Pendekezo la mgomo wa abiria nchi nzima

Pendekezo la mgomo wa abiria nchi nzima

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,316
Wadau bila shaka hamjambo. Nimefikiri kwa kina nikaona kuwa bila migomo na maandamano hakuna haki. Pia kila upande unapokumbana na na migomo kuna sehemu utekelezaji huchukua nafasi na hivyo haki hutendeka.

Najua kidogo ni ngumu lakini tukiamua kusimamisha shughuli zetu kwa kutoa muda mengine yapite tutakuwa tumejiokoa kwa siku za usoni.

Basi naomba na sisi abiria tugome kusafiri nchi nzima ili kurudisha thamani yetu. Tutachezewa na kurudishwa nyuma maendeleo yetu hadi lini?Leo nimetoka Lilambo Songea hadi Msamala kwa bodaboda Tsh 14000 kwenda na kurudi wakati huwa natumia Tsh 1800. Haki iko wapi?Tugome na sisi. Wenu Pastor Achachanda
 
Last edited by a moderator:
Naunga hoja. Ila tuanze mara baada ya madereva kumaliza mgomo wao. Alafu tuandame kwenda ofisi za mikoa kudai haki zetu
 
Ntaenda kazini kwa mguu tu! Hata gari binafsi pia nagoma kununua! Hata safari ya mbali mikoani pia ntasafiri kwa mguu! Sihitaji ushauri wala suluhu yoyote na mtu wala kikundi cha watu ama serikali.

Nimeamua mwenyewe nikiwa na akili timamu bila kushawishiwa na mtu.
 
Wadau bila shaka hamjambo. Nimefikiri kwa kina nikaona kuwa bila migomo na maandamano hakuna haki. Pia kila upande unapokumbana na na migomo kuna sehemu utekelezaji huchukua nafasi na hivyo haki hutendeka.

Najua kidogo ni ngumu lakini tukiamua kusimamisha shughuli zetu kwa kutoa muda mengine yapite tutakuwa tumejiokoa kwa siku za usoni.

Basi naomba na sisi abiria tugome kusafiri nchi nzima ili kurudisha thamani yetu. Tutachezewa na kurudishwa nyuma maendeleo yetu hadi lini?Leo nimetoka Lilambo Songea hadi Msamala kwa bodaboda Tsh 14000 kwenda na kurudi wakati huwa natumia Tsh 1800. Haki iko wapi?Tugome na sisi. Wenu Pastor Achachanda

Imekaa kinadharia zaidi mkuu.

Pata picha mgonjwa anagoma kutibiwa hata kama anapewa huduma duni na hospitali/daktari.

Asipoangalia anaweza akafa yeye. Sio kitu applicable.
 
Last edited by a moderator:
Tukimaliza mgomo huo tunaingia mgomo wa kula, mgomo wa kupiga kura sabab viongozi tunaowachagua vilaza.
Halafu tutaendelea na migomo mingine..
Asanteni
 
Usiige tembo kunya utapasuka msamba. Gari hazijagoma waliogoma ni madereva ambao ni watu. Sasa wewe labda ugome kuvaa viatu na utembe peku.
 
kwa mateso tuliyoyapata tangia jana bora tuamasishane kununua baiskeli. kijana unayependa maendeleo ya nchi yako, achana starehe, achana kulea nyama uzembe piga pedo hadi town .faida hakuna foleni,hakuna kugombania. ni afya kufanya mazoezi sasa.
 
Baiskeli hazitakiwi mjini. Kundesha baisketi mjini ni sawa na kuvaa kandambili ofisini.
 
Back
Top Bottom