Pendekezo la timeline ya Katiba Mpya 2026-30

Pendekezo la timeline ya Katiba Mpya 2026-30

..unaposema maridhiano una maana gani?

..hebu tuchambulie baadhi dondoo, au hoja, za maridhiano.
Maridhiano ina maana ya vyama vya siasa na serikali kukaa meza moja na kukubaliana masuala yaliyokwama. Dondoo kuu za maridhiano ni:-
1.Muundo wa Muungano: Kukubaliana kati ya mfumo wa serikali mbili au tatu.

2.Tume ya Uchaguzi: Kupata tume huru inayoaminika na pande zote.Mamlaka ya Rais:

3.Kupunguza baadhi ya nguvu za rais kiutendaji
 
Katiba iko . Tunaitaka ile ile iliyopitishwa na bunge 2014.

Hatua iliyobaki ni Wananchi wapige kura kuipitisha ili iwe katiba rasmi.

Tukisema mchakato uanze tena yatakuwa yale yale.

Kuna tume ya Jaji Nyalali, 1991 na tume ya jaji Kisanga 1998 .
Hii ya Jaji Warioba 2011 ni ya tatu na zote zilikuwa na nia ya kurekebisha katiba Na hakuna kitu yoyote imefanyika .

Katiba 1977 ndio inatuongoza. Hizi zote hazijapitishwa. Kwanini?
Miaka 12 imepita kuna mambo mengi yametokea hapo katikati. Kuna haja ya kuhuisha na hali halisi iliyopo kwa sasa
 
Katiba mpya haitapatikana kama CCM ndio itakuwa inaongoza mchakato wa upatikanaji wake, au ikipatikana itakuwa kama tume ya uchaguzi ilivyobadilishwa jina tu kutoka NEC kuwa INEC kisha tukaambiwa ndio tume mpya.
Wewe unataka taasisi gani ndiyo iandike Katiba?
 
Katiba tunayoitaka ni Ile rasimu ya Warioba ambayo haikuchakachuliwa na bunge 2014, hiyo katiba iliyochakachuliwa na bunge ni mbaya kuliko hata ya 1977.
Nakubaliana na wewe kuhusu rasimu ya Warioba na mimeinukuu pale kwenye andiko langu
 
ndio utaratibu, lazima uanzie kwa wananchi, then yale maoni yanaenda Bungeni (hapa haijadiliwi na wabunge ila ni wawakilishi wa wananchi wa kwenye kila sehem,vilema,vipofu,viwete,wamama,wababa,wababu,albino nk).

Alaf inarud tena kwa wananchi kuipigia kura ili iwe katiba rasmi.

Raisi anamalizia kutia tu sign.
Uko deep, asante kwa kumelewesha Yoda . Taratibu ataelewa maana yuko radical sana kama Heche
 
Kosa kubwa lililofanywa kwa makusudi 2014 ilikuwa ni kuligeuza bunge la kawaida kuwa bunge la katiba na kujaza kila aina ya watu ikiwemo wajinga kama Bashite. Bunge la Katiba linatikwa liwe la experts, watu nguli na mashuhuri katika Sheria, katiba, utawala na uchumi.
Sawa kabisa, naafiki hoja hii
 
Wewe unataka taasisi gani ndiyo iandike Katiba?
Bunge maalumu la magwiji wa Sheria, katiba, utawala na uchumi. Sio chombo cha kujaza sijui wakulima, wafugaji, wamachinga, vijana wa UVCCM au BAVICHA, wakina mama na upuuzi mwingine kama huo. Na sheria iwe watakaoshiriki kuwa wajumbe wa bunge la katiba hawatashika nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10 baada ya katiba kupitishwa na hawatashiriki chaguzi kuu mbili zinazofuatia chini ya katiba hiyo.
 
Tuitaka rasimu ya mzee WARIOBA iwe katiba mambo mengine nikutuchezea tu watanzania
 
Bunge maalumu la magwiji wa Sheria, katiba, utawala na uchumi. Sio chombo cha kujaza sijui wakulima, wafugaji, wamachinga, vijana wa UVCCM au BAVICHA, wakina mama na upuuzi mwingine kama huo. Na sheria iwe watakaoshiriki kuwa wajumbe wa bunge la katiba hawatashika nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10 baada ya katiba kupitishwa na hawatashiriki chaguzi kuu mbili zinazofuatia chini ya katiba hiyo.
Ni sahihi kuwa tunahitaji wataalamu (magwiji) kuongoza uandishi wa kisheria na tunahitaji kuweka sheria inayozuia wajumbe kutafuta madaraka kupitia katiba wanayoandika wenyewe.

Lakini ni kosa kubwa kuyaita makundi ya kijamii (wakulima, wafugaji, wamachinga) kuwa ni "upuuzi", kwani bila wao, katiba inapoteza uhalali wa kidemokrasia na haitakubalika na wananchi. Katiba bora inahitaji utaalamu wa magwiji pamoja na sauti za wananchi wa kawaida
 
Huhitaji Wakulima, Wafugaji, Mama Ntilie, Wamachinga, Bodaboda, Wafanyabiashara n.k kuwa waandikaji katiba au wajumbe wa katiba kwa sababu hawana utaalamu wa kuunganisha mambo mbalimbali na kuwa na grand vision ya miaka 50 ijayo bali huwa wanatazama mambo yao machache tu yanayowatatiza wakati huo. Wanaweza kutoa maoni yao kama raia wengine wowote.
 
Hoja hii ni finyu na inajengwa juu ya mtazamo unaotenganisha katiba na uhalisia wa maisha ya wananchi wanaoishi chini ya katiba hiyo. Kupinga hoja hii, kuna misingi mikuu minne ya kisheria na kijamii inayothibitisha kuwa ushiriki wa makundi haya ni wa lazima.

Katiba siyo Nyaraka ya Kitaalamu tu, ni Mkataba wa KijamiiKatiba sio kitabu cha sheria za mahakamani (Statute Book); ni mkataba wa kijamii (Social Contract). Kazi ya kuweka grand vision (dira kuu) haiitaji shahada ya sheria, inahitaji uzoefu wa maisha wa wale wanaozalisha uchumi wa nchi. Zaidi ya 70% ya uchumi na nguvu kazi ya Tanzania ipo sekta isiyo rasmi (Wamachinga, Bodaboda, na Kilimo). Ukawatenga kwenye meza ya maamuzi, unakuwa umetengeneza katiba ya wasomi wachache (Elite Constitution) isiyo na uhalali wa kijamii.

Katiba bora haitengenezwi na magwiji pekee, wala wananchi wa kawaida pekee. Inatengenezwa kwa mseto: Wasomi wanaleta kalamu na weledi wa kisheria, huku Wamachinga na Bodaboda wakileta roho na uhalisia wa maisha ya nchi
 
Back
Top Bottom