Pengo: Kilimo Kwanza ni wimbo tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo: Kilimo Kwanza ni wimbo tu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lunyungu, Dec 16, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

  Na Minael Msuya
  Mwananchi

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuna kila dalili za kukwama kwa Mkakati wa Kilimo Kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.

  Kardinali Pengo alitoa kauli hiyo jana katika hafla ya kuzindua jengo jipya la maabara katika Chuo cha Teknolojia ya Uhandisi cha Mtakatifu Joseph kilichopo Mbezi Luguruni jijini Dar es Salaam.

  Jengo hilo limepewa jina la ‘His Eminence Polycarp Cardinal Pengo Block’.

  Kauli ya Kardinali Pengo inakuja wakati serikali imekuwa ikielekeza nguvu nyingi katika kutekeleza mpango huo mkubwa, ikiwa ni pamoja na kusambaza matrekta mikoani.

  Akionyesha mtizamo huo tofauti, Pengo alisema, "Kaulimbiu inayotumiwa na viongozi wa nchi (Kilimo Kwanza), haiwezi kubadili au kuleta maendeleo katika kilimo, cha msingi hapa ni kumwezesha mkulima kwanza ili apate elimu ya kuendeleza kilimo.”

  Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.

  “Mkakati wa Kilimo Kwanza umekuja wakati mwafaka, lakini cha msingi ni kumuelimisha mkulima kwanza, hii itasaidia kilimo kiweze kuwa na maendeleo kwa kuwa wakulima ndio wanaotakiwa kuwezeshwa kielimu,” alisisitiza Pengo.

  Pengo ambaye ni nadra kuzungumzia utendaji wa serikali, alisema kilimo kimekuwa kikizungumzwa kama wimbo, bila kuweka nguvu katika utekelezaji wenye kuwawezesha wakulima ambao ndiyo wahusika wakuu.

  Alisema jambo hilo linachangia ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hasa maeneo ya vijijini.

  “Kwa kuwa kilimo kimekuwa kikizungumzwa tu kama wimbo, vijana wengi wamekuwa wakiondoka vijijini na kukimbilia kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, wakifikiri watapata maisha bora, kumbe wanakuja kukutana na ugumu wa maisha na kupoteza mwelekeo wao kabisa," alieleza.

  Alisisitiza kwamba, kutokana na hali hiyo vijana wengi wanaoishi maeneo hayo hukimbilia mijini wakifikiri ndiko kwenye fedha na badala yake hutumbukia katika dimbwi la umaskini na kujiingiza kwenye matendo mabaya.

  Kiongozi huyo wa kiroho wa Kanisa Katoliki, alisisitiza kuwa serikali ina wajibu kuhakikisha elimu ya kilimo inaifikia jamii na kumwezesha mkulima kwanza.

  Alisema atahakikisha elimu juu ya hilo inatolewa kumwezesha mkulima kwanza kupitia chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya kilimo kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa kilimo.

  Akizungumza na gazeti hili baada ya uzinduzi huo, mwanzilishi wa chuo hicho Thamson Ananth, alisema chuo chake kitaanza kuwapatia wanafunzi elimu ya kilimo kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka 2010.

  Alisema lengo ni kusaidia utekelezaji na kuikuza kauli na dhamira ya kumuwezesha mkulima kwanza na kuendeleza kilimo.

  Aliongeza kwamba, baada ya Agosti mwaka 2010 chuo chake kitakuwa kikitoa elimu hiyo ya kilimo kwa wakulima kupitia chuo chake cha Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma kwa vitendo.

  “Tutatoa elimu ya kilimo kwa kipindi cha miezi sita, tunaamini kauli ya kumwezesha mkulima itakuwa na nguvu kwa kuwapatia wakulima mafunzo hayo ya kilimo kwa vitendo kwani nao wataeneza elimu hiyo kwa wananchi," alisema Ananth.

  Tangu serikali kutangaza mpango huo wa Kilimo Kwanza, kumekuwa na maoni na mitazamo tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali huku wengine wakihofu kushindwa kwa mpango huo kutokana na kutomlenga zaidi mkulima.

  Kuanzia uhuru, kumekuwa na kauli mbiu ambayo ilikuwa ikisisitiza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na serikali ya awamu ya kwanza, ilitekeleza kwa vitendo na asilimia 80 ya Watanzania waliishi kwa kutegemea kilimo.

  Lakini, sekta ya kilimo ilianguka zaidi nchini baada ya mageuzi ya kiuchumi miaka ya 1990 hali ambayo iliua viwanda vya uzalishaji dhana na pembejeo za kilimo.

