PENDEKEZO: Sikukuu ya NANE NANE ifutwe

raymg

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
842
214
Binafsi sion haja ya kuendelea kua na sherehe kila mwaka na kutumia pesa kibao kuandaa maonesho ya wakulima ambayo hujaa bidhaa za wafanyabiashara na kukiuka lengo zma la maonesho hayo.
halafu siku kama ya leo ya wakulima inawasadia nn wakulima wa kijijin kwangu ambao leo wanauza pamba yao kwa Tsh 600/kg huku hali ya maisha ikiendelea kuwa ngumu kila kukicha....
 
Ni kweli kabisa haina mantiki yeyote kabisa, Wanaokuwa kwenye maonyesho mara nyingi si wakulima ni wafanya Biashara tu.
 
yan n njia tu ya kujipatia perDM.....CAG yupo wap
 
Yap ni kweli kama hii kanda a kaskazini maonyesho ya 88 arusha imekuwa biashara ya mitumba na nyamachoma
 
Kweli kabisa sijaona cha maana kinachofanyika katika maonyesho haya. Yalikuwa na malengo mazuri ila yanatumika vibaya
 
Kumbuka kwenye budget za wizara zetu kuna fungu la posho za kwenda kutembelea maonyesho hayo sasa yakifutwa unakuwa umepunguza perdiem za watu kwa mwaka! Napenda ifahamike kuwa kila kitu huwa kuna wanaonufaika na wasionufaika sasa hapa wanaonufaika ndio wanauwezo wa kusema maonyesho haya yaendelee kuwepo au yasiwepo then unategemea nini? Mkulima anakula hasara au anapata faida wao siyo tatizo hata kidogo, wakulima wamekuja au niwafanya biashara ndio wamejaa pale pia sio tatizo. Suala ni kwamba kiongozi kaja, posho yake kesha chukua na waandishi wa habari na makamera yao yapo basi!
 
hiyo pesa wanayotumia kuandaa hii sherehe ingepelekwa kwenye pembejeo za wakulima si ingekuwa swafi kuliko kuwapendezesha wanasiasa tu, kuna picha moja eti Pinda anashangaa maboga na Mihogo
 
mi napendekeza isifutwe japo wanaofaidika ni wale wanauza bia,chips,nyama choma,kiti moto na nguo,acha sikukuu iendelee watu wapumzike wengine wafanye biashara
 
Isifutwe bali iboreshwa kwa kunufaisha wakulima wanyonge wa tanzania.Huko vijijini wao wanasherehekea vizuri tu tena waipenda sana kwani tunawatabua.
 
acheni iwepo na kwa wasioitaka acheni mkae majumbani, kwani wanaoona manufaa wataenda, mbona 77 Dsm wanaenda na huko kuna Makampuni ya nje, Nani angejua km ardhi ya Dodoma ingekubali zaidi ya mazao 20 mapya ya kilimo korosho likiwa mojawapo, au nani angejua kazi za Brela za kuandikisha makampuni ni bei rahisi kuanzia 6,000/ mpaka 300,000/ wakati tulikuwa tukipitia kwa wakala na Wakili unachajiwa hadi 550,000/=
Msipinge kila kitu kwani hata mataifa mengine wana maonyesho yao ya vitu vya asili
MM NINGESHAURI LIGI YA MPIRA WA MIGUU TANZANIA INGEFUTWA KWANI SIONI FAIDA YAKE KWENDA ANGALIA WATU 22 WANASHINDANIA LIGOZI UWANJANI NA MASHABIKI KUUANA ETI SIMBA, YANGA, MAN U nk
jinsi ww unavyochukia hiki na mwenzako hakipendi ni shurti kuvumiliana
 
Ni kweli kabisa haina mantiki yeyote kabisa, Wanaokuwa kwenye maonyesho mara nyingi si wakulima ni wafanya Biashara tu.
Pia wanasiasa, na tena eti leo imeanzishwa zawadi ya kila mwaka ya 'kilimo kwanza' what a FUNNY!!
 
Ni kweli kabisa haina mantiki yeyote kabisa, Wanaokuwa kwenye maonyesho mara nyingi si wakulima ni wafanya Biashara tu.

Mkuu maonyesho hayo ndio mafisadi wanatumia kufuja hela za mashirika ya umma na mawizara, wewe jaribu kufanya utafiti kuhusu gharama zinazo tumika kutayarisha maonyesho hayo - utashangaa sana. Si hilo tu hata utoaji wa vikombe vya ushindi vina utata sana, mashirika mengine wanafanya lobbing ya hali ya juu sana ili washinde ili wapate mwanya wa kuhadaa dunia na viongozi wa nchi hivyo kuwafanya wapate mwanya wa kuendeleza ajenda zao za SIRI.
 
mi nashauri yaboreshwe kwani nilifunga safari toka Dar hadi Moro nilijuta kupoteza muda wangu ni makelele ya muziki unaonyeshwa ng'ombe unauliza wapi naweza kununua ng'ombe wanasema sisi tunaonyesha hatuuzi,aina za ng'ombe zenyewe ni aina mbili wakati tuna ng'ombe aina nyingi tofauti,hakuna wataalamu wa kilimo badala yake wamejaa wauzaji pembejeo na madawa ya kilimo ukiwauliza maswali ya kitaalamu wanashindwa kukujibu zaidi ya kusifia dawa zao ni bora hivyo maonyesho hayo yamepoteza maana zaidi ya kulipana posho na kufanya ufisadi wa kutengeneza tshirti
 
Yaboreshwe ili yaweje , unyoona saiz kuna tatizo gani na kwa nn tucya fute tu...funguka mkuu
 
Back
Top Bottom