Kwanini kinaitwa Polisi kitengo cha upelelezi badala ya Polisi kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai?

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,976
2,000
Kwenye jeshi la polisi kuna kitengo kinaitwa criminal investigation department kwa kimombo lakini kwa kiswahili wanaita kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai.

Swali langu ni kwa nini tafsiri ya investigation inakua upelelezi badala ya uchunguzi? Neno upelelezi limekaa kishambega, kiumbea umbea hivi ila investigation ama uchunguzi imekaa kitaalamu, iko facts based, kwamba unachunguza, unatafta kuujua ukweli na sio kupeleleza.

Kama investigation ni upelelezi, je spying iitweje?

Nashauri kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai kibadilishe jina kiitwe kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai. Kuchunguza maana yake ni kutaka kuujua ukweli ila kupeleleza kunaleta ukakasi.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,873
2,000
... umbea ni sehemu muhimu sana ya uchunguzi au upelelezi, vyovyote utakavyopenda kuuita. Kwa taarifa yako, wachunguzi makini ni wambea balaa; wengine wana "sahada za umbea" na ni wambea balaa. So, in short, usi-underestimate umbea katika medani za kipelelezi/kiuchunguzi. Yangu ni hayo tu, mengine nawaachia wataalamu.
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,251
2,000
... umbea ni sehemu muhimu sana ya uchunguzi au upelelezi, vyovyote utakavyopenda kuuita. Kwa taarifa yako, wachunguzi makini ni wambea balaa; wengine wana "sahada za umbea" na ni wambea balaa. So, in short, usi-underestimate umbea katika medani za kipelelezi/kiuchunguzi. Yangu ni hayo tu, mengine nawaachia wataalamu.
Nakubaliana kabisa na wewe. Nadhani huwa wanatakiwa watu ambao wanaweza wakapata taarifa na kuzifikisha kule zinakohitajika, ili mradi tu taarifa hizo wawe wamezipata kwa njia sahihi zinazokubalika na mamlaka zenye kuhitaji taarifa hizo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom