Pendekezo: Wabunge watokane na Madiwani wa Jimbo husika

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Kuepuka gharama, rushwa na mlolongo mrefu wa majukumu.

Napendekeza hivi:
  • Diwani awe na elimu ya chuo,
  • Mbunge atokane na madiwani,
  • Mkiti/Meya wa jiji/halmashauri/Mji/Manispaa
  • Wawe mbadala wa mbunge anapofariki au tatizo lakiafya.

M/Kiti Msaidizi:
Meya msaidizi apande na madiwani wamchague msaidizi.

Itungwe sheria,bunge kama haliisimamii serikali madiwani kila jimbo lipige kura yakulivunja bunge nakisha apelekwe mbunge kupitia madiwani bila uchaguzi kwa wananchi.

Mawaziri watokane na utumishi wa umma kwa kuteuliwa na Rais kisha kuthibitishwa na bunge.

SPIKA/NAIBU wawe wanasheria na waombe kupitia TLS na jina lipelekwe kwa katibu wa bunge.
Katibu wa bunge awe mtumishi wa umma ateuliwe na Rais.

Wagombea wa USPIKA/UNAIBU SPIKA wasiwe na itikadi ya chama chochote.

Kwakuwa madiwani wapo karibu na wananchi na Rais akiona bunge halina afya ni jukumu la madiwani kupiga kura zakutokuwa na Imani.
 
Back
Top Bottom