Pendekezo: Edward Lowassa awe Mwenyekiti wa CHADEMA

Pendekezo: Edward Lowassa awe Mwenyekiti wa CHADEMA

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,351
"Leo wameapisha Rais Mpya, Rais wao, Rais wa NEC, Rais ambaye anatokana na majina ya mfukoni ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi." Naweza nisiwe sahihi sana, lakini haya walau yanasadifu kwa kiasi fulani mawazo ya washabiki wa UKAWA na wenye mapenzi mema na umoja huo, ambao wanaonesha kutoridhika na uamuzi wa Watanzania waliomweka madarakani Rais John Magufuli.

Ukweli ni kuwa Chadema wameshiriki sehemu kubwa ya ukombozi wa kifikra wa taifa hili, ukombozi wa kisiasa wa baadhi ya majimbo na kata, lakini pia ukombozi wa Chama cha Mapinduzi hadi kikaona umuhimu wa kuwa na mgombea Urais muadilifu, mchapa kazi na mfuatiliaji.

Chadema hawahawa wakakubali bendera yao ipeperushwe na Edward Lowassa, mtu kutoka chama cha mapinduzi ambaye visa na visakale vyake vimeshasemwa sana tangu zamani, tangu zama za Mwalimu Nyerere, sina haja ya kuvirudia hapa, sote tunavijua.

Tukirejea kwenye upande mzuri, Lowassa ni alama ya mabadiliko, na ndiye aliyesababisha Watanzania wengi wazungushe mikono kwa bidii, wakitarajia kuikomboa nchi kutoka kwa Mkoloni mweusi, CCM, huku nae Bwana Mkubwa akipata nafasi ya kutimiza ndoto zake za kuwa Rais.

Kwa kipindi cha miezi kadhaa tangu jamaa ahamie Chadema, tumejua sifa zake zote, huku mashabiki, wanachama na wadau wa CCM nao wakijitahidi kumvua nguo, wakiwemo wale waliokuwa washabiki wake wa kutupwa.

Siko katika nafasi ya kusema kama wanaomshabikia wako sawa au wanakosea, lakini tuheshimu mawazo yao.
Lowassa wanampenda na wanamuamini, wampe uongozi ndani ya chama chao, na mimi nasema ni wakati sasa kwa wale wenye mapenzi mema na chama na wenye imani na Lowassa kushinikiza ndani ya chama Mzee apewe, au wampe uenyekiti wa chama.

Mwenyekiti anayemaliza muda wake, (kama wazo hili litapata mashiko) amekuwa msaada kwa chama na taifa, lakini haitapandeza kama tutakabidhi chama kwa mtu tunayemuamini, mwenye maamuzi magumu, alama ya mabadiliko, mwanasiasa anayependwa kuliko wote kwa sasa, mwenye nyota?

Najua fika kuwa Mzee alishasema ataenda kuchunga ng'ombe, lakini ni wakati muafaka wa kumbembeleza, kumuoshe tena gari, kumdekia barabara, awe mwenyekiti wa Chama chenu, awaonjeshe mabadiliko katika ngazi ya chama ili sote tuyashuhudie na mwaka 2020 tuseme kweli tulikosea kumchagua mpiga pushapu, kiongozi wa mfano si huyu?

Baada ya kuukosa Urais na kususa matokeo, Slaa aliendelea kujenga chama kwa moyo wake wote, nchi nzima, kwa nguvu zote, na matokeo yake walau nchi iwaponyoke nyamaume wa Chama cha Mapinduzi, Fisiem, kama mnavyowaita.

Nasubiri makamanda mpeane mwongozo, kwa maslahi mapana ya Taifa!
#KaziImeanza
 
Mzabinazabina mchokochoko nafikinafiki chochezi hajifichi hata aandike nini
 
Zanzibar hawana rais wa Zanzibar wala rais anaewatumikia katika muungano !
kura walizopiga octoba 25 zote zilikua batili na matokeo yakafutwa kama mtoto anavyofutwa uji aliojipaka..kirahiiiiiiiiisi !
 
Nadhani ni sawa.

Kwanza chama ni cha kwake. Tunafahamu alichokifanya hata akaingia chamani na kuwa mgombea wa urais. Ana haki ya kuwa kiongozi wa juu kwenye chama chake.

Ila kwa hakika wana Chadema asili wataanzisha chama chao.
 
Kwanza huielewi CDM.
Huyo kiongozi anayemaliza muda wake ni yupi?
Viongozi wa CDM huchaguliwa kwa mujibu wa katiba ya CDM.
 
Lowasa alisema kuwa anaenda kuchunga ng'ombe kwao Monduli. Kiu yake ilikuwa ni kuutaka urais tu
 
Akiwa mwenyekiti watakuwa mabumunda, hawajawasoma watanzania ndo itakuwa maana yake. Yaani aliyewageuza mawazo watanzania wasiichague chadema/ukawa ndo sasa awe mwenyekiti?
Watakuwa wanajichimbia shimo zaidi, MNYIKA ANATOSHA kuwa mwenyekiti, kijana, damu inachemka na hajaonesha ukigeugeu wa viongozi waandamizi wa ukawa.
 
Kafie mbele kule kilaza mkubwa wewe
 
Wewewe, na ruzuku zote zile Mbowe aaishie uenyekiti? Over his dead body. Walishamalizana na Lowassa baada ya kumruhusu agombee urais.
 
Wafuasi wa Mbowe mnasikitisha sana, kama mlikuwa tayari kumpa Lowassa nchi mnashindwa nini kumpa Uenyekiti wa chama ili akijenge kwa maandalizi ya 2020?

Kama mnaona hafai kuwa Mwenyekiti wa chama, kwa nini mlitaka tumpe nchi mtu ambaye hammuamini Kumpa chama.

Ili kuonyesha kuwa Chadema walikuwa sahihi na walimwamini Lowassa ni vema wampe Kiti cha chama!
 
Nadhani ni sawa.

Kwanza chama ni cha kwake. Tunafahamu alichokifanya hata akaingia chamani na kuwa mgombea wa urais. Ana haki ya kuwa kiongozi wa juu kwenye chama chake.

Ila kwa hakika wana Chadema asili wataanzisha chama chao.

Akili ya kuambiwa changanya na yako ila kwa kua ni taahira huwez!!!! Mbowe na Slaa ndo waliomleta Lowassa CDM! Hao chadema asilia waanzishe tu hatuwataki... Chadema asilia wawe wao??? Slaa mwenyw ni mamluki...na kina mtei uwaite kina nani ssa??? ACHA WASEPE TU NA MIHOGO WAO....ABIRIA AKISHUKA HUPANDA MWINGINE NA SAFAR HUENDELEA!!! Huyo slaa angekua ni kamanda wa kweli angekituliza tu na co kuinad ccm!!!! Mbona Lipumba alikaa kimya???? JAMAN CHADEMA MAMLUK MTOKE TU...chadema asilia ninaowajua mm hawakukimbia tatizo......Hongera Mbowe umepruv kua Mwanaume, una msimamo na na sio mnafik koz kwa usaliti wa kina lipumba,slaa na nccr na mikasa aliyokutana nayo EDDO ANGEKUA MTU MWINGINE ANGEMTELEKEZA ila uilicmama na hukuyumbushwa na mtu....Umeweka ubinadamu MBELE NA CIO SIASA HONGERA KWA HILO!!!! Koz at the end of the day ss wote ni binadam....SIASA ICTUFANYE KUA MBWA KOKO!!!! MBOWE NI MWANAUME WA NGUVU...WENYE HULKA ZA KIKE ZA KIMBEA NA KINAFIKI HUTUWATAKI...Pongezi kwako Mbatia tunataka watu aina yako msiobabaishwa na mtu.....
 
No. Awe mwenyekiti wa baraza la wadhamini, ana hekima sana. Uenyekiti ni mikikimikiki sana.
 
Back
Top Bottom