Pendekezo: ILi kumuezi dada Regia kiti chake apewe pacha wake

3squere

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
925
Reaction score
181
japo ni mapema sana lakini kabla ya mawazo kufika mbali ingekuwa busara sana jf na cdm kumpa nafasi ya kamanda wetu rejia mtema mdogo wake hili iwe ni moja ya kumuezi dada yetu alafu hikumbukwe kwamba uyo pacha wake alikuwa katibu wake na kwa ufupi alikuwa kamanda kikosi cha nyuma na ni mpanga mashambulizi.
Amen
 
ni wazo zuri bt nadhani tuache system ifanye mchakato na waje na pendekezo la mwisho.
 
Kama taratibu zikfuatwa na dada yake na marehemu akapata nafasi hiyo si jambo baya lkn kikitumika kigezo kimoja cha yeye kuwa dada wa marehemu mbunge hapo siungi mkono.
 
Kwa mtazamo huohuo unaonaje tukiomba Madaraka au Makongoro Nyerere awe rais ili kumuenzi hayati Baba wa Taifa? Au Katiba mpya iseme kabisa kuwa kiongozi akifa basi ndugu yake wa karibu au mtoto achukue nafasi yake ili kumuenzi marehemu?.
 
ha! ha! kweli we ni tata si tutu!
 
atajisikia uchungu sana kila anaposimama kuchangia point atamkumbuka pacha wake badala ya furaha itakuwa uchungu mi namshauri wala asiingie knye siasa bora awe mwanaharakati
 
japo ni mapema sana lakini kabla ya mawazo kufika mbali ingekuwa busara sana jf na cdm kumpa nafasi ya kamanda wetu rejia mtema mdogo wake hili iwe ni moja ya kumuezi dada yetu alafu hikumbukwe kwamba uyo pacha wake alikuwa katibu wake na kwa ufupi alikuwa kamanda kikosi cha nyuma na ni mpanga mashambulizi.
Amen

tehetehe hiyo siyo rahisi hivyo
kuna taratibu za kuwapata viti maalum na hata hivyo orodha yao ipo kwenye tume (NEC) tayari hivyo nadhani mbunge atakayefuata atakuwa anajulikana maana walipaswa kuwapanga kwa priority.
si mnakumbuka kifo cha Salome Mbatia na Amina Chifupa? kulikuwa na majina tayari kwenye tume ambako jina la anayefuatia linakuwa linajulikana ndiyo wakaingia akina Mh Mchungaji Rwakatare na nadhani na Dr. Ishengoma ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa
 
The Kingdom of CHADEMA, Slaa atamrithisha mtoto wake pia?
 
Si kila mtu anaweza kuwa mwanasiasa hata kama ni pacha wake, hawawezi kufanana kila kitu
 
Mbona status yake kwenye facebook inaonyesha ni Mwana CCM? Au apewe bila kujali chama anachotoka? Hata hivyo sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo. Kumuenzi ni kuendeleza yale yote mema aliyoanzisha na kupigania marehemu. Kuhusu nani atachukua nafasi nadhani ile orodha ya NEC inahusika, aliyefuata baada ya Sabrina Sungura au Anna Stela Mallac kama sikosei ndie anayestahili. Kinyume na hapo lazima tutasikia vurugu tu
 
Hivi na wewe ni great thinker kwa mawazo kama hayo duh!
 
Mnaonaje kama Ridhiwani akapewa Urais ili kumuenzi baba yake?
Kila chama ina katiba na taratibu zake za kumpata mtu atakayeziba pengo la mtu.
 
japo ni mapema sana lakini kabla ya mawazo kufika mbali ingekuwa busara sana jf na cdm kumpa nafasi ya kamanda wetu rejia mtema mdogo wake hili iwe ni moja ya kumuezi dada yetu alafu hikumbukwe kwamba uyo pacha wake alikuwa katibu wake na kwa ufupi alikuwa kamanda kikosi cha nyuma na ni mpanga mashambulizi.
Amen

Kwani hicho kiti ni cha Kifalme? CDM wana system waliojiwekea. Nafikiri kwenye list kuna mtu aliyekuwa anafuata kabla ya RED line. Kwa hiyo haki itendeke.
 
Vigezo vya kutosha kama anacho mie pia naunga mkono kwa asilimia nyingi.
 
japo ni mapema sana lakini kabla ya mawazo kufika mbali ingekuwa busara sana jf na cdm kumpa nafasi ya kamanda wetu rejia mtema mdogo wake hili iwe ni moja ya kumuezi dada yetu alafu hikumbukwe kwamba uyo pacha wake alikuwa katibu wake na kwa ufupi alikuwa kamanda kikosi cha nyuma na ni mpanga mashambulizi.
Amen
Sasa huo ni mfumo wa uchifu nadhani Tanzania tumeufuta kwanini apewe pacha wake je kama yeye ni mwana CCM au uwezo wake ni mdogo napo tumpe tu sababu ni pacha wa marehemu?tukumbuke hapa duniani sote tunapita tu kwa hiyo kila mtu awe nafasi kutokana na uwezo wake na si kwa kuangali undungu,nasaba na mambo mengine.Tunategemea Chadema iwe msitari wa mbele kuyapinga haya mambo ya kubebana eti kwa sababu ya kuenzi,tutaenzi wangapi,au mnataka tuwe kama Kenya ,India ,pakistani ambako vyeo huwa kama ni haki ya urithi.Acheni kuleta maudhi na tafakuri zisizo na mshiko kwa wakati huu wa majonzi
 
Mbona status yake kwenye facebook inaonyesha ni Mwana CCM? Au apewe bila kujali chama anachotoka? Hata hivyo sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo. Kumuenzi ni kuendeleza yale yote mema aliyoanzisha na kupigania marehemu. Kuhusu nani atachukua nafasi nadhani ile orodha ya NEC inahusika, aliyefuata baada ya Sabrina Sungura au Anna Stela Mallac kama sikosei ndie anayestahili. Kinyume na hapo lazima tutasikia vurugu tu

Kama si lazima atokee morogoro wanaweza kufuata series
 
Back
Top Bottom