Pendekezo: John Heche amrithi Zitto Kabwe


Hapa tungeanza kulinganisha kati ya Mbowe vs Heche halafu wengine wakafuatia. Pili, tutazame mapato na matumizi ya chama. Tatu, uchaguzi ndani ya chama uwe huru na wa haki. CHADEMA ni zaidi ya uijuavyo.
 
Watu wa kaskazini hamumtaki zito kwani mnajua anakubalika katika urais na ndio maana hamkosi sababu kila kukicha. Hivi umaarufu wa zito unaweza ukafananisha na nani hapo chadema
Kumbe Heche nae ni Mchaga!!!!!!!! CDM bwana, Nami Suggestion nikianza mambo nitaambiwa Mchaga kumbe mm Muha wa Kibondo
 

Ok mkuu nimeipenda CV yako kama mwandishi mwenye weledi mkubwa.

Sasa mkuu labda nisaidie hapa kwanini habari za Heche dhidi ya Zitto zinakuwa nyingi?
Kwanini ni Heche vs Zitto na si heche vs wengine au Zitto vs wengine?
Just asking to know mkuu Candid Scope
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, binafsi nakusoma na najaribu sana kukuelewa. Ni kweli kuna logic kwenye hiki unachokizungumza, ila wasiwasi wangu ni namna unavyoonekana kumshambulia moja kwa moja bw Zitto. Nijuavyo mimi kuna mtu huwa ana jukumu la kufanya katika chama. Binafsi sijawahi kupata uthibitisho wa wa wazi wa MAKOSA ya bw Zitto. Na nimekuwa mfuatiliaji kwa kiwango cha kuridhsha wa siasa za Tanzania kwa sababu naamini kwa Tanzania, siasa imebeba msingi wa maendeleo. Wataalamu hawana tena thamani mpaka wanasiasa wawahurumie. Bahati mbaya tumekuwa na wanasiasa wabovu ajabu (ccm) ambao ndo wana jukumu la kututenganezea mazingira mazuri ya sisi watanzania kujiendeleza, matokeo yake hatupigi hatua za maendeleo zenye kuwiana na rasilimali tulizonazo.
Nikirejea kwenye mada yako hapo juu, napata shida kidogo kwa namna ulivyomshambulia bw Zitto, labda nisaidie hili swali, ni nini mantik ya wewe kuwapambanisha Bw Heche v/s Bw Zitto huku ukionesha kabisa kuwa tayari umeshamponda Bw Zitto??? kwa nini usiwapambanishe wanachama wengine wa CDM???
Bw Zitto ana dhambi gani yenye uthibitisho ambayo mimi siifahamu??? nitasikitika sana kama yatakuwa majungu, kama unaweza nijibu hata kwa kuni-pm ili nami nimfahamu Bw Zitto pengine zaidi ya nimjuavyo kwa sasa. nakusubiri mkuu.
 
Watu wa kaskazini hamumtaki zito kwani mnajua anakubalika katika urais na ndio maana hamkosi sababu kila kukicha. Hivi umaarufu wa zito unaweza ukafananisha na nani hapo chadema


Heche nae ni wa kaskazini?......."ficha upumbavu wako , usifiche hekima yako" source: Invisible
 
Last edited by a moderator:

Zito tumetoka naye mbali, tunampenda, haya tunayoandika kuhusu kasoro zake tunataka ajitahidi kuwa na weledi wa kujirekebisha ili awepo kwenye mstari ambao wengi tunaona amekuwa wakati mwingine nje kidogo.

Kukosoa ni njia bora ya kumjenga mtu, lakini kushabikia tu hata anapofanya isivyo ni kumharibu, ndio tabia ambazo wengi tunazo za ushabiki zaidi bila ukweli ambao unaweza kumjenga mtu.

Zitto ni kijana jasiri katika mambo kadhaa, ila ana kazi ya ziada ya upande mwingine kujijenga, maana uongozi wa nchi si kama ukilanja wa darasani.
 

Napenda umakini katika kujadili na kukosoa kwa nia ya kuwajenga watu. Tanzania tumekuwa na kawaida ya kushabikia viongozi bila kuwakosoa wanapofanya ovyoo na matokea baadaye tunajutia yanayojilia. Uongozi katika siasa si vema kushabikia kama timu ya simba na yanga, la sivyo yanayotukuta kama tungekuwa na uchambuzi wa kina na kujaribu kuona nani wa kweli yasingetukuta, ila basi sasa hakuna jinsi maji ukishayavulia nguo .......

