Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Moja ya mambo ambayo yanaturudisha nyuma ni pamoja na hiki kitengo kinachoitwa cha upelelezi ambacho hadi sasa ni sehemu ya Jeshi la Polisi.

Na mara nyingine unakuta kuna tukio ambalo Polisi wanahusika na kitengo kinatakiwa kufanya upelelezi. Nadhani ni wakati sasa kukiondoa iwe taasisi inayojitegemea kama zilivyo taasisi kama hizi nchi nyingine.

Ina maana hata Rwanda wanatuzidi kufikiri vizuri. Rwanda mwaka 2018 wamekiondoa kitengo hicho Polisi na kuunda taasisi mpya inayo itwa RIB (Rwanda Investigation Bureau).

Nadhani Magufuli na Baraza lake wanaweza, jambo hili litakuwa muarobaini wa kesi nyingi ambazo zinawatesa wananchi kwa kusubiria upelelezi.

Tanzania Bureau of Investigation.

Soma pia: Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi
 
Unaaminisha nini unaposema DPP Ni execution...?

Mkurugenzi wa mashitaka mwenye mamlaka ya kuipeleka kesi mahakamani au la, huyu angekua mtu sawia ili anapoamua kupeleka kwa pilato faili linakua limeshiba.
Anaweza asifanye upelelezi wa uhakika kwa sababu dpp kazi yake ina siasa kidogo.

Epelelezi unatakiwa ubakie kama taaluma na utalaam.
 
Nchi nyingi zimesha ondokana na upelelezi kufanywa na jeshi la polisi. Kwa dunia ya sasa lazima twende haraka na kwa uhakika.
20191022_062838.jpeg
 
Moja ya mambo ambayo yanaturudisha nyuma ni pamoja na hiki kitengo kinacho itwa cha upelelezi ambacho hadi sasa ni sehemu ya jeshi la polisi.

Na mara ngingine unakuta kuna tukio ambalo polisi wanahusika na kitengo kinatakiwa kufanya upelelezi.

Nadhani ni wakati sasa kukiondoa iwe taasisi inyo jitegemea kama zilivyo taasisi kama hizi nchi nyingine

Ina maana hata Rwanda wanatuzidi kufikiri vizuri.

Rwanda mwaka 2018 wamekiondoa kitengo hicho polisi na kuunda taasisi mpya inayo itwa RIB.

Nadhani Magufuli na baraza lake wanaweza na jambo hili litakua muarobaini wa kesi nyingi ambazo zinawatesa wananchi kwa kusubiria upelelezi.

Tanzania Bureau of Investigation.
Ushauri mzuri sana
 
Vilevile ile bureau ikianzishwa itapunguza urasimu na rushwa kwa kiasi kikubwa ndani ya jeshi la polisi
 
Moja ya mambo ambayo yanaturudisha nyuma ni pamoja na hiki kitengo kinacho itwa cha upelelezi ambacho hadi sasa ni sehemu ya jeshi la polisi.

Na mara ngingine unakuta kuna tukio ambalo polisi wanahusika na kitengo kinatakiwa kufanya upelelezi.

Nadhani ni wakati sasa kukiondoa iwe taasisi inyo jitegemea kama zilivyo taasisi kama hizi nchi nyingine

Ina maana hata Rwanda wanatuzidi kufikiri vizuri.

Rwanda mwaka 2018 wamekiondoa kitengo hicho polisi na kuunda taasisi mpya inayo itwa RIB.

Nadhani Magufuli na baraza lake wanaweza na jambo hili litakua muarobaini wa kesi nyingi ambazo zinawatesa wananchi kwa kusubiria upelelezi.

Tanzania Bureau of Investigation.
Hiki kitu nikishakiwaza miaka mingi.ila sikua na uhakika kama kuna baadhi ya nchi imewezekana kukitenganisha na polisi.
Maana kuna kesi nyingi ambazo polisi wao binafsi ni watuhumiwa sasa hapo unafikiri itakuaje? Kosa lumetendwa na polisi, wapelelezi ni polisi,waendesha mashtaka sijui ni polis....kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom