Pendekezo: Unaibu Katibu Mkuu CHADEMA apewe Ben Saanane!

Pendekezo: Unaibu Katibu Mkuu CHADEMA apewe Ben Saanane!

Makaura

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
892
Reaction score
295
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CHADEMA,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zitto!

Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CHADEMA itaimarika!

===================
UPDATE BY BEN SAANANE
===================

Nyakageni na WanaJF,

Asante....

1: Uchaguzi ndani ya Chama bado na katiba ya chama ya mwaka 2006 ndiyo itakayotoa muongozo

2:Viongozi waliopo wanaendelea kufanya kazi na tunawasaidia katika ujenzi wa chama

3:Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu inahitaji uzoefu zaidi nje ya vigezo vya taaluma.Ni nafasi inayoshikiliwa na mtu ninayemheshimu kama kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia na ibara inayosimamia uchaguzi wa Naibu Katibu Mkuu ndiyo inayosimamia uchaguzi wa Katibu Mkuu baada ya Mapendekezo.

Ndani ya Chama wapo Kaka na Dada zangu walionizidi umri na uzoefu.Hizi ni tunu ninazozienzi katika utendaji wangu ndani na nje ya taasisi za kisiasa.Uzoefu wao ni wa muhimu zaidi katika kipindi hiki chenye changamoto

4:Nimetoa mchango wangu katika harakati za chama kabla sijawa kiongozi na au mtendaji wa chama makao makuu,siku zote ninaweka mbele maslahi ya chama kwa kushirikiana na wanachama na viongozi bila kujali vyeo

5:Mleta mada Makaura: Asante kwa kuwa na imani nami na wote walioonyesha imani yao kwangu kwa sababu walizo nazo.Mmenitia nguvu zaidi,sitaisaliti imani yenu kwangu kwa kubweteka bali njia pekee ya kuienzi imani hii ni kuebdelea kukitumikia chama na taifa letu kwa bidii kupitia nafasi niliyonayo.Nimeipitia thread hii kwa kina usiku huu

Kuna walionishauri kama wanachama,watanzania wasiokua na vyama au wenye vyama lakini vyama kinzani,kuna walioshauri kama Kaka na Dada zangu walionizidi umri na uzoefu (bila kujali umri).Mungu awabariki

Pia waliotoa mawazo hasi bila kujali itikadi zetu hata kama ni wa upande ule mwingine(CCM),nimewasikia na hii ndiyo demokrasia.Mmenisaidia kujijenga na kuinarisha ngozi yangu izidi kuwa ngumu

Wale waliotunga stori za uongo kwa nia ya kunichafua,wametekeleza wajibu wao waliotumwa/waliojituma.Sina tatizo kwani Ukiwa Mwanasiasa na ukasifiwa na watu hasa wapinzani wako kila siku basi ni bora uache siasa.Waliotunga stori za uongo na matusi,Hakika nao wameingia katika historia nyeusi katika kukuza demokrasia ya vyama vingi

Naomba niseme wazi,tunajiandaa na uchaguzi ndani ya chama.Muda ukifika kwa rehema zake Mwenyezi Mungu nitachukua hatua za kidemokrasia kwa nafasi ambayo nitaona ninaimudu kulingana na mahitaji ya muda na baada ya kutathmini mchango na matokeo ya mimi kuwa katika nafasi hiyo katika kukivusha chama katika kipindi hiki cha ukombozi wa pili endapo wanachama watanipa ridhaa kwa mujibu wa katiba ya chama chetu.

Nitatangaza nia yangu hadharani kama nilivyofanya tarehe 28/04/2011 nilipotangaza Rasmi mbele ya waandishi wa Habari pale Travertine Hotel nilipotangaza nia yangu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Vijana Taifa.Sina woga,napenda uwazi.

JF kama Mwalimu wangu,mlezi na rafiki katika safari yangu katika jangwa atakua wa kwanza kujua hatua nitakayopiga

Asanteni sana kwa kura ya imani (Hasi na Chanya),tuendelee kujenga chama chetu na tumuombe Mungu atutangulie mbele ya safari yetu.Jambo la Muhimu tuweke matumaini mbele juu ya mustakabali wa chama chetu kupitia mamlaka ya kikatiba,ili kiu na ndoto ya kuona Tanzania yenye Neema na ya kujivunia inafikiwa siku za usoni.Mbarikiwe!!!
 
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zito! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!
wazo zuri, Zitto pia anaweza kuchukua nafasi ya juu zaidi kama akipenda. lakini pia napenda kumwona Ben akijitosa kwenye jimbo lolote kwa ubunge 2015. ni kijana anayejenga hoja na si mkurupukaji kama walivyo vijana wengine. hawa ndiyo wanasiasa makini ambao Tanzania inawahitaji.

Ingawa kwa sasa hoja kuu ni kuimarisha chama na si kuchaguana.
 
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zito! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!

Wewe!akamalize wenzake na sumu?!naona huitakii chadema mema wewe!
 
wazo zuri, zitto pia anaweza kuchukua nafasi ya juu zaidi kama akipenda. Lakini pia napenda kumwona ben akijitosa kwenye jimbo lolote kwa ubunge 2015. Ni kijana anayejenga hoja na si mkurupukaji kama walivyo vijana wengine. Hawa ndiyo wanasiasa makini ambao tanzania inawahitaji.

Ingawa kwa sasa hoja kuu ni kuimarisha chama na si kuchaguana.

jimbo la Hai ,akapambane na Mbowe
 
Huyu kijana ana toaga hoja zilizosimama mawazo yakd ni ya juu sana
wazo zuri, Zitto pia anaweza kuchukua nafasi ya juu zaidi kama akipenda. lakini pia napenda kumwona Ben akijitosa kwenye jimbo lolote kwa ubunge 2015. ni kijana anayejenga hoja na si mkurupukaji kama walivyo vijana wengine. hawa ndiyo wanasiasa makini ambao Tanzania inawahitaji.

Ingawa kwa sasa hoja kuu ni kuimarisha chama na si kuchaguana.
 
Hebu tupe strengh za Ben Saanane zitakazofanya CHADEMA iimarike akipewa unaibu katibu mkuu?

Nitafurahi ukianisha mapungufu ya Zitto pia yaliyosababisha CHADEMA isiimarike.

Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zitto! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!
 
Hebu tupe strengh za Ben Saanane zitakazofanya CDM iimarike akipewa unaibu katibu mkuu?

Nitafurahi ukianisha mapungufu ya Zito pia yaliyosababisha CDM isiimarike.

Kwasababu ni kiboko ya Nape na Mwigulu.
 
Hebu tupe strengh za Ben Saanane zitakazofanya CDM iimarike akipewa unaibu katibu mkuu?

Nitafurahi ukianisha mapungufu ya Zito pia yaliyosababisha CDM isiimarike.

Hawezi kukupa kakurupuka tu baada ya kumaliza.......!
 
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zito! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!

Ben Saanane mtu ambae ana kashfa nzito ya kutaka kujua wenzake kwa ajili vyeo Leo hii ndio apewe madaraka hayo ili awamalize wenzake vizuri? Au wewe Mwenye ID hii ndio BEN mwenyewe umeingia humu ku test upepo mkuu.
 
Hiyo sumu ulimuuzia wewe?Mbona Chama chenu kinaongozwa na jangiri maarufu kama Dentist na hamsemi kitu chochote?
 
huyo BENSaanane huwa anatembea na sumu mifukoni na anazo tuhuma za ugaidi
 
Last edited by a moderator:
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zito! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!

Siku hizi rafiki umekosa hekima namna hii?..nani kakuambia Zitto hafai? Au gamba wewe...shenji kabisa
 
Hatimaye uchaguzi umekaribia ndani ya CDM,mi naanza kwa kumpigia kampeni Ben Saanane achukue nafasi ya Zito! Naamini akiingia kwenye uongozi bila shaka CDM itaimarika!
Kweli kabisa anafaa kutokana na ukaribu wake na Dr. kumbe Kujipendekeza kunalipa?
Msimsahau mwenzake EXaud MAMUYA naye pia anataka ubunge wa VUNJO MREMA kaachonjo.
Kweli CDM inaelekea vyema.
mamuya.jpg
 
Kweli kabisa anafaa kutokana na ukaribu wake na Dr. kumbe Kujipendekeza kunalipa?
Msimsahau mwenzake EXaud MAMUYA naye pia anataka ubunge wa VUNJO MREMA kaachonjo.
Kweli CDM inaelekea vyema.
View attachment 113975
Ningeshangaa sana kama nisingeona uharo wako kwenye hii Post.Haya endeleeni kupiga ramli sisi tuko site CHADEMA NI MSINGI.
 
Back
Top Bottom