Kama nilivyosema hapo awali, Zitto ni mpambanaji mzuri mjengoni kwenye mhimili wa bunge. Lakini chamani katika jitihada za kujenga chama anafanya kwa ujanja ujanja pale pasipo na dalili ya kupata matatizo anajaribu kuwepo. Lakini pale ambapo kunaweza kutokea matatizo Zitto hajawahi kujiingiza, hili ni tatizo na ni alama mbaya katika uongozi kwani ni dalili ya woga, kutojituma na kupenda kuelekea kwenye tambalare zaidi kuliko kupambana na magumu yanapotokea, kama nimekosea naomba nisahihishe. Zitto anakuwa mpambanaji mzuri pale sheria inapomlinda asidhurike au kuwajibishwa kisheria, ndivyo mfumo wa bungeni uliyvo tofauti na shguhuli za kujenga chama vijijini kupambana na mabomu ya polisi.

Zitto nilipoweka uzi mmoja hapa alijibu kupitia Twiter kuwa wanaopata matatizo ni kwa sababu ya kujitakia, ina maana kwa tamko hilo hayuko tayari kujituma palipo na ugumu katika kukijenga chama.
Zitto anaonekana kuwa busy zaidi na shughuli za Bunge kuliko shughuli za Chama, tungetazamia kama Kaimu Katibu Mkuu anakuwa na muda mwingi pia katika kukijenga chama, kwani ningetegemea Katibu mkuu angekuwa na mengi ofisini wakati fulani na kaimu wake kuingia vijijini kukijenga chama pamoja na makamanda wengine kwa kuwekeana zamu.

Weledi wa kupigania Urasi si kitu cha kawaida Chadema, lakini kama anafaa sina shaka Chama kitaridhia agombee, ila ana kazi ya ziada katika kuwa na ustahimilivu, kujituma katika mengi, maana kazi ya rais si kufuatilia wizara ya fedha na kashfa serikalini tu.

Kikwete alikuwa mzuri sana kama anavyofanya Zitto siku hizi, kama unaweza kuwa na kumbukumbu jinsi alivyomtoa kamasi hayati aliyefia Ulaya ambaye alikuwa waziri wa fedha wa kutokea kule Kilwa. Kitendo kile wengi tulimwona Kikwete ataweza kuwaadabisha na kuwawajibisha wazembe wengi serikalini akishika madaraka, kumbe tatizo tuliangalia kitu kimoja ambacho kikwete alikuwa anapigania na yule alionekana kuwa kukwazo cha yeye kupanda alipo.

Katika kujibu hoja yangu,
Wamunzengo ulitakiwa uweke hoja zako hapa za kutetea utendaji wa Zitto, kwani hujaniletea hoja ambazo zinaleta uzito wa hoja yako ya kupinga hoja zangu. Huo ndio ungekuwa uchambuzi tunaotaka kwa weledi wa habari.

Naamini una uwezo wa kujenga hoja, nahitaji hoja hizo ambazo tutazijadili, na ndiyo ninayotaka ili kumjenga Kamanda Zitto. Tunajadili hoja, hatumchukii mtu kwa kujadili uwezo wake na udhaifu wake, bali tunampenda kwa kujaribu kumwezesha kwa kuonyesha kasoro na madhaifu ambayo yanaonekana ili ayafanyie kazi awe kiongozi wa kiwango tunachotazamia wengi.

Kwa hiyo ndugu yangu, usiwe na mtazamo hasi juu ya uchambuzi wangu, hapa tunajitahidi kuwajenga viongozi hawa wa kesho kwa njia mbalimbali, na tuonapo kasoro fulani zinajitokeza au udhaifu wa kibinadamu na wa kizembe tunahitaji kuwaweka kiti moto ili wafikie weledi tunaotazamia. Vinginevyo kushabikia tu fulani anafaa bila kumjenga tunafanya yaleyale ambayo tunajutia huku sisiem kwa vile tumezoea kujenga tabia ya kulindana kiushabiki bila kujali mambo ya msingi katika uongizo hadi mambo yao kama yalivyo kila mmoja sasa anaona anaweza kuingia Ikulu, kwa nini kama afanyavyo fulani mboma mimi naweza kufanya vizuri zaidi.
 

Mkuu Hongera,upo juu.Appreciated!
 
Uchambuzi wako umetulia sana.Big up!
 
