Rwanda: Msanii maarufu wa nyimbo za injili Kizito Mihigo akutwa amejinyonga ndani ya Kituo cha Polisi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581933203996.png

Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo amekutwa amejinyonga kwenye Kituo cha Polisi.

Kwa mujibu wa tangazo la Polisi, maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alichokuwa anazuiliwa kwenye Kituo cha Polisi mtaa wa Remera, mjini Kigali.

Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho Polisi ilisema alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Rwanda.

Alikuwa ameanza kufanyiwa uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkamata.

Mwaka 2018 aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua Rais na kuhamasisha raia kupinga Serikali.

BBC Swahili

====

Rwanda’s artist Kizito Mihigo was found dead in a police cell from Remera police station, a communique from Rwanda National Police reads.

The vocal artists, Kizito, 38, was arrested last week while attempting to illegally cross to Burundi, according to Rwanda Investigation Bureau(RIB).

The police communique reads in part :” he has been in the police cell for the last three days as RIB accused him of attempting to cross the border illegally and corruption.”

The communique further reads that on February 15 and 16, Kizito was visited by his family members and his lawyer.

“Investigation is underway to establish reasons that pushed him to kill himself,” police communique reads.

Kizito Mihigo was first arrested in 2014 on several allegations including joining the Rwanda National Congress (RNC), a terrorist outfit whose leaders are based in South Africa seek to destabilise Rwanda’s security. He was found guilty and sentenced to 10 years in prison.

In September 2018, the head of State commuted his prison sentence among 2,140 convicts found eligible under relevant provisions of law.
 
17 Februari 2020

Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili,Kizito Mihigo ''amejinyonga'' Polisi wa Rwanda wanasema.

Kwa mjibu wa tangazo la polisi maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alimokuwa anazuiliwa kwenye kituo cha polisi mtaa wa Remera,mjini Kigali.

Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho polisi ilisema alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Rwanda.

Alikuwa ameanza kufanyiwa uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkata.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.
 
Back
Top Bottom