  Tayari kulikuwa na mipango mbalimbali ikiwemo ile ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mapinduzi ya Kijani na sasa Kilimo Kwanza kama mkakati mkuu wa kitaifa.

   
 2. p

  p53 JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sahihisha hiyo title yako.Ni Pengo siyo Pendo.Sijui mnakimbiliaga wapi na hizi copy paste zenu
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwa hili tunapiga hatua, maoni huru kama hivi yanasaidia sana kujenga nchi. Heko kardinali Pengo....Watanzania tumechoka kusikia wasomi wenye uelewa wa mambo wakiunga mkono hoja za kipumbavu ili mradi aliyesema ni kiongozi ccm/ serikali.
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wewe Mhehe nini? Mbona badala ya Pengo imekuwa Pendo? Hakuna uhusiano wa karibu wala wa mbali kati ya hayo majina mawali. sasa wewe umetafsiri kwa lugha gani?
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Moderator tafadhali nisaidie kubadilisha jina la Pengo mnisamehe kwa kukosea.
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kilimo kwanza itaongeza rate ya umaskini Tz.
   
 7. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JK anasema wanao criticise wana wivu:)
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kilimo kwanza ni slogan kuelekea uchaguzi mkuu, maana hata hawajatupa maelezo juu ya failure na mafanikio na MKUKUTA na MKURABITA, WANALETA MISAMIATI KUFICHA MAPUNGUFU YAO.
  mimi nawashangaa sana, naungana na Pengo kua tuanze na viwanda kisha mapinduzi ya kijani yatawezekana......hebu angalia EMBE, NANASI NA MATUNDA Mengine yanavyooza mitaani , huwezi kuendelea kwenye kilimo kama wakulima hawawezi kuondokana na hasara hizi baada ya jasho jingi...
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  viongozi wa tanzania wakiishiwa hoja wankuja na maneno ya kujitetea yasio na maana
  Mkapa= MiTanzania mingine ina wivu wa kijinga
  JK= 70% ya watanzania wanafata upepo

  sasa hapa nadhani kuna wakinapengo, Butiku na wengineo wanaingia kwenye hiyo ya Mkapa, na wengine tunafuata mkumbo wa kuvaa tshirt na kofia za ARI MPYA, KASI MPYA, NGUVU MPYA, na sasa KILIMO KWANZA nadhani wanaingia kwenye hiyo ya JK

  na mwisho kabisa JK anasisitiza UKILA SHARTI ULIWE
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,501
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Hivi yale mamilioni ya JK yameishia wapi???
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Get to the point mpwa si umeisha elewa ni nani anaeongelewa hapo juu sasa badala ya kutoa maoni yako we watujazia QUOTE hapa kwa page.

   
 12. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Cardinal Pengo amenena. Ni kweli ili kuwa na mabadiliko ya kweli kwenye Kilimo inabidi tuanze na wakulima. kauli yake ya WAKULIMA KWANZA ni sahihi kabisa na ina nguvu na radhaa nzuri kuzidi kauli mbiu ya KILIMO KWANZA. Tunawaombea mafanikio zaidi katika mkakati wao kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo wanachotegemea kukijenga mkoani Ruvuma kwenye eneo la Hekta 3,000.

  Kutokana na azma hii ni muhimu Serikali ikaangalia namna ya kuwasaidia kifedha. Suala ni uamuzi kwani fedha zipo.
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Alichosema Pengo ni ukweli mtupu; mabadiliko ya kweli hayatatokana na kauli mbiu za watu toka makao makuu bali elimu bora na uwezeshwaji wa wakulima huko vijijini.

  Labda ambacho pia Pengo angeongelea pia ni wajibu wa kanisa na wadau wengine wote katika kufanikisha hilo lengo la kumpa elimu Mtanzania na kumwezesha. Kama ambavyo kanisa limeshiriki vya kutosha kwenye masuala ya elimu na afya, wana nafasi pia ya kushiriki ipasavyo kwenye kilimo.

  Miradi ya kilimo inayoendeshwa na kanisa au msikiti kwa kushirikiana na waumini wao inaweza kuwa chanzo cha elimu kubwa na mabadiliko ya kweli kwa waumini hao.

  Kwa Tanzania wakati mwingine dawa sio kunyosheana vidole kila siku bali kuamua kushiriki kwenye jambo fulani na kuonyesha kwa vitendo kwamba we can do better than those folks in the government.
   
 14. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo makada wamesemama wanaompinga Jk NI WAHAINI ,KWANINI AWAKAMATWI.
  Kweli hii ni kilimo kwanza kabisa.
   
 15. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  This is what we call "walking the talk". Serikali ni maneno matupu jana nilimuona Waziri Wasira katika Jambo Tanzania-TBC1 anamungunya maneno kuhusu kilimo kwanza ni siasa tupu! Welldone Cardinal Pengo
   
 16. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtanzania, ulichosema ni kitu cha msingi sana. Binafsi sina wasiwasi na kanisa katoliki watafika mbali sana na hicho Chuo chao Kikuu cha Kilimo wanacho tegemea kukijenga mkoani Ruvuma kuanzia mwakani, 2010. Historia ya utendaji wao na mashirika yake ni ushahidi mzuri linapokuja suala na kuanzisha taasisi mbalimbali na kuziendesha kwa ufanisi pamoja na miradi husika.

  Kwa upande huohuo, naamini dini zetu zikiamua kushirikiana na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kumkomboa mkulima tutafika mbali sana ndani ya miaka 10 ijayo. Hapa napata wazo la dini zetu la kuwa na Mfuko wa Pamoja kwa ajili ya wakulima wetu hasa upande wa elimu na uwezeshwaji kama alivyoshauri Cardinal Pengo. Njia endelevu na nzuri ya kupata fedha kwa ajili ya Mfuko huo ni kuwa na UTARATIBU WA KUTOA SADAKA MAALUM KILA WIKI KATIKA NYUMBA ZETU ZA IBADA. Iwapo wazo hili litakubalika na kutekelezwa, sitashangaa kila mwezi Sadaka Hii maalum kuzidi shilingi bilioni 20 toka kwa zaidi ya waumini milioni 30 waliopo nchini mwetu.
   
 17. O

  Omumura JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kilimo kwanza ni mradi wa vigogo wa nchi hii kupata nafasi ya kuuza matrekta yao kupitia halmashauri za wilaya huku wakiwaacha wananchi maskini wakiendelea kulima kwa jembe la mkono na kuwa maskini, heko Cardinal Pengo kwa kuwaambia ukweli.
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa safarini mikoani hivi karibuni, kusema kweli kilimo kwanza is a serious joke. Mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya njiani ukipita mkulima bado yuko vilevile jembe la mkono, shamba lake halijaongezeka ukubwa, mbolea anabeba kichwani yeye mtoto wake na wajukuu kupeleka shambani. Literally hakuna kilichobadilika hebu tuelezeni vizuri kilimo kwanza maana yake ni nini mkulima mtanzania au kuna mkulima mwingine anayefikiriwa.

  Mnahangaika na power tillers, kama mkulima anashindwa jembe la kukokotwa na ng'ombe atawezaje power tiller ambayo itakuwa chini ya halmashauri ya wilaya yenye viwavi vyenye njaa ya pesa. Mkulima atasalimika mikononi mwa maafisa wajanja wa halmashauri?

  Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.

  Wazo la kilimo kwanza sio la mkulima Mhadhama Kadinali Pengo yuko sahihi kabisa, kwa vile mkulima hakuhusishwa wazo hili haliwezi kufanikiwa kwa mkulima mtanzania, linaweza kufikiwa kwa walengwa ambao sio wakulima Watanzania
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kilimo kwanza pesa zake zinatokea Ireland na JK na wenzae wamechukulia kama kauli mbiu ya CCM . Hawakuwa na wazo hili ila kwa kuwa mapesa yanatoka kwa wazungu wamechamkiwa sana na mwisho hakuna lolote . Hakuna cha kilimo kwanza wala nini ni ubabaishaji mkubwa . Fika kijijini kwetu huku wala hawana habari na Kilimo kwanza ila iko majukwaani huko mjini na huko hawalimi .
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Watanzania bwana. Hivi mnafikiri wazungu walipewa elimu kwanza ndio wakaanza kuwa wakulima wazuri?

  Ukienda huko Songea watu wanajua kucheza ngoma vizuri bila kupewa mafunzo yoyote yale. Wengine wanacheza vizuri unafikiri walizaliwa wakiwa wameshikilia ngoma.

  Tuachane na mambo ya ubishi ubishi. Kuna kazi haziitaji elimu hata kidogo na mojawapo ni ya ukulima. Fomula zote za kulima vizuri zipo na watu walichazitumia kwa zaidi ya miaka 2000 kwanini mnapoteza muda kutaka kusomesha watu?

  Hata suala la kilimo mnataka kuingiza siasa.
   
Loading...