Pendekezo: Tanzania iweke Balozi Uholanzi!

Pendekezo: Tanzania iweke Balozi Uholanzi!

It is igh time now kuwa na ubalozi Uholanzi
 
Mzee Es
Huu ujumbe wa ubalozi kutakiwa huko Uholanzi umesha upeleka maana najua JK anajua fika lakini ataweza kumuondoa jamaa ? Maaa nasikia hata BM siku anaambiwa tena mbele ya mzungu huyo alisema unajua Holland wana msaada sana na ukimuondoa si vyema nk . Haya yalikuwa majibu ya BM na sasa mzungu kesha jikita hadi hazina yetu kama nilivyo soma hapo juu je JK anaweza kumuondoa ? Hebu Es sema kama umesha fikisha ujumbe bro.
 
tafiti bado hujamaliza utafiti wako maana ulisema kwamba madai ya hap hayakuwa ya kweli kwa kuwa ulipita Ulaya July baada ya kombe la Dunia je una nini cha kutueleza maana ili info ziwe credible lazima ujisafishe kwamba ulikosea kusema habati ambazo hukuzijua na watu wana zijua vinginevyo hatutakuamini kabisa .Rekebisha hili kwanza kama ulikosea sema ama kama una info lete hapa hadharani usiingie mitini .
 
eeeeh, tafiti uliahidi kuja na data au ku admit kuwa ulikosea baadhi ya vitu.. kama vile kusema watu wa ubalozi walikwenda Uholanzi kushughulikia paspoti .. ilhali wenye we kina Mugishagwe walioko huko wanasema hajawahi kuja ofisa yeyote kwa shughuli hiyo. Unasubiriwa hapa.. muda umekuwa mrefu. Kama unavyowashauri wengine ... muda wa kuadmit kukosea bado upo!
 
Ndiyo bwana kusema samahani nilitleza ni uungwana na pia watu mjifunze kuto kutetea jambo tu kwa kuwa unapenda kitu ama kwa maslahi. Hii issue Mugishagwe na Ubalozi tuko wengi tunaijua mshangao wa tafiti unafanya sasa kila alisemalo hapa tuwaze kama tumuamini ama hapana . Mimi Nakutajia sasa si Mama Nyagetera wala Zoka wala yule Mama wa Kihindi au yule jamaa mfupi wa huko Iringa alifika .Hawa jamaa walifika Uholanza siku ambayo BM alitia timu Uholanzi na issue ya Passport ilikuwa moto mpaka huyu Mkurugenzi ikabidi aombe msamaha.Lakini kabla ya hapo kuna watu walifanyiwa mauza uza na ubalozi ukawa unasema hauna majibu na mmojawapo wa watu hao walitafutwa na Mkurugenzi kwa uharaka na kuombwa kutulia il yaishe maana yeye alisha pelekewa PP yake hadi nyumbani kwake .Unasemaje ?Bado unataka data ili utafiti ama umelowa useme ukweli ? Mjihadhiri na ushabiki wa mambo ambayo hamna uhakika nayo ndugu zanguni .
 
Naam kama nilivyowahi kuweka wazi hapa kwamba mimi ni mwepesi sana kuadmit nikiwa wrong na sioni aibu wala fadhaa kwa hilo ila ni baada ya kuujua ukweli upo wapi ndio huamua kufanya hivyo.

Nilikuwa Ubelgiji nikitokea Ujerumani nikapitia nchi zote mbili yaani Uholanzi na Ubelgiji, nashukuru nilifanikiwa kukutana na mheshimiwa Balozi wetu Mlay na pia afisa Mkuu ZOKA na mama Nkamba ambae ni administrative assitant.

Katika mazungumzo nao waliniwekea wazi kwamba hakuna watanzania wengi nchini Ubelgiji kwa sababu za lugha zinazotumika yaani kifleming na kifaransa hivyo kwa wao kuonana na watanzania basi huwa wanawaona sana Uholanzi kwa vile hapo kiingereza huwa kinatumika kiasi na wakatoa mfano kuwa recently walikwenda kugawa fomu na kuchukua fingerprints za hawa watanzania.

In fact mama Nkamba ambae aliishi sana Tanzania anasema huwa anapata muda wa kupractice kiswahili chake.

I did not have any reason kuidesbelieve hii habari na kwa hakika nilipoahidi hapa kwamba ninafanya utafiti nilikuwa nikijaribu kuwasiliana na ubalozi wetu belgium na pia kujua kama kuna mtanzania yeyote ambae anaishi Holland aliewahi kuchukua pasi kwa kufuatwa na maafisa hao, bahati mbaya sana watanzania wote [watatu] niliobahatika kuongea nao wanaishi kama wakimbizi wa nchi nyingine [what a shame] na jitihada zangu za kumpata bwana ZOKA zimegonga ukuta kwa vile nilipiga nikaambiwa yupo safari.

Kwa vile ni habari ongoing hapa naendelea kusaka ukweli lakini naona kutokana na challenges kwa wingi ni vyema niweke wazi kuwa sijaona kama kuna upotoshaji wa ukweli kwa upande wangu, i provided the information in good faith based on the information obtained first hand from the officials concerned by myself sasa sina sababu ya kutoamini kuwa hawajafika lakini kama obviously kwa vile kuna watanzania hapa wanaoishi Uholanzi basi inawezekana kuwa wao wakawa na uhakika zaidi hivyo kiungwana kabisa nimeonelea niwithdraw my earlier statement due to lack of supporting evidence na nawaomba radhi wale wote ambao habari hii imewaoffend in one way or the other, this was not my intention.

I still believe there is no justifiable case to have the embassy of tanzania in holland based on my other arguments, again aopologies to all the parties affected.
 
Mi nakupongeza kwa hili la kutoona tabu wala kuwa too proud to admit a mistake. Ni wachache wenye kuliweza hili... hata wakiwa na uhakika 100% kuwa wamekosea bado watapinga au the best they can do ni kukaa kimya.

Kuhusu kuwepo ubalozi, you are entitled to your own opinion, but I would think walio uholanzi wanafuatilia zaidi ushirikiano wa nchi hiyo na Tz .. they are in a better position to feel the need as to whether ubalozi unatakiwa kuwepo au la.. kuliko wewe uliopita siku mbili tatu tu.
 
Kwako tafiti hongera sana kwa kuwa mweli .Maana nilijua kwenye hili huna ujanja utaongelea habari za ubalozi lakini si huduma za balozi zetu nje . Mimi nimeingia Dar leo lakini ni mimi niliye waambia watu wa ujerumani kwamba nendeni mkapate habairi za PP mpya Ubelgiji .Yaan Karume na watu hawakujua kama tunabadilisha PP na hata walipo pewa gazeti walisema hawana muda na magazeti .It was a very frustrating situation watu wakawa wana haha nikawaambia kupitia forum kwamba fika Brussels pata huduma wakati mimi nikiwa nimesha chukua finger print huko .

Zoka was not able to leave the office japokuwa alikuwa tayari kwa kuwa allowance ilikuwepo lakini hakutoka .Ulikuwa unapiga simu unapata appointemt ndiyo una enda kufanya mambo ya vidole .Brussels kiasi wana sae vizuri Watanzania .Zoka is a good guy ila kama yeye na balozi walikueleza habari hizi za kuja Holland kwa ajili hiyo nasema ni waongo naweza kuwaeleza haya hata mbele ya rais.

Ubalozi haujui nani anakaa wapi si Brussels wala Konshula .Wana matatizo kidogo siwezi kuingia huko haya ni mambo yao na ndiyo maana tunasema tunahitaji Ubalozi .Kuna mengi ya kusema lakini mengine tunaachia kweney vikao we know better than you do .Wewe ulipita na kusema but we lived with them .Kwa mfano kuna Nyerere day hii inafanywa na watanzania a Uholanzi kwa kukusanyika na kufanay Ibada na baadaye kwenye hall na speeches etc. Muulize balozi Mlay kesha kuja mara ngapi ? None nina ushahidi .Kuna watanzania wana maliza masomo wanaomba balozi ma ubalozi uwepo . Muulize kesha kuja mara ngapi? Hakuna hata siku ila Mama Nyegetera na Zoka been down there a couple of times kama mara 2 hivi .Sasa mengine nin kujiosha .

Ukifika kwao wan huduma nzuri sana sana sana lakini waache tuwasifie sisi.Konshula anataka yeye awe mkuu wa shughuli za Kitanzania mbele ya Watanzania na watanzania wanamtaka mweusi mwenzao kazi inaanzia hapo .Umenielewe hapa nini kitafuata sitaingia huko .Au niseme kuna conflict of ........................ utamalizia na kazi ni kwa mzungu na si Ubalozi wetu ndiyo tunasema we need Ubalozi .Acheni mauza uza kumbe wew unaongea na wakimbizi ambao hata ofisi ya konshula hawaijui iko wapi na wala mikusanyiko ya Watanzania hawafiki utajua nini Mzee tafiti poleeeeeeeeeee
 
Bravo Mzee Shughuli,

Maneno mazito hayo!, isipokuwa kwa hii forum tuna kazi kweli kweli!, yaani let me get this straight, ukikamatwa huna ukweli jawabu ni kusema AAahhhhhh mimi ninakubali lakini wengine humu hawakubali? Unapaswakusema Jamani samahani kwa kutaka kuwapotosha bila ya kuwa na ukweli, FULL STOP!

Hadhi ya hii forum haiwezi kujengwa kwa kukwepa responsibility na kujaribu kuwarushia wengine kubali yaishe basi, ama sivyo mnaishusha hadhi ya hii forum na haya mafumbo yenu yasiyokwisha, mikikamatwa kubalini kuwa hamjui, PERIOD!

Msilete hadithi za Abunuwasi hapa, sisi wote ni watu wazima hapa umekamatwa kuwa hujui ulichoahidi au hujui ulichokisema as the case katika hii mada, kubali yaishe, na ndio maana tulisema huo ukweli wa 100%, mnaoudai hamuuwezi na hatuutaki maana tulijua kuwa sisi wajumbe humu sio PERFECT, tulijua kuwa mambo kama haya ya mjumbe kuja humu na kusema asichokijua yatatokea na ni kawaida kwa binadamu, ndio maana mzee Fillga nimeomba wajumbe wapewe muda wa kufikiri kwanza kuhusu sheria, huu ndio mfano wenyewe maana kama ingepitishwa ile sheria jana kama yeye mwenyewe alivyolilia,

Leo angekuwa Ex-member, hiyo hatutaki maana tunaheshimu michango yenu na tunaelewa binadamu sio kamili hukosea kama mlivyokosea hapo juu, ila mkikosea, kubalini bila mafumbo ama sivyo apology yenu inakuwa sio ya kweli, na ya kudharau hii forum, dawa ni kukubali yaishe, ndio uungwana!

Walllahi, I love this forum, IDUMU!
 
Kwenye hili nilijua kwamba tfiti hatfika mbali maana alianza na mbwembwe nalo .Nikajua huyu kanasa kwenye matope mazito .Ujue bwana tafiti kwa taarifa tu hata huyu konshula ambaye wewe unadhani kwamba ni bora aendele kabla ya kuwajua watu kama sisi hapa marafiki zake wakubwa walikuwa hawa wakimbizi wa uongo , yaani wote mna bahati ya kujuana na wakimbizi wakati watu kibao tuko hapa.Nina habari za uhakika kwamba aliwasaidia hata wengie kuja Holland na wakaingia mitini hadi leo na hawa ndiyo watu wake. Huyu jamaa akikutana na vichwa huwa hapendi kabisa maan anajua maswali na maongezi huwa mazito hayawezi.

Huyu ndiye wakati mmoja watu wanakutana na BM alikuja akakatuta watu wamekaa wanafunzi a MSc na PhD wanaongelea mambo yao bila kujali akawaita kwa kusema hamjambo wasela wa kijiweni? Mambo vipi ? Ama mambo kwa soksi na kilongalonga changu kiko kibindoni.Huyu jamaa ana anadharau sana na sasa kajikita kwenye Utalii TZ na biashara zake za malori na ujanja kibao .

Mambo ya Brussels umesha elezwa na sina la kuongeza ukweli ni huo na hautabadilika kamwe.Kawaeleze kwamba we know much and we cannot be fooled.Ofisi ya Konshula iko porini sana kwenye ofisi yake ya kuuzia magari na ukifika anakwambia mimi ni mfanya biashara na si mwanasiasa .

Je unajua kwamba wakati wa BM kampuni ya Phillips ya ilituuzia utra sound machine kwa kila Wilaya ? Je zinafanya kazi ? Zina thamani gani ? Umeme uko wa kuziendesha ? Kwa nini utra zile wakati huko kwenye hosp hizo watu wanalala chini hakuna vitanda wa njia sahihi za kuingilia hosp ? Kwa faida ya nani?Kazi ya huyu mzungu sasa .Very corrupt na wewe tafiti unaleta zako hapa.
 
Duh! yaani Mugichangwe na Nzee mashughuli bwana mm mmechema maneno ya kweli na kwetu ntupi huyu utafiti naye chijui ana hisa na anaacha kutafiti maneno ........................
 
Watanzania walienda kumuambia Hakkenburg matatizo gani ambayo hakuyashughulikia?.

Ninavyojua Hakkenburg nimtendaji mzuri wa kazi na hana yale mambo ya uswahili swahili yakuzungushana kusiko na msimamo.

En wat nog, Ik heb nog nooit gehoord dat de Nederlanders die naar Tanzania reizen, 't probleem gekregen van meneer Hakkenburg.

Na kama nikiswahili Hakkenburg anazungumza Kiswahili hata kushinda mswahili wa Manzese.
Anajua hata kiswahili cha mitaani.
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti leo kuwa Tanzania imeamua kufunga ubalozi wake nchini Uholanzi sio tuu kutokana na hali ya uchumi bali pia "conflict of interests" kati ya Uholanzi na Tanzania huku Uholanzi ikijikita zaidi kwenye uwekezaji na biashara. Nimesoma taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje lakini haijazungumizia kama ubalozi wetu nchini Uholanzi haujafungwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen: "It is obvious that there was a deterioration of the diplomatic relationship between Tanzania and Holland," said Mr Haule. "We decided to close our office after our colleagues concentrated on protecting their investors and businessmen in the country. Tanzania did not get what it wanted."

All is not lost, though, as the government still owns a house in Holland, which is in the care of the honorary consul. "Our house in Holland brings at least 8,040 Euros to the government every year and, at the moment, we have a honorary consul officer who reports to our embassy office in Brussels," he explained.

Source: http://thecitizen.co.tz/news/-/19759-cash-crisis-hits-foreign-ministry
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti leo kuwa Tanzania imeamua kufunga ubalozi wake nchini Uholanzi sio tuu kutokana na hali ya uchumi bali pia "conflict of interests" kati ya Uholanzi na Tanzania huku Uholanzi ikijikita zaidi kwenye uwekezaji na biashara. Nimesoma taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje lakini haijazungumizia kama ubalozi wetu Uholanzi umefungwa.
Kwani Tanzania ina ubalozi uholanzi?
 
Haya sasa!..
The country is in its final step to collapse!
Save us or Lord!
 
Back
Top Bottom