Pembe za Ndovu kutoweka Uganda

utafiti

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
12,783
7,657
View attachment 203552

Maafisa watano wakuu wa mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori nchini Uganda wamesimamishwa kazi kwa muda baada ya zaidi ya tani moja ya pembe za Ndovu zilizokuwa zimenaswa kutoweka kutoka katyika kituo cha serikali.

Pembe hizo zilikuwa na thamani ya dola milioni moja.

Msemaji wa polisi Fred Enanga, amesema kuwa Pembe hizo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwa angalau miaka kumi, zilizpaswa kuchomwa.

Inadaiwa kuwa pembe hizo zilikuwa zitumike kama mtego kwa wawindaji haramu wa ndovu lakini maafisa hoa waliziuza kwa manufaa yao wenyewe.

Shirika la kimataifa la polisi, Interpol lilikuwa limetakiwa kusidia Uganda katika kuchunguza wizi huo, kufuatia wito kutoka kwa Rais kutaka wahalifu hao kuwakamata.

Watano walioachishwa kazi ni pamoja na mlinzi mkuu wa mbuga za kitaifa.

Maafisa wakuu walisema kuwa kama kawaida waliangalia kuona iwapoa pembe hizo zilizokuwa na uzito wa kilo 1,335 zipo katika sehemu ambako huhifadhiwa kila siku, ingawa hawakuzipata dalili ya kwamba pembe hizo zilikuwa zimeibiwa.

Wachunguzi wanashuku kuwa wafanyakazi wa serikali wamekua wakishirikiana na walanguzi kuhusu ambavyo wangezisafirisha pembe hizo

Inadaiwa baadhi ya maafisa wafisadi walikuwa wamesema wanazihifadhi Pembe hizo ili waweze kuzitumia kama mtego kwa wawindaji haramu lakini baadaye wao ndio waliofaidika kwa kuziuza.

Visa vya uwindaji haramu, vimeongezeka kote barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni vikichochewa na biashara ya pembe hizo barani Asia hasa pembe za vifaru ambazo zinadaiwa kuwa tiba ya kienyeji.
 
aisee pembe hizi zinaonekana kuwa na bei sana
Viol usisahau kutunza picha za tembo ili watoto wako waje kuona japo walikua wanaonekanaje hawa wanyama, huenda watakua wanasikia tu story zao ila sio kuwaona
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom