Pendekezo: Dkt Kitila Mkumbo awe mrithi wa Dkt Slaa

Pendekezo: Dkt Kitila Mkumbo awe mrithi wa Dkt Slaa

Status
Not open for further replies.

Kimboka

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
353
Reaction score
163
Katika pitapita zangu mikoani na kuzungumza na makamanda wanaonesha wazi kuwa ni muda mwafaka kwa Dr Kitila kushika nafasi ya Dkt Slaa ktk nafasi ya Katibu Mkuu,

Sifa za Kitila Mkumbo hazina pingamizi kwa yeyote anaetaka mabadiliko;Kitila ni msomi anaetambua umuhimu wa mabadiliko,Hana makundi ndani ya chama,Kasaidia kutatua mizozo mingi ndani ya chama,Ni msema kweli daima,

Tukumbuke kuwa kitila amelimaliza kisiasa li Gaidi Mwigulu Nchemba uko iramba mpaka sasa halijafika iramba kwa hofu ya kuzomewa baada ya ziara nzito ya kitila mkumbo,Jesca kishoa na David Djumbe.

Tunatambua mchango mkubwa wa Dr Slaa ila kwa sasa tunahitaji mtu atakaepanga mipingo mikakati itakayotekelezeka bila kukigawa chama ktk makundi ili tuweze kuifikia salama nchi ya maziwa na asali.

VIVA MAKAMANDA, VIVA MABADILIKO.
Utaratibu wa kumpata Katibu Mkuu wa CDM unajulikana na hii ya kupigiana kampeni kwenye mitandao sio mojawapo.

Mnaleta mijadala ambayo haipaswi kuwepo na kusababisha mitafaruku isiyo na maana na kupoteza muda wa kuidhoofisha CCM.

Nina kazi kubwa ya kuelimisha vijana wetu katika vyuo vikuu na ninaifurahia kazi hii. Mchango mdogo ninaotoa kwa CDM kwa nafasi niliyo nayo sasa unatosha na ninaridhika.
 
Credibility ya Dr.Kitila haina ubishi. Binafsi naunga mkono hoja hii japokuwa kuna wengine watakuja na hoja ya uzoefu lkn kimsingi Dr.Kitila ameongoza ldara nyeti ya Saikolojia pale UDSM kwa mafanikio makubwa. Kwakua Ukatibu ni utendaji zaidi, sina shaka jukumu hilo atalimudu vema.

Naunga mkono hoja!
 
Dah...!! ukiona uko vitani na adui yako afu adui yako anakusifia kwa hatua unazochukua think twice..!!
 
Chadema wanasema katibu ajae lazima awe mchaga la sivyo kutachimbika aisee mangiii.
 
Nakuunga mkono 100% ila tusiishie hapo tuende hadi kwenye nafasi ya Uenyekiti,Kitengo cha Habari na Kitengo cha Fedha pia.
 
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
 
Mkuu Kimboka,kwa vyovyote vile Kitila Mkumbo anao uwezo,wakati ukifika na taratibu zifuate.Pia Mwenyekiti kwa maoni yangu ni wakati ukifika angefaa sana Prof.Abdalah Jumbe Safari.Ni kikosi kikali na kizuri sana.Wacha tusubiri viti hii ya mazandiki iishe.Kila jambo kuna majira na wakati mwafaka
 
MIMI NAONA NI HERI AWE NAIBU KATIBU WA CHADEMA ILI APATE EXPOSURE KWANZA KWANI ZITO YUKO KI MASLAI ZAID, PIA ANAUKARIBU NA MAccm JAPO KWA SIRI
 
Sio Rahisi CHADEMA wampe wadhifa mkubwa hivyo Kitila Mkumbo , kuna mambo kadhaa inabidi yarekebishwe kwanza! likiwemo hili la ukabila!
 
Naunga hoja, slaa tayali tumeuona uwezo wako na inavyoonesha amefika upeo wake wa mwisho. Sasa ni muda wakufanya mabadiliko ili kukisongesha chama mbele. Kitila mkumbo anafaa nafasi ya katibu mkuu na mwenyekiti awe profesa baregu au zito, na naibu katibu mkuu awe mnyika na masuala ya propaganda na sera aachiwe tundu lissu. Ila uongozi wa sasa hauna budi kupumzika ili tuweze kusonga mbele
 
Na nafasi za Mbowe, Zitto, Mnyika???
nafasi ya Mbowe apewe zitto, na nafasi ya mnyika apewe yule mwenyekiti wa Arusha alovuliwa uongozi Mwigamba a.k.a maskini mkulima, na kamati kuu wateuliwe wale masalia waliofukuzwa uanachama, warudishwe wote kwa jina la mwenyekiti mpya zitto, nawataja kwa majina, Juliana Shonza, mtela mwapambo, david kafulila, habibu mchange mwizi wa simu, deogratius kisandu........ hii timu ikiwepo lazima ilete ushindi wa kimbunga 2015.
 
CHADEMA ina hazina kubwa sana ya wanachama wenye uwezo wa kukiongoza chama kiasi ambacho kimeonekana kuwa ni chama tishio kwa chama tawala.Tatizo ni namna ya kumpata mtu mwenye uthubutu wa kuyakataa mamilioni ya CCM ambayo imeamuwa kutumia fedha kuwanunua wapinzani wake ili iweze kuokoa utawala wake ambao umefika ukingoni.
 
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Usitoke nje ya mada,zuzu we.
 
nafasi ya Mbowe apewe zitto, na nafasi ya mnyika apewe yule mwenyekiti wa Arusha alovuliwa uongozi Mwigamba a.k.a maskini mkulima, na kamati kuu wateuliwe wale masalia waliofukuzwa uanachama, warudishwe wote kwa jina la mwenyekiti mpya zitto, nawataja kwa majina, Juliana Shonza, mtela mwapambo, david kafulila, habibu mchange mwizi wa simu, deogratius kisandu........ hii timu ikiwepo lazima ilete ushindi wa kimbunga 2015.

Tunazungumzia namna ya kukisuka kikosi kipya cha ushindi kwaajili ya 2015 general election na wewe unaanza kuleta ukilaza wako hapa..
 
Naunga mkono hoja,hasa ikizingatiwa dk slaa atagombea uraisi,na kuna uwezekano mkubwa akawa raisi.
 
Tunazungumzia namna ya kukisuka kikosi kipya cha ushindi kwaajili ya 2015 general election na wewe unaanza kuleta ukilaza wako hapa..
kwani hicho sio kikosi kazi? kwanza tangu lini mi'CCM ikapanga kikosi kazi chama cha CHADEMA?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom