Mpaka lini sisi tutaendelea kuitwa masikini? Huu umasikini tunaoitwa nao kila leo, sababu yake ni ipi kama sio hii ya wakubwa kuiba mapesa yetu? Ni kweli kabisa sisi ni masikini au ni upumbavu wetu?
Umasikini upi tulionao sisi ili hali robo nzima ya bajeti yetu, inaishia mifukoni mwa viongozi? Unajua inauma eeh? Pale unapolipa kodi tena kwa vitisho na wakati mwingine unaletewa na maasikari ili tu ulipe kodi! Unalipa na mafaini kibao, unaendelea kudunduliza tena mara ghafula tena, kodi unaodaiwa, unapaswa kulipa!
Inapotokea mambo mabaya kabisa kwa serikali unayopaswa kuitii kwakulipa kodi ili iturahisishie huduma kwa kutusogezea karibu, unaambiwa mabilioni ya kodi hizi zimekwapuliwa na wahusika kuishia kutolewa kwenye nyadhifa zao bila hatua nyinginezo za kuwalazimisha kurudisha pesa hizi! Inauma, inakera! Inatia uchungu na kuhudhunisha sana, pia inakatisha tamaa sana kwa walipa kodi waaminifu na wenye mapenzi na nchi!
Kwa namna hii, wananchi yatubidi kuonyesha hisia zetu bila kujali tofauti ya vyama vyetu!
Hawa wakurugenzi, madiwani na wengine ambao ni wasimamizi wa kodi zetu, hivi tuwafanyeje sisi? Tuwatafune? Tuwameze? Au tudili nao kwa namna gani nzuri ili wawe mfano kwa watakaofyata?
Ikiwezekana sasa, wananchi wote, mikoa yote tuandamane kupinga ulaji wa kodi zetu hizi
😎😎😎
Mh Raisi! Wewe usipate kazi kubwa, onyesha udikiteta kiduchu tu sisi huku tuwakanyage!