Mkuu Candid Scope, nahisi wote tupo kwenye muelekeo sawa, ila pengine hisia na hasira zetu za kudhulumiwa na ccm ndo zinatufanya tuogopane. Binafsi napenda kumtendea haki mtu, bw Zitto ana mazuri yake mengi tu hasa kazi nzuri anayoifanya pale bungeni. Kwa bahati mbaya labda kwa upofu wangu siyajui mabaya ya dhahiri ya bw Zitto. Ukifuatilia siasa za hivi karibuni za vijana majasiri hapa Tanzania huwezi ukampuuza bw Zitto. Na kwa wakati wake, ukumbi mzuri uliotoa fursa ya mtu kujijenga na kukijenga chama chake kisiasa ilikuwa ni bungeni. Na ni wakati huo bw. Zitto aliposimama kidete kupingana na maslahi haranu ya watawala mafisadi wa ccm. Kwa hili huwezi ukapuuza kuwa bw Zitto hakuhatarisha maisha yake, na ndo maana kuna kipindi hata ile ajari ya Mudhihiri Mudhihiri kule kusini ilihusishwa na njama za kumfanyia kitu mbaya bw Zitto (tetesi). Au labda kwako wewe mtu kuhatarisha maisha yake ni mpaka aende kwenye eneo ambalo kuna uwezekanao wa kupigwa mabomu tu??? nijuavyo mimi namna yoyote ile ambayo mtu anapinga kihalali maslahi haramu ya watawala mafisadi/madhalimu huwa ni kuhatarisha maisha, NA HII ZITTO KAIFANYA SANA. AU WEWE HUJUI???

Nionavyo mimi, huwezi kubeza mchango wa bw Zitto kwenye siasa za mabadiliko Tanzania, mpe haki yake. Lakini huwezi ukapuuza kazi anayofanya
bw Heche kwa sasa, ni kazi nzuri ya kuungwa mkono. Hivyo basi, naomba tuthamini michango yao wote, hatuna haja ya kumponda mmoja wao kiupogoupogo. Tuendelee kuelimishana mkuu, ila lengo letu liendelee kuwa kuhakikisha tunauondoa huu utawala dhalimu wa ccm.
 
John Heche bado amejichimbia vijijini akikijenga chama.
 
Mwakani mkwe wa mbowe hatasikilizwa tena mbowe na slaa hana chake ndani ya chadema lazima tubadilishe ukanda na ukabila maana tumechoka na huo ubaguzi yaani mpaka madeleva wa makao makuu ni wachaga watupu hii haikubaliki hata siku moja.

WEWA acha uongo madereva gani wachaga. Yule ABBAS uliyekuendesha kpndi unajipendekeza na ANTONI KOMU ni MCHAGA? mbona hausemi Tulikupa sh 2M na usafiri ukajijenge jimboni wakati wa chaguzi ndogo za vijiji MBOZI ulikuwa MCHAGA?
 
WEWA acha uongo madereva gani wachaga. Yule ABBAS uliyekuendesha kpndi unajipendekeza na ANTONI KOMU ni MCHAGA? mbona hausemi Tulikupa sh 2M na usafiri ukajijenge jimboni wakati wa chaguzi ndogo za vijiji MBOZI ulikuwa MCHAGA?

Mkuu achana na huyo mjinga ni sawa na pepo mchafu.
 
Ccm wasitegemee kuivuruga cdm-zitto
 
Heche hana uwezo wa kuvaa mikoba ya zito km bavicha imemshinda imekosa mwelekeo viongozi wake wamekuwa wanatupiana maneno ya kutuhumiana hadharani, hatuoni juhudi zozote zinazofanywa na bavicha kukiendeleza chama lakini leo anakurupuka mtu hapa na kutaka kumlinganisha raisi ajaye na heche huyo mtu yupo wrong. Km hufahamu zito ndo msigi wa cdm bila zito mafanijio uyaonayo ya cdm yasingekuwepo
 
Tuko pamoja mkuu.

Kila kukicha Zito, Cdm tunaowabunge wengi ambao majukumu yao hayaeleweki ndani ya chama, wala kwenye M4C hawashiriki, mfano Mbunge wa Rombo, Mbunge wa Mpanda, Mbunge wa Mbozi, Mmbunge wa Karutu, Mbunge wa Ukerewe na jimbo jingine la mwanza mjini na wabunge wa vitu maalumu mfano dada yake ya Mh Lisu. Lakini kelele za vipandikizi vya CCM kila siku ni kuhoji Zitto. Zitto ni naibu km hivyo katibu kama yupo kwa nini afanye kazi za katibu, yeye ni msaidizi tu iwapo katibu kasafiri au anamajukumu mengine ndio anaweza kumkaimisha Zito. Mfano umeshaumuona naibu Katibu Mkuu wa CCM bara katika harakati za kila siku za Chama ?. Tuelewe mipaka ya kiutendaji katika uongozi wa vyama vyetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…