Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 299
- 58
Barua ya kwazi kwako Ndugu JK rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Nchi tajiri sana Duniani ina mbunga kibaoo, maziwa yenye kutoa samaki hadi Sauper akaja kupatia jina huko,Nchi yenye watu wavumilivu sana na wanaopenda lakini Serikali muda wote ina waangusha lakini hawakati tamaa.
Nchi yenye kuongozwa na watemi na wenye kauli jeuri kama Kalamagi lakini ndugu rais yuko kimya , Nchi inayo sadikiwa kuwa na makaa ya mawe, gesi, mafuta, urenium,madini ya kutengeneza meli, madini kibao , maua nk .
Pamoja na mambo hayo hapo juu bado tunasoma na kusikia toka kwa wakuu walioko chini yako nikiwa na maana ya mawaziri nk kwamba bajeti yetu 50% inagharamiwa na wazungu .Mali tunazao , akili tunazo na uwezo wa kuzifanya mali zetu ziwe msingi imara wa kulambwa na kubembelezwa Duniani hakuna .
Serikalio ya Uholanzi iko kwenye Umoja wa EU lakini kama serikali imekuwa kati ya Nchi marafiki wakubwa sana wa Tanzania kwa hila hali . Wanamwaga mapesa , yao kwa mikopo na hata misaada sawa , wamekuja kuwekeza kwa wingi sana Tanzania na sasa wako watu wao ambao wanafanya biashara na hasa utalii bila ya vibali na hawalipi kodi .
Hili nitaliacha kwa sasa ila nitalisemea pengine .Waholanzi kwa siku za karibuni wamekuwa marafiki wa karibu kuanzia kutoa mafasi za masomo kwa Watanzania kwa ngazi za Masitatz(Masters) na diploma na hata PhD na mengine mengi lakini ndugu Rais hujawahin kufika kwao kujitambulisha .Sijui labda wewe mkuu una sababu yako lakini bado najiuliza sana .
Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na ukaribu wote bado hakuna Ubalozi wa Tanzania Uholanzi.Balozi wetu wa Ubeligiji sina uhakika kama kapata kibali sasa kuja hata kuwatembelea Watanzania wa Uholanzi maana nakumbuka kwaba hata ndugu Mkapa anaenda mwaka jana kuaga Uholanzi balozi alienda kwa special permit .Uone mambo haya na kwa miaka kama 2 sasa tangia awe balozi pale Ubeligiji.
Tuna mtu anaitwa Hakkenburg ni mdachi huyu ambaye kwa kweli ni business minded .Hana habari na watanzania na mambo yake hayaeleweki . Ndugu Mkapa alisema siku ile ya kuagana na Watanzania wa Uholanzi kwamba kwenye handouts zake atakueleza juu ya umuhimu wa kuwa na Ubalozi Uholanzi je umepata ujumbe ule ? Ama bado kuna kubana matumizi hata mahala pale ambapo tunapata faida ?
Ubalozi wa Tanzania ama ofisi ya Konshula Uholanzi iko ofisini kwa huu mwakilishi wa watanzania Mzungu.Hatumbagui lakini pia kwenye habari zake wapi pa kumpata mara ya mwisho niliona kwamba anapatikana The Hague lakini ukweli ni kwamba anapatikana kwenye kijipori fulani ukipita kwenye highway utaona bendera ya TZ imepauka haishuki wala kupanda ilisha panda basi , hakufikiki bila ya taxi ama personal vehicle . Ndugu rais tafadhali fikiria hili ili ulipatie jibu ka Nchi hapa kama kana kuwa msaada mkubwa namna hii kwa Tanzania kwa nini basi tusipate Ubalozi na kuhudumiwa na Mtanzania badala ya sasa ilivyo shida kubwa hata ya kumpata mwakilishi wetu ?
Naomba chonde chonde ulikuwa mkuu wa mambo ya nje unajua vyema kuliko mimi sasa litupie macho hili .
Mimi Mtanzania mwenzio
Mugishagwe Mwana wa Majimoto