kwenye gazeti asubuhi inakuwa kama kukopi na kupest kweli tupiganie mwanahalisi lifunguliwe.
 
Mwanahalisi angekuwepo angetuhabarisha matukio ya mauaji ya David Mwangosi kuanzia kabla, baada na majina ya waliohusika na njama hizo tungeyapata!!
Salaam wana Jf

kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na kutokuwa na gazeti mbadala ni pengo kubwa imefahamika.

Tanzania tunayo magazeti mengi ya siasa lakini mengi ya hayo magazeti yana nidham ya uoga.katika tukio la mauaji ya mwandishi RIP Daud mwangosi,pamoja na ushahidi wa picha uliopo magazeti yetu yaliyobaki hakuna hata moja lenye uthubutu wa kufanya uchunguzi na kuanika majina ya wale askari waliokuwa wakimpiga mwangosi.

Kuna habari zimeenea kwamba mwangosi alipigwa kwanza risasi akafa,akalipuliwa na bomu kuficha ushahidi wa risasi.magazeti yetu yameshindwa hata kuwahoji watu waliokuwa wanachungulia madirishani na kutupa habari za uhakika hapo ndipo naposema pengo la MWANAHALISI halizibiki.

Natoa wito kwa wanahabari,wanaharakati kufanya jambo fulani kuishinikiza serikali ilifungulie gazeti hilo kwani tunachopata sasa ni taarifa tu na sio habari za kiuchunguzi,vile vile na nyie wamiliki wa vyombo vya habari boresheni MAGAZETI yenu mtupe habari zinazokamilika,

mwisho WANAHARAKATI mlitoa siku saba kwa serikali kulifungulia MWANAHALISI je mmeishia wapi tupeni majibu mmetuacha njia panda,na wewe SAED KUBENEA mbona uko kimya sana au umeridhishwa na ukandamizaji huo?

Karibuni tujadili.
 
Jamani wana Jamvi kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kumesababisha wananchi tulio wengi tukose habari za ukweli na zilizofanyiwa utafiti wa kutosha, mfano kuanzia gazeti hili limefungiwa kuna matukio mengi yametokea na kutokana na kukosekana kwa chombo cha habari chenye uthubutu kama mwanahalisi wa kuandika habari kwa kina bila uoga kumetukosesha haki ya msingi sana

Tukumbuke kuwa karibia matukio yote mabaya na mazuri gazeti hili lilijitahidi sana kuweka mambo yote wazi. MFANO habari ya kutekwa na kuteswa kwa Dr ULIMBOKA ni gazeti hili lililojitahidi kuandika habari ile kwa uwazi na tukio hilo ndilo lilishindilia gazeti hilo kufungiwa kwa muda usiojulikana.

Wito wangu kwa serekali hii ya JK walifungulie gazeti hili ili kila kitu kiwekwe wazi,,,, mambo ya kuficha kwa dunia ya sasa hayapo tena na kila kitu kitajulikana tu.

Habari hizi ni miongoni mwa zilizoandikwa na gazeti hili kwa waliokuwa wasomaji wa makala za MWANAHALISI.................................................................................................................
 
Attachments

  • 11.jpg
    11.jpg
    262.2 KB · Views: 29
  • 13.jpg
    13.jpg
    269.2 KB · Views: 26
  • 17.jpg
    17.jpg
    254.3 KB · Views: 22
  • 14.jpg
    14.jpg
    248.7 KB · Views: 24
  • 21.jpg
    21.jpg
    258.1 KB · Views: 20
  • Tisa.jpg
    Tisa.jpg
    265.2 KB · Views: 24
  • Tatu.jpg
    Tatu.jpg
    268.3 KB · Views: 23
  • Nane.jpg
    Nane.jpg
    237.4 KB · Views: 22
  • Mbili.jpg
    Mbili.jpg
    267.8 KB · Views: 23
  • 25.jpg
    25.jpg
    259.8 KB · Views: 22
Jamani wana Jamvi kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kumesababisha wananchi tulio wengi tukose habari za ukweli na zilizofanyiwa utafiti wa kutosha, mfano kuanzia gazeti hili limefungiwa kuna matukio mengi yametokea na kutokana na kukosekana kwa chombo cha habari chenye uthubutu kama mwanahalisi wa kuandika habari kwa kina bila uoga kumetukosesha haki ya msingi sana

Tukumbuke kuwa karibia matukio yote mabaya na mazuri gazeti hili lilijitahidi sana kuweka mambo yote wazi. MFANO habari ya kutekwa na kuteswa kwa Dr ULIMBOKA ni gazeti hili lililojitahidi kuandika habari ile kwa uwazi na tukio hilo ndilo lilishindilia gazeti hilo kufungiwa kwa muda usiojulikana.

Wito wangu kwa serekali hii ya JK walifungulie gazeti hili ili kila kitu kiwekwe wazi,,,, mambo ya kuficha kwa dunia ya sasa hayapo tena na kila kitu kitajulikana tu.

Habari hizi ni miongoni mwa zilizoandikwa na gazeti hili kwa waliokuwa wasomaji wa makala za MWANAHALISI.................................................................................................................
 
Jamani wana Jamvi kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kumesababisha wananchi tulio wengi tukose habari za ukweli na zilizofanyiwa utafiti wa kutosha, mfano kuanzia gazeti hili limefungiwa kuna matukio mengi yametokea na kutokana na kukosekana kwa chombo cha habari chenye uthubutu kama mwanahalisi wa kuandika habari kwa kina bila uoga kumetukosesha haki ya msingi sana

Tukumbuke kuwa karibia matukio yote mabaya na mazuri gazeti hili lilijitahidi sana kuweka mambo yote wazi. MFANO habari ya kutekwa na kuteswa kwa Dr ULIMBOKA ni gazeti hili lililojitahidi kuandika habari ile kwa uwazi na tukio hilo ndilo lilishindilia gazeti hilo kufungiwa kwa muda usiojulikana.

Wito wangu kwa serekali hii ya JK walifungulie gazeti hili ili kila kitu kiwekwe wazi,,,, mambo ya kuficha kwa dunia ya sasa hayapo tena na kila kitu kitajulikana tu.

Habari hizi ni miongoni mwa zilizoandikwa na gazeti hili kwa waliokuwa wasomaji wa makala za MWANAHALISI.................................................................................................................

siku hizi sinunui gazeti tena.Mwanachi na Nipashe ndio kidogo yanaweza nifanya nisijutie hela yangu baada ya ku-scan kurasa haraka haraka.Ila nayo kuna siku ni vichwa vya habari tuu na si habari,kwani habari nyingine ni shallow kuliko postings sa kawaida kabisa ktk jf.Halafu bado ni mzigo wa makaratasi.

Huwezi amini kuna vipindi nimejikuta najilaumu nunua gazeti kabla sijpokea change.Na huwa sipendi rudisha,ila siku hizi huwa naona ni bora mlipa kijana muuzaji bei kubwa kuliko faida ya gazete nilisome halafu nimrudishie auze tena au awarudhie uchafu wao.Ni bora muungisha yeye kuliko wamiliki wa magazeti wasio na huruma na nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom