Opaque
JF-Expert Member
- Oct 24, 2008
- 1,359
- 732
Ni maoni yangu tu kama mwanachama, kwamba chama cha CUF kitafufua imani ya watanzania na huenda kikapata kura za kutosha za urais iwapo kitamsimamisha Julius Mtatiro kama mgombea urais na Magreth Sakaya kama mgombea mwenza, kutegemea mabadiliko ya katiba kuhusu umri wa kugombea urais. Pia kwa upande wa Zanzibar wajaribu kumsimamisha mtu mwingine mbali na maalim Seif ambaye anaonekana ameshindwa katika majaribio yake kadhaa ya kuukwaa urais sambamba na Lipumba. Lazima tukubali kuwa mgombea urais ana ushawishi mkubwa katika hata kinyang'anyiro cha ubunge wa wabunge wa chama chake, na bila shaka CUF itaongeza idadi ya viti vya ubunge upande wa Bara, kwani Visiwani huwa tuna uhakika wa viti vyote vya Pemba plus kimoja au viwili vya Unguja. Hakuna asiyejua ushawishi wa Mtatiro majukwaani, na wa Sakaya kule bungeni. Ningependa maoni zaidi ya matusi hapa, tusije tukawa kama wabunge wa aina ya Serukamba na Mkamia
