"Pembe" za Tembo

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Kwanini zinaitwa pembe za ndovu na sio za tembo? Ndovu ni nini? Kama ndovu ndo pembe, kwanini hawasemagi amekamatwa na ndovu tu bila kusema "pembe" za ndovu? What if yale ni meno?
 
.
Mkuu KakaJambazi Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI


Kiswahili kwenda Kingereza


Ndovu = elephant.
Tembo = elephant

Kingereza kwenda Kiswahili


elephant = tembo, ndovu


Sasa kukujibu swali lako


Ivory = meno/pembe ya ndovu
.
 
Na kwa kuongezea tu KakaJambazi, hawawezi ita ndovu peke.
Cheki hapa.
Kisawe cha neno Tembo ni Ndovu
Nyati ni Nyumbu
Treni ni Garimoshi n.k
KISAWE: Ni neno lenye maana sawa na maana yenyewe ila lenye kuandikwa na kutamkwa tofauti,na lenye maana hiyohiyo.

SOURCE: Madame B
 
Last edited by a moderator:
Na kwa kuongezea tu KakaJambazi, hawawezi ita ndovu peke.
Cheki hapa.
Kisawe cha neno Tembo ni Ndovu
Nyati ni Nyumbu
Treni ni Garimoshi n.k
KISAWE: Ni neno lenye maana sawa na maana yenyewe ila lenye kuandikwa na kutamkwa tofauti,na lenye maana hiyohiyo.

SOURCE: Madame B

Kisawe cha Nyati ni Mbogo, si Nyumbu. Nyati na Nyumbu ni wanyama wawili tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom